Kagame: Nipo tayari kuendelea kuongoza Rwanda kwa miaka 20 zaidi

Xi Jinping kabla ya kuwa Rais 2013 amehudumu katika ngazi mbalimbali za chini za chama na serikali kwa muda wa zaidi ya miaka 40
 
China Rais pamoja na politburo [ consists Seven members] yote ile haitokei hovyo hovyo wale watu wanapikwa ndio maana wote ukichunguza miaka yao ni kuanzia miaka 50 kuendelea kwa sababu mpaka ufike pale juu lazima utendaji wako uwe bora na lazima ufaulu mitihani ambayo huwa wanatoa China watu wa hovyo hovyo hawakabidhiwi uongozi wa nchi uongozi sio zawadi Bali ni utendaji wako wa kazi ndio humfanya mtu kupata uongozi na kupanda nafasi.
 
Singapore
Sio kweli.

Lee Kuan Yew alikuwa ni dikteta aliyepiga marufuku vyama vingi.

Na alichoma moto nyumba za waliokuwa wanagoma kuhama ili kupisha mipangomiji yenye tija.


Singapore sio ya kuongelea sana. Ukubwa wake ni nusu ya mkoa wa Dar es Salaam huku ikiwa na bandari ambayo ilikuwa namba moja duniani mpaka mwaka 2014 ilipopukiwa na China. Kwa sasa ni bandari namba mbili kwa umuhimu duniani.

Sasa fikiria bandari ya Dar ingekuwa mapato yake yote yanatumika kuendesha "nchi" yenye ukubwa wa nusu ya Dar.
 
Wewe unajua.
 
Mfano wako ni irrelevant kwa nchi Kama US, UK
 
Kajifunze "power struggle" za kumrithi Joseph Stalin zilizotokea USSR alipofariki mwaka 1953, Wakomunisti hardliners walivyotaka kumpindua Gorbachev 1991.

Soma na Jifunze pia power struggle kubwa iliyozuka wakati wa kumrithi Mao Zedong China na jinsi Deng Xiaoping alivyosaidiwa na baadhi ya "wenye chama" cha CCP kuupata ukuu wa chama na nchi kisha akawapukutisha waliomsadia.

Udikteta na Ukomunisti mifumo ya hovy sana ambayo inaiweka nchi rehani kwa migogoro na machafuko wakati wowote.
 
Ziangalie hizi nchi na watawala wake waliodumu kwa zaidi ya miongo miwili halafu uniambie walifanya au wamefanya nini cha maana kwenye nchi zao.

LIBYA- Gaddafi- Miaka 42

Gabon- Omar Bongo- Miaka 42

EQUATORIAL GUINEA - Teodoro Obiang - 41

CAMEROON - Paul Biya - Miaka 38

Togo- Gnassingbe Eyadema- Miaka 38

CONGO REPUBLIC - Denis SNguesso - 36

ZIMBABWE- Robert Mugabe- Miaka 36

ANGOLA-Jose Dos Santos- Miaka 37

UGANDA - Yoweri Museveni -Miaka 34

eSWATINI - King Mswati III -Miaka 35

CHAD - Idriss Deby - Miaka 30

ERITREA - Isaias Afwerki - Miaka 28

BURKINAFASO- Blaise Compaore- Miaka 27

RWANDA - Paul Kagame - Miaka 21

DJIBOUTI - Ismail Omar Guelleh -Miaka 22

GAMBIA -Yahya Jammeh- Miaka 23

Hizi ni baadhi tu, ila zimebaki nyingine nyingi kwenye bara hili zenye viongozi waliokaa madarakani zaidi ya miongo miwili wakaondoka wakiziacha nchi maskini wa kutupwa.
 
