Kaka zangu nimekuja tena kwenu kuomba ushauri wenu kwa habari ya kusalitiwa/Cheating

Kaka zangu nimekuja tena kwenu kuomba ushauri wenu kwa habari ya kusalitiwa/Cheating

Nlkushauri uzi wa mwanzo,sikiliza kwa Makini:

Usaliti hauvunji ndoa
Kukosekana kwa penzi ndio kunavunja ndoa
Ndo mana nikasema mimi mume wangu akichepuka nitamuacha endapo tu nitajua mapenzi alonayo kwangu yamehamia huko anakochepuka.
 
Niende moja kwa moja kwenye Ushauri;
Ukiwa na hakika mume wako anacheat; mpikie chakula kizuri anachokipenda hasa wikiendi. Akisha kula akashiba kabisa; mueleze hizo taarifa kwa upole na jinsi zinavyo kuumiza. Na unavyo hayo mahusiano yake mapya yataweza kuharibu hata malezi ya watoto. halafu Nyamza usirusie hata wiki nzima.
Amini usiamini...dawa ya moto ni maji...
Asante kwa somo.
Akiongea mwanaume kuhusu uanamme nasikiluza kwa makini.

Ujue mkuu hakuna binadamu me au ke anapenda kusalitiwa.Inauma sana ila mimi naamini kuna aina mbili za usaliti upande wa wanaume.

1)Mwanaume anasaliti sbb ana tabia mbaya tu za kimalaya.
2)Usaliti wa kuzidiwa kwa sababu za kimaumbile.

Pamoja na kwamba usaliti ni usaliti tu hata uwe wa aina gani ni mbaya ila mimi naona kuna kitu hakipo sawa(kwa sisi wanawake) kuhusu maumbile ya mwanaume.Sijui sayansi inasemaje kuhusu hili ila naamini wakristo na waislamu walipaswa kuruhusiwa kuwa na masuria kutokana na maumbile yao na kama sayansi inadhibitisha hili wanawake tueleweshwe kuwa wanaume wetu ndivyo walivyoumbwa.Pawepo na utaratibu mzuri wa wao kuwa na masiria ambao hautaumiza moyo wa mwanamke wa kwanza.Kwa sasa roho zinatuchoma sababu tunaamini mume akitoka nje maana yake hanipendi tena.Maana yake hathamini yote ninayomfanyia.

Pamoja na kuwa huyu baba akichit atapata tabu sana ila nitamsamehe kwa sababu yeye ni nani aishinde tamaa ya kuonja asali ya nje iwapo mfamlme Daudi kipenzi cha Mungu alishindwa,Samson na miguvu yake alishindwa,Suleiman na hekima zake alishundwa akakusanya pisi kama zote,mtume Nuhamad nae pia alishindwa akajiolea pisi zaidi ya moja na manabii wengine weengi wa kwenye biblia nao walishindwa na tamaa za mwili.

Nitamsamehe kwa sababu kama Hilary Cliton na Beyonce walisalitiwa ila wakaelewa na leo wanazeeka na waume zao mimi ndo niwe mjinga nimuache wangu.HAPANA.Nitazeeka nae kama Hillary alivyozeeka na Bill wake.
 
Kwani anapokuwa anacheat hajui kwamba mkewe hafurahishwi na pia Mungu yupo juu anatazama? Hili nalo hadi mtu akumbushwe na mke wake?😂😂😂😂😂.Umenivunja mbavu zangu kwa kweli.
 
Bora umesema wewe mkuu,kwanini kama mwenzio ana kosa wewe ukimbilie kuchepuka? Kwani kutafuta suluhisho mbadala umeshindwa??
Mimi kwangu hakuna sababu yoyote inayohalalisha uzinzi,haipo.
 
Mkuu, kama nimefikia hatua ya kumsababishia mume wangu achepuke,maana yake sifai kuwa mkewe. Mahusiano yetu yafike mwisho ili akakae kwa uhuru na huyo mwanamke mwingine ambaye hatampa sababu ya kuchepuka.
Mambo ya mguu nje mguu ndani hapana na hakuna ndoa inayohusisha strangers.
 
Hizo kauli wanazitumia kuwamanipulate wake zao na kujiona inferior na wakosaji ili waendeee kuvumilia ujinga wao. Jiulize ni kwanini kosa hilo hilo akimsababishia mkewe kulifanya, anakuwa mbogo?
 
