TANZIA Kahama: Watu 19 wafariki dunia kwenye ajali inayohusisha trekta, hiace na lorry!

TANZIA Kahama: Watu 19 wafariki dunia kwenye ajali inayohusisha trekta, hiace na lorry!

Je hao watu walikuwa wamefunga mikanda? nazungumzia hao wa kwenye daladala maana 16 ni wengi ukilinganisha na hali ya gari inavyoonesha.

Wangekuwa wachache tu watatu au wawili [wa ile eneo ilobondeka tu]

Watanzania tuamke, hakuna gari iliyowahi kutoka kiwandani bila mikanda ya usalama, yaani ni kama tu ambavyo hakuna gari inaenda barabarani bila matairi. Sasa tutabaki kuusema tu mwendokasi lakini haya ni matokeo ya kutumia gari nusunusu. Gari ina taa huziwashi, ina breki huziservice, ina mkanda na hufungi unachotumia ni ile tu ina spidi mia mbili[kumalisa kisahani] hapo lazima matatizo kujiletea.

Tumia gari nzima au achana nayo hakuna cha katikati hapa. Askari nao wafanye kazi yao sio nusunusu, umegundua kosa zuia hadi lirekebishwe. Gari mbovu mtu apaki hadi aletewe breakdown akilipa gharama mara mbili/tatu akili itakaa sawa. Sio gari mbovu unachukua buku tano. Ndo nini sasa? ndo italitengeneza gari au?
 
Matrekta naona Kama yamesahaulika yapo mengi sana barabarani na mengi ni mabovu
Hayana Bima na unakuta Dereva hana Leseni na hizo kuni pia zimevunwa kiwizi.

Ndio maana anatembea usiku wa manane

Hiyo kama hana Bima Trekta iuzwe ili angalao iwe Rambirambi kwa wafiwa japo kiduchu.
 
Uganda walitimua askari barabarani wakabaki wa kuhesabu mmoja mmoja tu lakini suala la ajali ni kitendawili.

Zambia unaweza kutembea kilometers 500 usikutane na askari barabarani zaidi ya watu wa uhamiaji tu na hakuna ajali za kizembe kama hapa kwetu wanapolundikana traffic kila baada ya kilomita 3.

Elimu kwa madereva na wasafiri kwa ujumla ndiyo inaweza kupunguza ajali.

Ama itumike njia ya artificial intelligence ambayo itawaondoa traffic wote barabarani kwakuwa mfumo haudai rushwa kama hawa viumbe.
tunaomba takwimu kwanza ya waganda,barabara na idadi ya traffic ili tulinganishe na hili dude letu lenye maelfu ya kms,maelfu ya magari na malaki ya watumiaji wa vyombo,tabia zetu waafrica zinafanana.

tusijekuwa tunasifia tusivyovijua.
 
Kinana kashasema trafick watolewe barabarani haya ndio wanayataka Acha tuvune tulichopanda juzi nimepanda basi NBS Kutoka Tabora mpk dodoma basi halijasimamishwa ili hali lilijaza watu sana.
Kweni huwa kuna Trafiki usiku wa manane.
 
So sad,hii ajari imesababisha kifo cha mdogo wangu kwenye hiyo IST,laiti ningemkamata dereva wa hilo trekta,ningemtatua malinda bila kalainishi.
Pole sana chief[emoji22]
 
Inaonekana mtu wa hiace Alikua speed 100+. Km/hr
Huenda hata alikuwa 80 kph lakini labda hakuona ishara yoyote na huenda huyo mwenye Lori hakuwasha double hazzard au hata kumflashia taa ili dereva wa Hiace ashtuke.

Kumbuka Nchi hii inawatu wenye roho mbaya mabarabarani wenye kupenda kuona damu wakiona Mbwa au vinyama vingine vya mwitu wanahakikisha wamevigonga na kuviulia mbali.
 