Nimekuekewa mwanafalsa, naona una propagate kutawaliwa na mtu ambaye ni dikiteta, au ningesema " dikteta mwema" mwenye maono, kama Mwenyekiti Mao, lakini unajua gharama ambacho wananchi wengi walilipa? Uko tayari kwa hilo? Hebu tupe njia rahisi ya kumpata dikteta wa aina hiyo.....Kwa kura, demokrasia ambayo wewe huitaki,hivyo inabakia ni kutumia nguvu, njia ambayo wewe huitaki.Mawazo au mtazamo wako wa kumpata kiongozo wa ki imla mwenye maono ni vigumu mno katika ulimwengu wa leo ambao binadamu wamefunguka macho, na hawako gizani na tayari wamaisha onja dhana ya uhuru, Huwezi kurudisha gurudumu la kuwatawala watu kimabavu leo, na kusema una maono yako binasfi,huko nyuma iliwezekana. Tusaidie mwanafalsafa jinsi ya kumpata dictator mwenye maono hasa katika nchi za Kiafrika, Nigeria jeshi limejaribu sana kupindua Serikali, na majenerali kuongoza ili wa fix mambo, lakini wakajiona wanazunguka mduara tu! Nchi za kiafrika kwa mtazamo wangu kuanzia miaka ya 60 zilikua na mahali pengi oa kujifunza jinsi ya kuendesha nchi zao, lakini zilishindwa kwa sababu mbalimbali, Nyerere alijaribu akiwa ni benevolent dikteta mwenye maono, lakini hata bila pressure toka nje, modal yake ya kujenga nchi ilishindwa kabisa, aliweza tu kutuunganisha Watanzania, Hivyo modal yako ya kiongozi wa Ki imla naona ni Pata potea, iliwezekana huko nyuma kama nilivyosema, ulimwengu wa leo ni ngumu sana.
 
[emoji1][emoji1] motivational speakers bana.

"To be an enemy of America can be dangerous, but to be a friend is fatal.” — Henry Kissinger
Still simplistic grasp. Kissinger was merely stating a hard fact that’s true of all smart nations. The national interests adage. Nothing motivational about that.

Watch your EAC and it’s intrigues for a lesson.
 
Still simplistic grasp. Kissinger was merely stating a hard fact that’s true of all smart nations. The national interests adage. Nothing motivational about that.

Watch your EAC and it’s intrigues for a lesson.
😄😄 haya tuma salamu kwa watu watatu tafadhali.
 
Naona hujasoma andiko langu lote. Tulia ulisome tena maana nimewaongelea viongozi kadhaa. Ishu sio kukaa madarakani. Ishu ni akili, utendaji, maono na uzalendo.
 
Kanuni ya kumpata hata nikiitoa haitaweza kutumika.

Kwa hiyo ni suala la kusubiri bahati tu siku akipatikana mtu wa aina hiyo afanye mapinduzi.

Dhana za uhuru na demokrasia sio shida. Hakuna anayetaka uhuru usio na mipaka. Na wabishi wabishi wachache huwa hawakosekani, lakini matunda ya uongozi huwa yanatosha kuwanyamazisha.

Mfano Magufuli wapo waliomlalamikia lakini mwisho wa siku matunda ya uongozi wake kwa maslahi mapana ya nchi (badala ya maslahi binafsi ya watu) waliyaona na wakayakubali.

Majenerali sio kwamba ndo wanajua kuongoza. Wengi ni tamaa tu ya kula nchi sio wazalendo.

Mzalendo anakuwa kama Nyerere, yaani kwanza kabisa asiwe na tamaa ya kujitajirisha yeye au kabila lake.

Usiniulize kuhusu kanuni, hili ni suala la kubahatika zaidi kumpata mtu sahihi atakayeweka nchi vizuri. Maana hakuna formula ya kuwa Mkuu wa nchi. Wengi hupiga hesabu za kuupata ukuu wa nchi na huukosa.
 
