Nakuunga mkono asilimia 1000 kwani madaraka kupita kiasi hulevya kupita kiasi. Kagame akumbushe kilichompata nduli Idi Amin alipoichokoza na kuichokonoa Tanzania. Awaulize wareno kilichowapata Angola na Msumbiji.
Hawa wanasiasa watawala wa sasa hivi ninachoona wanali compromise tu jeshi letu.
Kuna mambo serikali inanawafanyia wananchi na mifumo ya nchi mpaka wananchi wanaamua kujikatia tamaa na kujiona kama vile wanaishi kwenye nchi yao kwa hisani huku jeshi la Wananchi likiangalia tu.
Unaona kabisa vile wananchi wanajiona wao wenyewe are useles, basi hisia hizo lazima waliambukize Jeshi lao sababu hao wananchi wanakuwa enlisted jeshini wanatokana na wananchi hawahawa mbao wapo demoralized, wanaonyanyaswa, na wenye hofu na wanaohisi wapo kwa huruma tu za wengine..
Jeshi litokanalo na wanainchi wa aina hii kamwe haliwezi kuwa imara. Matokeo yake huku mitandaoni tunabaki kuimba uingo tu mara ooh Jeshi letublimefanya kweli, mara ooh limewafurumusha na kuuchukua tena mji , wakati kule on griund hali haipo kama inavyopambwa mitandaoni.
Tunalipenda sana Jeshi letu, lakini watawala wanaluharibu kupitia mifumo yao ya kuminya wananchi wanaounda Jeshi lile.
Nilianza kuiona thamani ya Jeshi letu kuwa hatarani kipindi cha Mwendazake, Jeshi letu lilidharirishwa na hawa wapumbavu wa M23 kule Congo, vijana wetu wakauawa, Kagame akajiona mshindi. Serikali haikuongea neno, wananchi wakaufyata, miili ya wanajeshi wetu ikapelekwa Tanzania, mazishi ya heshima ya kitaifa yakafanyika Dodoma lakini rais hakuhudhuria.
Mambo kama haya yakitokea watanzania huwa hawaongei. Kutoyaongea haya ni mbaya sana, jeshi hujiona lipo lenyewe, halina wa kuwatetea mwisho litageuka kuwa kama sisi watanzania tulivyo.
Tuache unafiki wa kujifanya tunalishangilia likiwa limepata mafanikio, tuache unafiki wa kulitengenezea matukio ya kishujaa ambalo halijayafanya. Ni Jeshi letu, lazima tujifunze kulipigania, lazima watanzania watambue wana wajibu wa kuilinda brand ya Jeshi letu.
Watanzania ni Jeshi pekee ambalo wamekuwa wakijuvunia, si utalii, si maliasili, si katiba, si serikali, vyote havina msaada, limebaki Jeshi tu ndiyo wanajivunia. Jeshi nalo linapaswa kuhakikisha watanzania wanaheshimika, mifumo yao inaheshimika, katiba na sheria zao zinafuatwa. Jeshi zuri na imara haluwezi likatokana na wananchi wa hovyo.
HIi ni wakeup call kwa Wananchi, serikali na Jeshi lao.