Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 3,474
- 3,744
20 May 2024
Ikungi, Singida
Ukoo pia wanakijiji wameamua baada ya kuligusa gari na yale matundu ya risasi watafanya tambiko la kijadi
View: https://m.youtube.com/watch?v=w8L0W7rtMX8
Msemaji wa familia ya ukoo na pia kaka wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Mh Tundu Lissu, advocate Bw Alute Simoni Lissu Mughway mjukuu wa Muro baada ya kumaliza shughuli za kijadi za kiukoo, mbele ya ukoo amesema suala la madai ya Tundu Lissu ...
Advocate Bw Alute Simoni Lissu Mughway mjukuu wa Muro azungumzia ujasiri uliopo katika ukoo wao na kutoa mfano babu yao alivyoua simba jike kwa mkuki akiwa pekee yake machungani .... na kama inavyofahamika simba jike ni mkali na mtata kuliko dume ...
Pia gari la Tundu Lissu limekaguliwa na ndugu kuona matundu zaidi ya 30 ya risasi za waovu wale waliotaka kuondoka na uhai wa Tundu Lissu na ukoo pia wanakijiji wameamua baada ya kuligusa gari na yale matundu ya risasi watafanya tambiko la kijadi ...
Advocate Bw Alute Simoni Lissu Mughway mjukuu wa Muro amesema tambiko ni muhimu na kumsifia Tundu Lissu kuweza kuendeleza msimamo wake pamoja na majeraha pia vitisho anavyopitia makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara mheshimiwa Tundu Lissu ...
HAKI HUINUA TAIFA