Huu ni ukweli. Badala ya Watanzania wote kuungana pamoja wote kukemea huu uhuni sababu yoyote anaweza kutekwa kutoka chama chochote, dini yoyote, kabila lolote.
Utakuta watu kadhaa wananzisha mjadala wa kwamba Polepole hakuwa na strategy, Polepole ni mjinga, Polepole angekuwa nje ya nchi, Polepole alihusika na utekaji wakati wa JPM, machozi ya mama Polepole siyo ya ukweli, Polepole amekufa ingawa bado hatuna taarifa hizo na tukipiga kelele bado wanaweza kumuachia.
Kuna watu inaonekana moyoni mwao wanasukumwa na udini, Uzanzibari, waendelee kulamba asali, wengine ni wabishi by nature wanatafuta umaarufu, roho mbaya wanafurahi yoyote aliye juu kushuka.
Wanawasaidia genge la watekaji kwa kuwagawanya watu, divide and rule, kupunguza pressure, kuwapa mambo mengine ya kujadili distractions badala ya mambo ya msingi kwa sasa.