TANZIA Kaka wa Freeman Mbowe, Charles Mbowe afariki Dunia

TANZIA Kaka wa Freeman Mbowe, Charles Mbowe afariki Dunia

Jambo la heri kwa nani? Uliwahi kumsikia marehemu kabla ya umauti kumkuta? Uamzi wa kutoa sababu za kifo cha mtu yeyote asiyekuwa public figure ni wa familia na hamna mtu mwenye haki ya kulazimishataarifa hiyo itoke. Hapo uliko bila shaka umeishawahi kufiwa na watu wako wa karibu na hatujakusikia ukija JF kutoa taarifa zao na sababu za kifo chao...

Soma kuelewa.

"Jambo la kheri" ni kauli ya kiswahili kilichokomaa kuwa "bila shuruti, ushawishi wala hiyana."

Usikonde lakini. Kiswahili kilizaliwa Pwani.

Apumzike kwa amani Charles Mbowe.
 
Taarifa zilizotufikia kutoka Chadema zinaeleza kwamba Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho amelazimika kukatisha kampeni za operesheni haki huko Zanzibar na kurejea Tanganyika baada ya kupokea taarifa za kifo cha Kaka yake aitwaye Charles Mbowe...
Rip Charles na pole Kamanda Freeman. Bwana alitoa na sasa ametwaa. Amen.
 
Na mimi sikuzaliwa pwani.

Amandla...
Mkuu hapo una debate na psychopath anayeiwaza Corona masaa 24. Anatamani kila anayekufa isemekane ni COVID. Thinking capacity yake ipo very low na mbaya zaidi hajui. Huwezi kulazimisha uambiwe marehemu kafa kutokana na nini wakati haikuhusu na sio mwana familia na bado hakuelewi. Achana nae..
 
Duu! Pole nyingi kwa kamanda Mbowe na familia ya marehemu! Mwenyezi Mungu ampuzishe kwa Amani!
 
R .I P Charles Mbowe. Kwenye vifo tunaweka uvyama pembeni.
 
Apumzike kwa amani kaka wa Kamanda wetu Mungu akawe mfaliji mwema wakati huu mugumu kwa wana family
 
Pole nyingi kwa familia na watu wake wa karibu.

Tuendeleeni kuchukua tahadhari zote wakuu, hili wimbi la tatu litatumaliza.
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na awape nguvu faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao. 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Kama ni Uviko, familia ya Mbowe haiwezi kuficha, itaujulisha umma. Maradhi na kifo, siyo vitu vya aibu, hakuna aliye na uwezo wa kuvizuia.

Pole sana Mwenyekitibowe, poleni wanafamilia wote na watu wa karibu na marehemu.

Mungu wa huruma awajalieni moyo mkuu wa kuyapokea mapenzi yake kwa unyenyekevu,
Vipo vifo vya aibu, mtu kama kafia kifuani huko gesti kwa kuzidiwa na utamu utakuja kutangaza na kusema kifo si kitu cha aibu?
 
Back
Top Bottom