TANZIA Kaka wa Freeman Mbowe, Charles Mbowe afariki Dunia

TANZIA Kaka wa Freeman Mbowe, Charles Mbowe afariki Dunia

Taarifa zilizotufikia kutoka Chadema zinaeleza kwamba Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho amelazimika kukatisha kampeni za operesheni haki huko Zanzibar na kurejea Tanganyika baada ya kupokea taarifa za kifo cha Kaka yake aitwaye Charles Mbowe.

View attachment 1845577

Kwa niaba yangu binafsi na familia yangu na kwa niaba ya wanajf wote , nachukua nafasi hii kumpa pole kamanda Mbowe na ndugu zake kwa msiba huo .

INNALILLAH YA INNALILLAH RAJUUN .

View attachment 1845579
Poleni Ndugu , Jamaa na Marafiki.

Charles Mbowe ndiyo mwenye Mbezi Park?
 
Corona au
Nauliz hivyo kwa sababu vijana wa chadema huwa mnadhani wale wafuasi wa CCm wanaokufa wote ni kwa kutofata taratibu za kujikinga, pia wote wanaokufa ni corona.
Na mmekuwa mkitoa pole za kejeli je huyo nae hakupata chanjo?
Nawapeni pole makamanda ila kifo hakina chama wala mjanja.
Muwe na staha wanapokufa wa upande mwingine kwani wote ni binadam.

Nasema hivyo baada ya kifo cha yule diwani pale moshi, kuna comment humu zulikua zinakera.

Corona ni ugonjwa unaiuwa kama yalivyo magonjwa ya moyo, figo, kansa nk. Ugonjwa uliomwondoa marehemu haubadiliki kwa kuupa jina jipya:

IMG_20210708_121816_467.jpg
 
Uviko au?
Kama ni Uviko, familia ya Mbowe haiwezi kuficha, itaujulisha umma. Maradhi na kifo, siyo vitu vya aibu, hakuna aliye na uwezo wa kuvizuia.

Pole sana Mwenyekitibowe, poleni wanafamilia wote na watu wa karibu na marehemu.

Mungu wa huruma awajalieni moyo mkuu wa kuyapokea mapenzi yake kwa unyenyekevu,
 
Kifo ndio mwisho wa kila kiumbe chenye uhai,kifo ni ukumbusho kua hii Dunia ni mapito tu.

Poleni sana,
marehemu mwendo ameumaliza.
 
Taarifa zilizotufikia kutoka Chadema zinaeleza kwamba Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho amelazimika kukatisha kampeni za operesheni haki huko Zanzibar na kurejea Tanganyika baada ya kupokea taarifa za kifo cha Kaka yake aitwaye Charles Mbowe.

View attachment 1845577

Kwa niaba yangu binafsi na familia yangu na kwa niaba ya wanajf wote , nachukua nafasi hii kumpa pole kamanda Mbowe na ndugu zake kwa msiba huo .

INNALILLAH YA INNALILLAH RAJUUN .

View attachment 1845579
poleni kwa msiba, pole mheshimiwa Mbowe
 
Apumzike kwa amani Charles Mbowe.

Familia ya Mh. Mbowe ionyeshe mfano kwa kuweka sababu za kifo hadharani na kwa uwazi.

Mola awape nguvu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
Hazituhusu.

Charles Mbowe hakuwa public figure. Ni ndugu wa mwanasiasa lakini sio mwanasiasa mwenzake. Muache apumzike kwa amani.

Amandla...
 
Hazituhusu.

Charles Mbowe hakuwa public figure. Ni ndugu wa mwanasiasa lakini sio mwanasiasa mwenzake. Muache apumzike kwa amani.

Amandla...

Apumzike kwa amani Charles Mbowe.

Kuweka wazi sababu ya kifo cha binadamu yoyote ni jambo la kheri kuliko kuvumbua jina jipya la ugonjwa na kumvesha marehemu.

Ugonjwa uliomwua marehemu haubadiliki kwa kuupa jina jipya.
 
Poleni sana familia kubwa ya kina Mbowe, ndugu, jamaa, marafiki na waTanzania.

RIP Charles Mbowe.
 
Apumzike kwa amani Charles Mbowe.

Kuweka wazi sababu ya kifo cha binadamu yoyote ni jambo la kheri kuliko kuvumbua jina jipya la ugonjwa na kumvesha marehemu.

Ugonjwa uliomwua marehemu haubadiliki kwa kuupa jina jipya.
Jambo la heri kwa nani? Uliwahi kumsikia marehemu kabla ya umauti kumkuta? Uamzi wa kutoa sababu za kifo cha mtu yeyote asiyekuwa public figure ni wa familia na hamna mtu mwenye haki ya kulazimishataarifa hiyo itoke. Hapo uliko bila shaka umeishawahi kufiwa na watu wako wa karibu na hatujakusikia ukija JF kutoa taarifa zao na sababu za kifo chao.

Msipende kuwa na tabia za u voyeur. Sababu za kifo za marehemu hazitusuhusu na ibaki hivyo hivyo. Zitoke tuu kama ndugu zake wataona kuna haja ya kuzitoa na sio kwa shinikizo la keyboard warriors wa JF.

Amandla...
 
Back
Top Bottom