Nakuunga mkono asilimia 1000 kwani madaraka kupita kiasi hulevya kupita kiasi. Kagame akumbushe kilichompata nduli Idi Amin alipoichokoza na kuichokonoa Tanzania. Awaulize wareno kilichowapata Angola na Msumbiji.
Hawa wanasiasa watawala wa sasa hivi ninachoona wanali compromise tu jeshi letu.

Kuna mambo serikali inanawafanyia wananchi na mifumo ya nchi mpaka wananchi wanaamua kujikatia tamaa na kujiona kama vile wanaishi kwenye nchi yao kwa hisani huku jeshi la Wananchi likiangalia tu.

Unaona kabisa vile wananchi wanajiona wao wenyewe are useles, basi hisia hizo lazima waliambukize Jeshi lao sababu hao wananchi wanakuwa enlisted jeshini wanatokana na wananchi hawahawa mbao wapo demoralized, wanaonyanyaswa, na wenye hofu na wanaohisi wapo kwa huruma tu za wengine..

Jeshi litokanalo na wanainchi wa aina hii kamwe haliwezi kuwa imara. Matokeo yake huku mitandaoni tunabaki kuimba uingo tu mara ooh Jeshi letublimefanya kweli, mara ooh limewafurumusha na kuuchukua tena mji , wakati kule on griund hali haipo kama inavyopambwa mitandaoni.

Tunalipenda sana Jeshi letu, lakini watawala wanaluharibu kupitia mifumo yao ya kuminya wananchi wanaounda Jeshi lile.

Nilianza kuiona thamani ya Jeshi letu kuwa hatarani kipindi cha Mwendazake, Jeshi letu lilidharirishwa na hawa wapumbavu wa M23 kule Congo, vijana wetu wakauawa, Kagame akajiona mshindi. Serikali haikuongea neno, wananchi wakaufyata, miili ya wanajeshi wetu ikapelekwa Tanzania, mazishi ya heshima ya kitaifa yakafanyika Dodoma lakini rais hakuhudhuria.

Mambo kama haya yakitokea watanzania huwa hawaongei. Kutoyaongea haya ni mbaya sana, jeshi hujiona lipo lenyewe, halina wa kuwatetea mwisho litageuka kuwa kama sisi watanzania tulivyo.

Tuache unafiki wa kujifanya tunalishangilia likiwa limepata mafanikio, tuache unafiki wa kulitengenezea matukio ya kishujaa ambalo halijayafanya. Ni Jeshi letu, lazima tujifunze kulipigania, lazima watanzania watambue wana wajibu wa kuilinda brand ya Jeshi letu.

Watanzania ni Jeshi pekee ambalo wamekuwa wakijuvunia, si utalii, si maliasili, si katiba, si serikali, vyote havina msaada, limebaki Jeshi tu ndiyo wanajivunia. Jeshi nalo linapaswa kuhakikisha watanzania wanaheshimika, mifumo yao inaheshimika, katiba na sheria zao zinafuatwa. Jeshi zuri na imara haluwezi likatokana na wananchi wa hovyo.

HIi ni wakeup call kwa Wananchi, serikali na Jeshi lao.
 
Baada ya kuondoa vichwa kama Nyerere na Magufuli na kuongozwa na wanaofikiri kwa matummy na mabutty, unategemea nini? Zama za mchonga mdudu kama Kagame wala asingetingisha mkia wake kabla ya kushikishwa adabu.
 
Lakini Ramaphosa hakusema vibaya kwa maoni yangu
Ajibizane na huyu pia 👇

 
Baada ya kuondoa vichwa kama Nyerere na Magufuli na kuongozwa na wanaofikiri kwa matummy na mabutty, unategemea nini? Zama za mchonga mdudu kama Kagame wala asingetingisha mkia wake kabla ya kushikishwa adabu.
Kipindi cha Magufuli ndiyo Kagame alianza kuishika matako Tanzania, Kipindi cha Magufuli ndipo aliua Wanajeshiwetu, baada ya kufanikiwa kutusambaratisha kule ndiyo akapata ujasl wa kupeleka Jesh lake Msumbiji hata baada ya kusikia tupo kule kusaka waasi. Alipeleka jeshi lake wakati kikao cha SADC kikiendelea na kupanga kupeleka Jeshi, yeye akapeleka kivyake akiwa conttracttedna France.
 
Kagame ni kama Mke mdogo au Last born jinsi anavyobehave.
Kagame anabehave kama make mdogo au Last born.
Hawajui west vizuri, ye aendelee kulinda maslahi yao ila wakimchoka ni kama toilet paper tu.
Anauwa waafrica wenzake jwa ajili ya ujinga kabisa na tamaa za kipumbavu.
Nguvu ya kushutumu waafrica wenzake anatoa wapi?
 
Kagame hayuko peke yake ana support kubwa kutoka Kwa mabeberu akiwemo USA.

..hapana.

..Kagame ana unlimited funds za kupigana vita.

..fedha hizo zinatokana na madini yanayochimbwa DRC.

..Ramaphosa inabidi aombe fedha bungeni ndipo aweze kupigana vita.

..pia South Africa ni mbali na DRC kwa hiyo ni gharama sana kupigana vita na M23 na Kagame.
 
Hahaha mnachekesha huyu Kagame na kainchi kake saizi ya mkoa kanaliza mataifa majitu ya Afrika.
Simpendi jamaa ila nakubali sana uthubutu wake.
Hakuna cha uthubutu, ni kwamba mataifa makubwa ni wastaarabu. Hawapendi kuanzisha vita vya kihayawani. Ni aibu Waafrika badala ya kujenga umoja wa kiuchumi tuanze kupigana vita vya kikabila/ mipaka kwenye karne hii ya 21. Wakati nchi za wenzetu zinapiga hatua kiteknolojia na akili mnemba
 
USA ndio anai run hii dunia Kila sehemu ana mkono wake IDF vs Islamists groups, Russia vs Ukraine, Sudan wars , Congo DRc na akiamua viishe ni dk 0 tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…