Kagera (Bukoba) mahali pa ovyo kuwahi kutembelea

Ila kuna vitu kaviongelea zaidi ya lugha..na wengi wamedhibitisha hivyo..so inabidi watu wa huko wajifunze
Kuna makabila au jamii zikiongelewa vizuri humu ndio utashtuka.

Yeah kuna vitu ni kweli ila kuna kukuza mambo kupitiliza na mtu akisikiliza anaweza kuona kama ni sehemu mbovu kuishi kuliko zote Tanzania na wakati mambo mengi aliyoyaongelea yapo sehemu nyingi ambazo zinatawaliwa na wenyeji..

Hapa bongo sehemu ambayo mgeni anaweza fit in haraka ni jamii za kisukuma na pwani kiasi ila the rest ni mtihani
 
Wewe ndio umeishi nao kinagaubaga haswa.

Wageni waendelee kwenda wachangamshwe ama wapotelee Uganda.
 
unafiki na majungu uko sahihi 100% nimekaa kiasi maeneo ya rwamishenye hapo jamaa ni wanafiq sana. wana nafikiana hadi wanafamilia kisa kipato pumbavu sana

ukifahamiana na wenyeji utapata viwanja kwa bei pungufu kidogo
Rwamishenye pande zipi bingwa ? Nimeishi karibu na msikiti wa zamani wa hapo rwamishenye ,nikifanya kazi mjini Ila mleta mada nahisi kila alichosema sidhani Kama kina ukweli 100%.
Maana Mimi nikiwa mgeni wa mji huo Ila ujombani nilisaidiwa na watu wasio hata ndugu kutoka kule na kupanda cheo zaidi bwana Khamis kagasheki na mdogo wake Sued Kagasheki nasalute Sana .

Kuhusu mzunguko wa hela ni kweli uko chini Ila sio habari ya uvivu Ila tujue kuwa Kagera hususani mjini hawalimi wanaishi Kama Dar es salaam Ila ubaya biashara bado hazijachangamka hivyo ni lazima mzunguko wa hela uwe chini
 
It takes a Dead man to recognize one.
 
2005 kuna jamaa “mlangila” aliona fursa akafungua kijiwe cha kitimoto pale jirani na Hospitali ya mkoa kati kati ya mji
Aiseee jamaa alipigwa majungu na wale waislam wa kihaya wanavaa nusu suruali na ndevu wanapakaa rangi ya gold wakiwatumia diwani, mwenyekiti wa mtaa ofisi ya mbunge nk nk

Ilibidi ahamishie kijiwe kule juu kabisa nje ya mji Rwamishenye
Huko weekend ndio tulikua tunakuta “walangila” wote ambao tupo mkoa ule kikazi tunajifariji
Bado na huko majungu yakafika
Aisee jamaa akaitwa hadi na boss wake aachane na hiyo biashara kama anataka kuendelea na kazi Bukoba

Natumini siku hizi vijiwe vya mbusi katoliki vitakuwepo hadi mjini kati

NB
WALANGILA ni jina la watu wasio wenyeji wa Bukoba
 
Bro walangila ni wenyeji wa bukoba na ukisema mlangila unakuwa unamaanisha jamii ya bukoba ambayo ni loyal family .

Specifically kuniita mlangila ikimaanisha mtu aliyezaliwa katika familia za kichifu mfano akina lwekamwa wote wanajiita walangila sababu ni chimbuko la familia ya kichifu
 
Noma sana!
 
Yeah ila ukiwa na akili ya kuwavimbia lazima uwaone wabaya , mhaya mpe nafasi avimbe na kutamba anavyotaka ndio utaona ukarimu wake .
😁😁😁
Bongo tunahitaji sana social skills niamini, tumezoea kuishi kwa aina flani ya maisha kwamba wote lazma tufanane. Kuna mtu alifungua thread kuwa mwanza ni mbaya kwa sababu haina Cinema wala coffee shops. Watu hawana exposure etc

Sasa unajiuliza huyu mtu anataka kila kitu kiendane vile anataka ili mji uwe mzuri. Mimi napenda miji midogo maana huwa ipo peaceful, wenyeji notakavyowakuta ndivyo nitaendana nao. Mbona huwa sipati shida
 
Watu wasio wahaya wanaitwa wanyamahanga mkuu na wengine tulikuwa tukiitwa waswahili 😁😁

Walangira ni wahaya from Royal families, yani watu waliotokea koo za kichief. Au kwa kizungu tungewaita "nobles".
 
Ila mkuu si umeona mwenyewe baadhi ya wajumbe wengine wameunga mkono hoja......na ushahidi juu bado tukaze fuvu tu tukubali tu
 
haahaa
 
Hivi wahaya wa vijijini washaachaga kutandika nyasi chini kama floor kwenye nyumba zao za udongo? Nilionaga ilikuwa fashion miaka ya 2000
 
Funza ni hatari k Funza ni hatari kwa bukoba ,wanatafuna miguu na viganja hatari mzee ,usipokuwa makini ni hatari
 
Eyce natamani ungepita Kwa comment zote ujionee... Ukiangalia vizuri utagundua kuwa wewe ndo PEKEE unajitahidi kuwa positive.. Mimi nakuelewa attitude Yako ila ukweli umeelezwa humu Tena Kwa mifano.
 

Mimi sina cha kuongeza, Najua watakupinga kama mimi nilivyopingwa saana na kushambuliwa baada ya kutoa machapisho mawili kuhusu madhaifu ya Bukoba (Angalia hapa chini)


1) "Uvivu wa kutisha, uchawi (kulaguza), na vijana kuamini kwenye quick gain ni baadhi

ya sababu zilizorudisha nyuma maendeleo ya Mkoa wa Kagera"


2) "Mkoa uliong'aa (THE SHINY BUKOBA) Leo hii Umekuwa Mkoa Mweusi (THE DARK

BUKOBA) kwenye kila sekta ya Maendeleo;Nini Kimetokea kwa Nshomile Hawa

Mimi nilfocus kwenye social cultural issues . Ila watu wa Bukoba ifike mahali, kwanza mtambue hakuna anayewachukia, pili jirani kutaja madhaifu yako ndiyo njia Mubadala ya kukufanya wewe kujitathmini na kubadilika. Hakika nikiangalia majibu ya wachangiaji hasa wale wa Bukoba inaonyesha bado wako kwenye “DENIAL STAGE” na ni ngumu sana kubadilika kama ukibaki kwenye denial stage all the time.







 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…