Polisi waache kuisikiliza CCM

28 July 2022




29 July 2022

 
Inanikumbusha boda boda mmoja pale mapinga.
Kuna Lori la cement limetoka kushusha likagongana na gari la maji la afya.njia ikawa imefungwa na hayo magari.ilikuwa usiku sana.yule bwana na haraka zake yuko speed balaa watu wanammulika tochi lakini wapi.asikii Wala haoni akaenda kugonga ubavuni mwa gari la cement akalala juu .na kiuno akateguka.
Tuweni makini madereva mwendo kasi haufai
Mkuu hapakuwekwa viashiria vya ajali? Huenda boda alihisi ni majambazi mnataka kumteka na hzo tochi zenu!
 
Waanzishe kikosi cha kukagua barabara, na mtu gari likiharibika atakiwe kisheria mbali ya kuweka triangle au majani barabarani basi mwenye chombo atakiwe kuliondoa haraka barabarani au kikosi cha patrol wafike haraka kuliondoa na kumtoza gharama ya kulivuta / kukiondoa chombo kilichoharibika barabarani.


Hata kama polisi wakifanya patrol lakini hawawezi kuwa kila sehemu gari ilipoharibika kwa wakati. Gari inapoharibika, dakika tano tu ni muhimu sana.

Tujiulize nchi zilizoendelea kama za Marekani ya Kaskazini, Ulaya, Japan, Australia na China kwa kuzitaja kwa uchache wana vikosi vya doria vya usalama wa njia kuu / highway patrol iwe vipi nchi ya Tanzania ishindwe na kukosa kuona umuhimu wa kikosi cha doria cha usalama wa barabara kuu ?

Bonus Scene : Always On Patrol I Heavy Rescue : 401


Law enforcement on the 400 series highways is a massive task. The Ontario Provincial Police responds to calls big and small - all of them vital to making the highways safer.
Source : Discovery Canada
 
HITAJI KWA JESHI LA POLISI KUJIKITA KUFANYA DORIA KUONDOA MAGARI YALIYOHARIBIKA BARABARANI

Mfano mafunzo kwa askari wa usalama barabarani na vikosi vya uokozi vya zimamoto kufika haraka eneo la tukio ili kuondoa magari yaliyoharibika barabarani ili kuzuia ajali kutokea.

Askari wa usalama barabarani walazimishwe kisheria ku patrol barabara na kuhakikisha magari yaliyoharibika barabarani yanaondolewa haraka na pia madereva kulazimika kisheria kuripoti kuhusu magari yao yaliyoharibika barabarani ili vyombo husika kama askari wa doria wa usalama barabarani/ magari ya breakdown/ zimamoto n.k wafike na kuyatoa au kuyakokota kutoka ktk barabara ili kuepusha uwezekano wa ajali iwe usiku au mchana au mvua inanyesha au jua kali lipo.

Pia kuna ulazima wa haraka bunge kuja na muswada wa dharura ili serikali kuunda kikosi maalum cha highway patrol ambacho kazi yake kubwa ni kuhakikisha usalama ktk njia zote kuu za usafiri, hiki ni tofauti na trafiki wa usalama wa barabarani katika miji.

Serikali imewekeza sana ktk miundombinu barabara za lami hivyo hitaji la kikosi cha doria cha barabara kuu ndiyo wakati umefika maana wanaotumia barabara wameongezeka na changamoto pia .

Rescue teams train to keep drivers safe by clearing accidents on AZ roads

First responders are trained to handle bad accidents quickly and safely. Here's an inside look at how rescue teams prepare for dangerous road situations.
 
Naunga mkono lakini ungekuwa ni mtumiaji barabara wausiku ungeelewa namna wajinga wa matrekta, pikipiki na baiskeli za kubeba mkaa zinavyo leta shida. Hasa barabara ya Dar - Mwanza, Tinde - Kahama. Pia taa za booster kwenye Fuso na gari ndogo ni balaa.
 
Back
Top Bottom