Ni usiku (saa nne) wa kuamkia leo Agosti 9, 2022.
Gari ndogo IST inatokea Kahama fresh, inaelekea Tinde. ikaparamia trekta lilokua mbele limejaza kuni halafu halina taa za nyuma wala reflector. Watu watatu wakafa kwenye IST!
Dereva wa Trekta akakimbia!
Wakati uokoaji unaendelea, ikaja Hiace iko full nyomi full speed, kutoka Kahama kuelekea Tinde.
Kufumba kufumbua mbele (kwenye ajali ya Trekta na IST) wametandaza majani, uokoaji unaendelea. It was too late!
Dereva wa Hiace akapoteza control, akakwepa lile Trekta akaparamia Lori lilikokua limepunguza mwendo kupisha uokoaji upande wa pili wa barabara.
Watu 16 wakafa papo hapo (na dereva akiwemo)!
Jumla watu 19!
Majeruhi 15 wamekimbizwa Hospital ya manispaa ya Kahama.
RPC na RC Shinyanga wamefika eneo la tukio Alfajiri.
View attachment 2318712