#COVID19 Kaka yangu amefariki kwa ugonjwa wa CORONA

Poleni sana, leo mimi najisikia ovyo kweli nimetapika angalau najisikia nafuu sijui ndiyo yenyewe dah
Yenyewe hiyo, delta one mkuu, uchovu, kuharisha, kutapika,koo kuuma,,
Poleni sana,,hali ni mbaya mno
 
Sayansi ilitumika kuchapisha Biblia, kujenga makanisa, kusafirisha waumini na wachungaji, vipaza sauti, vyombo vya muziki etc...
Hivi kwanini unajitoa ufahamu na kusema dini na sayansi vikae separately?
Chanjo ni muhimu acheni upuuzi wenu!
 
Pressure Na uoga inawezekana ikawa Ndo sababu.

Akawa kama ametengwa hospital bila kupewa Huduma.

Pole sana
 
Alivyo kuwa akisema Freeman Mbowe tena akitoa mifano hai kuanzia Mwanawe Dudley na hata karibuni tu alivyo zungumza kumpoteza Kaka yake Charles Mbowe na kuomba taifa lichukue tahadhari,alidhihakiwa sana tena humu humu kwa wana JF wenzetu, anyway MUNGU atuvushe na kutunusuru katika janga hili
 
Poleni sana. Halafu wakina Gwajiboy na kundi lake wanahubiri funza kuhusu chanjo, kaka yako alikuwa ni mzee??
 
Pole sana huko Hai hali ni mbaya sana.. Ibada moja misiba 9
Your browser is not able to display this video.
 
Hii kitu inawatokea wengi,ila ukijipeleka kwa matabibu inakuonesha adabu.
Chamsingi ukijiskia umechoka jilazimishe kutembeatembea,kula matunda kwa wingi,ondoa hofu ,baada ya mda mfup utaona nguvu zinaanza kurejea
 
Katika watu bado wabishi kuamini ili gonjwa lipo na linakata watu ni wasukuma jamani.nipo nao kanda ya ziwa ukimwambia ukweli hana kuambia angekuwepo magufuli haya yote yasingekuwepo [emoji23].
Sasa gonjwa linasubiria mtu
 
Huyo alikua na magonjwa mengine either kisukari au HIV,
Mkuu hii ya sasa imekuja kivingine nimempoteza mdogo wangu wiki iliyopita dada wa miaka 40 Hana sukari Wala HIV She was health aliwekewa oxygen siku 2 tu na nilikuwa nae emergency siku zote hizo tunazungumza anakula lakini alizidiwa ndani ya dk tano tu na kufariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…