Hayo yote uliyosema nimekwisha jifunza na kusoma, mahali popote penye mkusanyiko wa watu tofauti lazima ziwepo na mawazo tofauti pia lakini haimaanishi CPC Hakuna migogoro la hasha migogoro ipo kwenye chama chochote kile dunia ndio maana hata hapa Tanzania migogoro ipo kwenye vyama karibia vyote migogoro ipo iyo upelekea kuzaa makundi ndani ya chama lakini kinachotazamwa ni msimamo wa chama kwa ujumla ni upi CUF migogoro ilikuwepo na kupelekea kuzaa makundi mawili Kati ya lipumba na maalim seif, chadema migogoro ilikuwepo ya kimaslahi na kiuongozi mfano mwaka 2015 wakati chadema wanataka kuweka mgombea wa urais kulikuwepo na mgogoro Kati ya slaa na lowasa mbowe na wenzake wanataka kumuweka lowasa mwishoni kitu hiki kilizaa mgogoro chadema uliopelekea Dr . Slaa kuondoka ndani ya chama lakini Mwisho wa siku chadema wakampitisha lowasa hivyo hivyo CCM kulikuwa na mgogoro na makundi Kati ya timu membe na timu lowasa Mwisho wa siku CCM wakampitisha Magufuli . Alafu CPC kabla ya Mao Zedong ajafariki alimuandaa kwanza Deng Xiaoping aje kuwa mrithi wa uenyekiti wa chama na kuwa Rais wa China lakini wakati wa utekelezaji wa sera ya Cultural revolution Deng Xiaoping na Xi Zhongxun[ baba yake na Xi Jinping , Zhao Ziyang na wengineo ] hili lilikuwa ni kundi la Rightist ndani ya chama Cha CPC lilipinga sera hizo za Mao lakini lilikuwa halina budi kuzitekeleza sera .huku Leftist wakiwa wakina Mao Zedong , Zhuo Enlai , Hua Guofeng, Gang of four na wazee wa chama hawa waliunga mkono sera ya cultural revolution ya Mao kwa hiyo Mao baada ya kuona Deng Xiaoping na kundi lake kupinga sera zake mbalimbali ambazo baadae hazikuzaa matunda tokea kwenye sera yake ya awali ya great leap forward 1950s Deng Xiaoping alipinga pia na hii sera ya miaka ya 1960s ya cultural revolution Mao alimuondoa Deng Xiaoping ndani ya chama na akapelekwa jeshini huku baba yake na Xi Jinping mzee Xi Zhongxun yeye alifungwa kifungo Cha nje kilichopelekea Xi Jinping kutengwa mbali kabisa na familia na wazazi wake na kupelekwa maporini vijijini huko kipindi hicho akiwa na umri mdogo tu lakini Wanachama mbalimbali walimuombea msamaha Deng Xiaoping pamoja na Xi Zhongxun wasamehewe na Mao na warudishwe ndani ya chama lakini Mao awali alikataa . Mao akawa amebadilisha mawazo yake na kumuandaa Zhuo enlai awe mrithi wake lakini bahati mbaya Zhuo enlai alifariki mapema kabla ya Mao. zhuo alifariki mwanzoni mwaka 1976 huku Mao yeye alifariki miezi ya mbeleni kwenye huo huo mwaka 1976 baada ya kufa Mao gurudumu la uongozi wa nchi akachuku Hua Guofeng kwa kipindi Cha mpito wa miaka miwili kitu kilichokuwa kibaya kwa Hua ilikuwa ana zihusudu sera za kiuchumi za Mao ambapo alihimiza utekelezwaji wa sera ya great leap forward kwa namna yake tofauti na Mao Zedong kitu ambacho Rightist hawakupenda kwa sababu sera ya great leap forward ilifeli na kuleta baa la njaa wakati wa utawala wa Mao Zedong . Wakati huo Deng Xiaoping yupo jeshini baada ya Mao kufariki Deng akaomba tena arudishwe chamani ndipo msukumo wa kundi la Deng Xiaoping au Rightists ndani ya chama ukapelekea Deng Xiaoping na wenzake wakina Xi Zhongxun kurudishwa ndani ya chama mwaka 1976 na mwaka 1978 ulipofanyika mkutano wa kumchagua mwenyekiti wa CPC na Rais wa China ndipo Deng Xiaoping alionesha nia ya kutaka kuwa rais wa china huku nyuma akipewa support ya jeshi na Rightist ndani ya chama huku Hua Guofeng akiwa na support ndogo ndani ya chama hasa hasa kundi la Leftist wakiwemo gang of four na wazee wa chama Mwisho Deng Xiaoping akashinda na akawa katibu wa CPC na Rais wa china. akaanza kuwapunguza taratibu leftists ndani ya chama bila kukosana nao Ila gang of four aliwafyeka wote kwa kuwa walifanya mauaji ya watu wengi katika utekelezwaji wa sera ya cultural revolution na akaahidi kufanya political reform ndani ya chama Cha CPC kwa kupunguza madaraka makubwa aliyonayo Mwenyekiti wa chama ndipo akawa anakiboresha chama upya wale waliokuwa mstari wa mbele kupinga sera za kiuchumi za Mao ambazo hazikuwa bora walipata wadhifa wa juu wa chama . Zhao Ziyang alikuwa makamu wa Deng Xiaoping huku Xi Zhongxun alipewa kitengo Cha katibu mwenezi wa chama na akapangiwa kwenda mkoa wa Guadong ilipo shenzhen kufanya economic reform na huyu mzee Xi Zhongxun baba yake na Xi Jinping ndipo akaja na wazo la uanzishwaji wa Special economic zones kwenye costal areas ilikukuza uchumi wa china uliodorora chini ya utawala wa Mao Zedong.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…