Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Nyie watu sijui mnaakili gani ?!!

Sisi ndugu zetu wezi wa kuku kila siku wanadhalilishwa lkn kuonekana picha hizi ndio mnajifanya mnaumia....

Hawa ni wahalifu, utaratibu uendelee kama kawaida.
Wewe ndio ujiulize una akili gani!! Paskali hapa anakumbusha tu kwamba sheria ipo lakini haifuatwi, hata hao wezi wa kuku hawatakiwi kudhalilishwa.
 
sheria nyingi,taratibu na kanuni tumecopy kwa wakoloni,nao waliturishisha kwa makusudi ili tusipate maendeleo, huo ustaarabu gani wao wahalifu wanafanya kutufanyia uhalifu alafu sisi hata tusiwaone ................wacha wakinyweee
 
Mkuu pasco siku zote watuhumiwa wanafanyiwa haya inamaana hujawahi kuona? Au Leo mabilionea wametendewa ndio kelele zinapigwa? Watuhumiwa wengine wa kila siku wanafanyiwa haya hawana haki hizi
 
Nakubaliana na mtoa mada, kosa ni kosa haijalishi kafanyiwa nan iwe Kina TID na wenzie au Rugemarila na mwenzie, ni kinyume cha utaratibu wa sheria na taratibu ambazo tunazifata kama nchi, ukiangalia Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 inakataa vitendo vya udhalilishaji kama hivi..Tukiendelea kunyamaza ni kulea kosa
 
Tafuteni vyakutetea
Tusifiche makosa yetu kwenye makosa ya wengine.... THE FACT KWAMBA KAKUIBIA, HAKUKUPI HAKI YA KUMUUA, KUMDHALILISHA, AU KUFANYIA CHOCHOTE KIBAYA... sheria inasema au inatamka namna ya kushughurika na wezi, majambazi na wanaovunja sheria mbalimbali
 
Wanatafuta kiki kwa pikipiki,ama white ama black vip.
Nakumbuka Ruge alipolipwa bilions zile na kununua Royce rollyce mupyaaa kabisaa ya karatasi na kukodi ndege ya kuileta mpaka bongo,sasa nadhani litataifishwa.
Haya Matatizo ni mabaya kuyakabili ktk umri wa hawa Wazee,maana pressure,kisukari,kiharusi ni fasta kuwasumbua.kutokana misukosuko ya watu wa usalama.Ni kuwaombea tu wakiri kurudisha mambo yaishe basi.
 
Paskali,

Tuache unafiki. Hebu niambie ni waTanzania wangapi wanaodharirishwa tena zaidi ya hao walioambiwa kuchuchumaa and no body cares?

Tuache huu unafiki. watu wamepiga kelele jinsi wafungwa/mahabusu wanavyokuwa treated, jinsi magereza yalivyo machafu but no body cares. hata sidhani kwenye bajeti kuna mbunge anasimama kuhoji magereza yanaendeshwa vipi. Leo singa singa ameambiwa achuchumae chini unaandika thread ndeefu kwamba amedharirishwa? Human rights zinakuwa human rights for the rich and stronger but not for the poor and the wretched of the earth? Si ndiyo?

Ngoja tusubiri tuambiwe kwamba inabidi wajengewe gereza lao maana yaliyopo ni machafu.

Kaka yangu Paskali, wazungu wanasema: If the society cannot protect the weak in its midst, what makes you think that they will protect the stronger when times come?

All I can say: Tupige kelele wee..lakini Magufuli anatufundishia watoto kitu kimoja muhimu sana (it may be late for me and you) kwamba CRIME DOESNT PAY! Tufanye kazi kwa bidii tule na kuridhika na tunachopata kwa halali. Mengine ni porojo.

Masanja
Mkuu na wewe umechukuliwa na hisia, haya mambo huwa yanapingwa sana hapa yanapoonekana, wanyonge wanapodhalilishwa picha zao zika trend watu wanakemea, anaweza kuwa sio pasco muanzisha uzi ila haimaanishi kuwa sio concerned,

Kuna nyuzi nyingi za kuwatetea wanyonge wanapoonekana wamedhalilishwa, mfano wale madereva waliopita barabara za mwendokasi kupigwa picha wameshika mabango, walemavu kupigwa na polisi (hii ipo ina trend hadi leo), na picha zao kutupiwa mtandaoni, watu wlilaani sana hilo, kuna mtoto wa Kenya kupigwa picha kashikishwa bango la kumwita mwizi lilipigiwa sana kelele pia na Pascal Mayalla alilianzishia uzi

Bango la "Mwizi Mkenya!" Mlimani City ni Ubaguzi!, Udhalilishaji!, na Very Undiplomatic Gesture!.

Polisi waanza kutekeleza adhabu "kali" kwa madereva wanaovamia barabara za mwendo kasi
 
Paschal hajawahi kutoa dukuduku kama hili kuwatetea wanyonge wanapodhalilishwa na polisi....but this time tycoons wameguswa ndio anajua kuwa polisi wamevunja sheria.
 
Khaaaaa...hawa majizi ni stahili yao hiyo..Tena haitoshi walipaswa kutembezwa uchi...Wezi wa kuku wanafungwa jela au wengine wanachomwa moto..hawa wanapaswa kuchomwa mishikaki
 
Bro napingana na wewe... kule Afrika Kusini ile kesi ya Oscar Pistorious mbna ilikua inarushwa live na mtuhumiwa anapigwa picha kabisa?
 
juzi tumezungumzia swala la raia wa Tanzania kukamatwa kwa kupiga picha za maiti huko mbeya kwa kuwa mtindo huu unaendelea huku muda mrefu wewe ukiwawakilisha waandishi wahabari wenzako waelimishe wasiweke picha za udhalilishaji badala ya kuwalaumu polisi pekee kwani hapo wahusika ni polisi, magereza na hao waliopiga picha
 
Na iweje uneoneshwa kukerwa na tukio hili la hawa mafisadi? If you're genuinely against this culture, kwanini usingeprotest kipindi kile wale wasanii wa bongofleva walivyo fanyiwa the same thing, probably the worse thing than hawa mafisadi?
 
Back
Top Bottom