Mkuu,kuchepuka ni uamuzi wa mtu. Kuna watu huwa wanajitoa kwa wenzi wao hadi kujimaliza lakini wenzi wao bado sio waaminifu. Mimi kwakweli kama huyo mwanaume anaona sijafika viwango anavyovitaka kiasi kwamba anahitaji kutoka nje,anambie tu safari yetu ivunjike ili aende kwa yule anayefikisha viwango anavyovitaka yeye. Kwangu mimi ndoa ni all or nothing, ni aidha tupo kwenye ndoa miguu yote au hatupo. Mambo ya tupo kwenye ndoa halafu anaenda kwa wengine hiyo sio ndoa tena ni biashara huria,mimi hicho chama cha biashara huria sitaki kujiunga. Kama anaona sifiki viwango vyake, kama anaona simpi amani,kama anaona mimi sio mke bora, anambie mi nipishe ili awe na yule anayefikia viwango vyake na kumpa amani tena awe nae kwa uhuru sio kwa kujifichaficha maana michepuko huwa inafichwa.
Ndoa zina matatizo sio kila siku ni furaha lakini suluhisho la matatizo sio michepuko, kama tunakoseana tunaongea tunasuluhisha,ikifika hatua matatizo ni magumu hadi inabidi mtu atoke nje basi hakuna ndoa hapo.