Toka maktaba :
Mazungumzo ya
Nairobi I na
Nairobi II kuhusu Congo chini ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu utatuzi wa mzozo wa Congo
View: https://m.youtube.com/watch?v=BI5HRv7WVrA
Uhuru Kenyatta, rais wa zamani wa Kenya, aliyeteuliwa kuwa mwezeshaji wa mchakato wa Nairobi na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anatathmini safari yake ya saa 48 mjini Kinshasa tangu Jumapili, Novemba 13, 2022. Pia inashughulikia suala la usalama mashariki mwa DRC.
Mstaafu Uhuru Kenyatta alikutana na mheshimiwa Rais Felix Tshisekedi wa DR Congo na kiongozi mkuu wa MONUSCO (SRSG-Head of MONUSCO), Bi. Bintou Keita .... kuhusu vita inayoendelea na kuona kwa njia gani wanaweza kusaidiana na wananchi wa kabila mbalimbali na jamii mbalimbali mbalimbali
Mwezeshaji wa mchakato wa Nairobi rais mstaafu Uhuru Kenyatta anasema wakutoka nje wenye maslahi binafsi wanawagawa siyo kwa mapendo bali wanaangalia madini kwa manufaa yao na kuwa bunduki na risasi haziwezi kuleta amani juu ya mzozo wa Mashariki ya Congo
Nimepewa jukumu hili na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki EAC kuwa bunduki na risasi haziwezi kuleta ushindi wowote, mimi nimetoka Ethiopia kule wamakubali Tigray na Amhara kuwa bunduki na risasi hazileti amani na ujumbe wangu kwa Congo ni huo huo asisitiza rais mstaafu Uhuru Kenyatta
Jukumu letu kama viongozi ahadi kubwa unayoweza kutoa kwa raia ni usalama wao kwa kuhakikisha hakuna umwagaji wa damu ili watu waendelee na maisha yao ya kujiletea maendeleo
Shida zilizopo zitatuliwe kisiasa na tusiwe na fikra kuwa jamii moja inaweza kushinda pekee bali wakongomani wa aina zote wakae pamoja kwa mazungumzo
Mazungumzo ya mèzani ni muhimu iwe M23 au serikali wote kwa kuweka bunduki chini, njia ya nguvu haitafauli na wala haitaleta ushindi ...