Kagera: Watoto 10 wamefariki na 6 kujeruhiwa baada ya shule Msingi Islamic Byamungu kuwaka moto

Huu ni ubaguzi ndugu yangu, Natamani ufute hii msg yako
Mkuu sikubaliani na wewe. Kuna trend kubwa sana ya shule za kiislam kuungua moto huko Dar, Same na sasa Bukoba. Why shule za kiislam tu? Kila siku chanzo cha moto wanasema hakijulikani. Walichoma za wakubwa baada ya kuona wengi wanajiokoa wameamua kuhamia za watoto. Hili jambo sio la kuupuzwa. Serikali ikae na makundi yote ya kiislam kuona kuna nini kati yao. Inauma sana kupoteza watoto kizembe namna hii.
 
Mbona shule za kiislam tu?
Kuna kitu nyuma ya pazia sio bule.
 
Kwenye Uislam ikhtilafu zipo nazo ni za kimitizamo ya kielimu. Hizi ikhtilafu zipo tangu kipindi cha Maswahaba mpaka sasa na wala haikuwa na haijakuwa sababu ya kutoana roho ama kuleta maangamivu.

Tunatofautiana mitizamo ya kihoja kielimu kama vyanzo ama Taasisi nyengine zinavyotofautiana kihoja kuhusu masuala ya kielimu.
 
Andika kiswahili basi mkuu. Samahani lakini.
 



Innalillahi wainna ilayhi rajiuun
 
R.I.P wadogo zetu... Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un [emoji120]
 
Shule za kiislam na Moto kulikoni? Mola wape pumziko la heri watoto hao.
 
apa tusi chengeshe maneno hapa, ni Dhahiri kabisa hujuma inahusika hapa na hii si sawa hata kidogo
 
Tatizo lipo kwa wamiliki na serikali kwani lilitolewa agizo kwa shule zote kununua vifaa vya tahadhali ya majanga ya moto na vifaa hivyo vinauzwa bei rahisi inaonekana hiyo shule haikununua hivyo vifaa na pia serikali haijafanya ukaguzi kuhakikisha kama shule zote zimetekeleza agizo lake.
Nawapo pole wote waliofiwana kupoteza mali zao.
 
Kamati ipo ila sijui inakwama wapi kutujulisha sababu ya moto katika shule hasa za kiislamu
Maana haiwezekani iwe ajali za kawaida, sasa sijui wanasubiri nini kuwakamata watuhumiwa
 
Poleni Sana Kwa Msiba.
Majeruhi Wapone Haraka
 
Hoja za waislam kutofautiana zipo lakini hii ipo beyond na tofauti za kiimani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…