Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Watanzania nani katuroga?

Ina maana hao ndio watu wa kwanza kuchuchumalishwa?

Mkuu au na wewe ulipewa marbolo yenye wekundu wekundu?

Ndio maana tunashuhudia viongozi wetu wanafanya mauaji hadharani na kupewa adhabu ndogo tu ya kulipa pesa kidogo ila kosa hilohilo akifanya mlalahoi adhabu yake ni kifungo cha maisha.

Watanzania tuna unafiki sana.

Nchi za wenzetu hawa jamaa washenzi na wale waliopokea magunia yaliyojaa pesa ilitakiwa wapigiwe risasi mbele ya watu mchana kweupe.

Tanzania sheria zipo kuwahukumu masikini sio matajiri.

 
MBONA HII AFADHALI KULIKO KUNYEA DEBE? UMESHAWAHI KUELEZWA KUONA AU KUSIKIA JUU YA HILI? MBONA LUPANGO ZA WENZETU HAWAFANYI HAYAA WANA VYOO VYA KIBINADAMU? WAHANDISI WETU WAMESHINDWA KUWEKA VYOO SALAMA
 
Umesema ya ukweli Paskali lakini tatizo kubwa watu hapa hawatakuelewa maana wewe ulikua mtetezi wao mkubwa huko nyuma hivyo watu watadhani kuna maslahi gongana japo unaloliongelea ni la kweli. Halafu pia umesahau uzi uliouandika juu ya fedha za ESCROW siyo za umma.
 
Nina wasiwasi ni akili yako
 
Mkuu chukua Kilimanjaro moja hapo ulipo kwa bili yangu.
 
Pascal Mayalla

Mvunja sheria/katiba mkuu ni huyo huyo umsifiaye humu kila uchwao na Taasisi nyingine zote zinajifunza kwake.

Imeonekana hiyo ndiyo style pendwa ya awamu hi, acha double standards.


Yaani unajisahaulisha kabisa dhalili mbaya zisizomithilika wanazofanyiwa watuhumiwa wamakosa mbali mbali?

Wale mashekhe wanateswa na kudhalilishwa kuliko kawaida lakini hadi Leo hii "uchunguzi haujakamilika", Wale Waliotajwa na Makonda kwenye hekaya ya "dawa za kulevya" (Yule unayetaka awe Rahisi ajaye baada ya pombe), Wabunge Wa Upinzani Wanadhalilishwa mno ndani ya Bunge yote hayo huyaoni.

Sizonje anataja taja majina ya watu hovyo hovyo huku akiwa "brand" hatia mbali mbali hata kabla hawajafikishwa mahakamani, hayo uliyafumbia macho sasa wameguswa wenye nazo umekurupushika kuleta "uzi gazeti" la kupinga udhalilishaji.



Tuvumilie hii ndio style pendwa ya awamu hii kila taasisi inatafuta "kiki".
 
Kaka Pasco , nimekusoma
Katika hili andiko lako iko hoja ya msingi ,ambayo kwa bahati mbaya watu wengi hawataiona . Hii inatokana na hisia mbalimbali ambazo zimejikita katika mioyo ya watu wengi kwa sasa. Katika kipindi hiki unapojaribu kukosoa jambo fulani lazima uwe makini sana , vinginevyo unaweza kuonekana unatetea wahujumu uchumi.

Lakini kuna kitu pia nimejiuliza. Je hii ni mara ya kwanza watu kupigishwa magoti pale Kisutu? .Mbona kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa tabia hii wamefanyiwa watu wengi sana? , je kwa nini tulikaa kimya mpaka hawa matajiri wanapigishwa magoti?

Kaka Pasco huoni kwamba watu wanaweza kutafsiri kuwa tumeongea kwa sababu labda wapendwa wetu wameguswa na hii aibu?

Nataka kusema kuwa kwa mda mrefu sasa katika jamii hii kumekuwa na tabia ya watu kudhalilishwa tena mbele ya kamera za waandishi wa habari halafu hakuna mtu anayeshituka na kukemea udhalilishaji huo. Sasa imeanza kuonekana kumdhalilisha mtu ni ushujaa katika jamii hii.

Juzi tu tumeona matukio ya walemavu wakipigwa mbele ya kamera za waandishi wa habari , hakuna mtu aliyekemea hali ile. Leo katika jamii yetu imeanza kuonekana chuki ya wazi kabisa hata katika misiba . watu wanachukiana kwa kiwango ambacho hajiwahi kuonekana katika Taifa .

Hii tabia ambayo leo mimi nina nguvu naweza kufanya chochote haitasadia taifa hili hata kidogo. Kwa kipindi hiki tumeona baadhi ya watu ambao hapo awali walipokuwa na nguvu waliweza kufanya chochote dhidi ya wenzao. Lakini leo hii na wao yanawakuta yale yale waliyowafanyia wenzao kipindi wapo madarakani. Tujifunze kukemea uovu katika jamii tusisubili yatukute sisi kwanza ndio tuseme.
 
Pasco nzi wa kijani hawakawii kukupiga chapa ya utetezi wa mafisadi.
 
I felt heart sick nilivyoona Mzee Rugemalila akipiga magoti na rozari yake.

Hakuna asiye mdhambi, hakuna apendaye kudharirishwa. Hakuna mkamilifu.

Wakipatikana na makosa wahukumiwe ila si busara kuwadharirisha.
 
Mbona umewaona hawa tuu?wakiuliwa watuumiwa wa ugaidi upo kimya masheikh wanapigwa picha wanadhalilishwa mbele ya haki nyie kimya why hawa??
 
HIVI KWANINI MAGU HAMTEUI JUDGE MKUU. MWAKA WA PILI SASA. MAANA ULE NAO NI MUHIMIRI WA SERIKALI AMBAO UNATAKIWA KUWA NA KIONGOZI WAKE ILI KUSAIDIA CHECK AND BALANCE
 
Sasa Kama mawazo ya nchi yameshikwa Mabashite unategemea nini ? Tupo kwenye show off tukimaliza tutarudi kwenye code of conduct.

WEZI WEZI HATA KUWAUWA SAWA..HAWANA FAIDA
 
Paskali, utawala huu unavunja kstiba, sheria, taratibu and everything you can think of.. the list is endless!
It is a pity kuwa hata Mkuu akivunja hayo, watanzania tunashangilia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…