Kwanza niwashukuru kaka zangu kwa ushauri mzuri mlonipa kwenye uzi wangu kuikataa misri ya u singo maza.

Pili naomba niwape mrejesho au matokeo mazuri ya ushauri wenu.Yote mlonishauri ambayo ni HESHIMA,KUTUNZA AMANI,UPOLE na UNYENYEKEVU tayari vilikua vinatamalaki nyumbani kwetu kasoro kimoja.KUTOA MBUSUSU BILA KUSUASUA.

Niwe mkweli sipendi mizagamuo😭.
Sio kama sinogewi ila huwa natamanigi zile siku za ovulation au siku nyingine mara chache so mizagamuo ya mara kwa mara ni kero kwangu jambo ambalo lilifanya mume wangu awe analalamika sana.

Hata hivyo,baada ya kuona kaka zangu wote mkihimiza kugawa kila inqpohitajika nikaiona hatari nikaamua kubadilika na sasa natoa as much as posipo na sisubiri anianze.Naona kaanza ku glow kwa furaha na mood nzuri kila siku.Naona kazidi na kunipenta.Vijizawadi kama vyote..
ASANTENI SANA.🙏🙏

Sasa tuachane na hayo.
Mimi leo naomba kuwauliza na mnijibu bila upendeleo.

Kaka zangu,mlinihimiza sana kuwa hampendi MAKELELE.
Mnapenda mkirudi nyumbani nyumba iwe na AMANI na UTULIVU.

Sasa naomba mniambie.
Ikitokea nimejua kwa hakika kuwa mume wangu ananisaliti na hasira,uchungu na huzuni vitanitamalakia.

Je,nyie katika serikali yenu isiyotaka makelele na gubu huku ikihitaji amani na utulivu ili penzi lidumu mna muongozo gani wa reaction sahihi ya vipi mwanamke anapaswa kuwakablii pale anapowakamata katika maufuska yenu?

Nimeandika haya baada ya kushuhudia mbeijing mwenzangu akiwa kamkamata mumewe na mchepuko ikawa analalamika sana.Malalamiko yalivyozidi baba yule akahamia mazima kwa mchepuko huku akijitetea kuwa kakimbia makelele ya wife wake nyumbani.

Hivi kweli umenisaliti halafu utegemee niendelee kuwa kwenye peacefully love mood?

NB;Sijasalitiwa.(bado)
Wewe unawekeza kwenye hisa kweli?
 
Ukitaka ujue wanahalalisha mambo ya ajabu, waulize" mume akikosea mke anaruhusiwa kuchepuka?". Sikilizia majibu utakayopewa.
Naungana na wewe lovie.
Yaani nimekosea uniadhibu kwa ku chit?
 
Sawa mkuu.
Mimi nimemchimba biti kuwa siku akichepuka nikajua ajue sitataka mjadala wowote na ameamini kuwa nilimaanisha ila moyoni mwangu kuna siri kuwa akichepuka simuachi. na kamwe hatakaa aijue hii siri.
Hata hivyo nashukuru so far huyu baba hajanipq viashiria vya uchepuki na ikitokea kachepuka nitamsamehe baada ya kumtesa sana kisaikolojia.
Nzuri hiyo madam,ukiwa na lengo la kuilinda ndoa yako ina maana unaiheshimu ndoa yako kama Mungu alivyoagiza kuwa ndoa na iheshimiwe so kama umejua hilo Mungu atakuepusha na vikwazo vitakavyo haribu ndoa yako,yoye ya yote mfanye ampende Mungu mwenza wako ili awe na hofu ya Mungu,ukishakua na hofu ya Mungu unajikuta huwezi kuwaza kuchepuka maana utathamini uhusiano wako na Mungu automatic utajikuta kila kitu kinaenda kwa kusudi la Mungu
 
System imetumanipulate sana, ndio maana hata mtoa mada anajiona yeye ndio anaweza kusababisha mwenzake achepuke. Hivyo anapaswa kuhangaika na kuhakikisha mwenzake hachepuki. Anasahau kuwa hawa huwa hawatafuti sababu, likitokea si atajiua huyu🤣
Hebu nipe para au sentensi inayosupport haya madai yako mkuu.
Huyo unayemuongelea kwenye hii comment sio mimi mkuu.
Nina uhakika hujaelewa ninaposimamia..
 
Back
Top Bottom