Kafulila watu wameanza kumdharau wamegundua anapitiliza

Kafulila watu wameanza kumdharau wamegundua anapitiliza

Ulivyolitumia hilo neno audacity hapo nathubutu kusema hilo neno hujui maana yake kabisaaa! Umetokea tu kulikariri na huna habari kama ni Kinyantuzu au Kidengereko, pole sana mkuu!
Tumpe benefit of the doubt, anajua maana ya audacity and Kafulila is all that.

Mwache atupe entertainment kwa angle anayotaka.
 
Uzalendo ni kumtetea Rais na Serikali yake,
Sio kutetea nchi, wananchi na rasilimali za nchi husika ?
Kafulila ni Mzalendo wa kweli, Hali Wala hapokei rushwa ila anapiga spana sana
Sasa kama alikuwa anapigia chapio kina ADANI waje kusambaza Umeme wakati wanajulikana kwa Mlungula unategemea hapo alikuwa anapigia chapio kitu gani (ukizingatia historia yao katika umeme hata kwa layman inajulikana)
Kazi ya mwanaCCM yoyote ni kuilinda na kuitetea CCM na Serikali yake.
Kafulila ni kiongozi wa mfano.
CCM ni nani na yanayofanyika na yanayofanywa na hawa walamba asali na madalali yamo kwenye dhima ya CCM (Chama cha Wakulima na Wafanyakazi) ? Au kishabadilika na kuwa chama cha Madalali bila kupeana taarifa
 
🤣
Mkuu jina linaandikwa Two2 au Too2
Either way, he is now a political nuisance.

Kwanini asitulie tu kwenye nafasi yake na kufanya kazi; kuliko kila siku kutokea kwenye media.

Yaani anatokea kwenye media kuliko msemaji wa serikali, CCM, CDM, ACT na wasemaji wa wizara wote combine
 
Yaani anatokea kwenye media kuliko msemaji wa serikali, CCM, CDM, ACT na wasemaji wa wizara wote combine
Zamani wazee walikuwa na msemo 👇
Panya akitaka kutajwa jina hutoka shimoni na kurudi shimoni baada ya kutajwa
 
Hili nimeliona na kuna watu Lumumba wanazungumza.kuwa dogo sasa anaropoka sana. Yeye anataka kuwa Katibu wa Chama kwa maoni ya watu wengi.

Ameanza kukera baadhi ya watu kuwa ana jikomba mpaka anajikomboleza.mwishoni atabakia hana kitu. Wataalamu wanasema pengine ni ushamba na pia kuchanganyikiwa. Alikaa sana juu ya mawe sasa kuja pewa kitengo ni jambo ambalo limemchanganya.

Kwa hali anayoenda nayo wataalamu wanasema siku zijazo atakosa la kuzungumza na watu wata play audio au videos zake kumkumbusha alivyokuwa aki rorojoka. Wanasema aweke akiba ya maneno asiseme akamaliza.

Naona wapinzani kama wameamua kumwacha ili asipate attention na hili ni jambo linaomuumiza sababu anatamani sana apate nafasi ya kupambana aoneshe yeye ni CCM kweli kweli kuliko CCM wenyewe. Sasa wao wanamwacha anaongea peke yake hawamgusi. Hili linamfanya ajaribu kuomba hata midahalo. Wanamwambia yeye hana cheo cha kujadiliana nao. Anaumia.
Huyu jamaa ni chizi pesa za mama zinamchanganya sana.
 
Back
Top Bottom