Kaka zangu nimekuja tena kwenu kuomba ushauri wenu kwa habari ya kusalitiwa/Cheating

Kaka zangu nimekuja tena kwenu kuomba ushauri wenu kwa habari ya kusalitiwa/Cheating

Nzuri hiyo madam,ukiwa na lengo la kuilinda ndoa yako ina maana unaiheshimu ndoa yako kama Mungu alivyoagiza kuwa ndoa na iheshimiwe so kama umejua hilo Mungu atakuepusha na vikwazo vitakavyo haribu ndoa yako,yoye ya yote mfanye ampende Mungu mwenza wako ili awe na hofu ya Mungu,ukishakua na hofu ya Mungu unajikuta huwezi kuwaza kuchepuka maana utathamini uhusiano wako na Mungu automatic utajikuta kila kitu kinaenda kwa kusudi la Mungu
Mume wangu ni msabato imara
 
Hakuna mwanaume ana mwanamke Mmoja Hilo ni swala la kuelewa

Kwahiyo wewe hakuna MTU amekuchiti

Kama mnashindwa kuelewa hiyo simple mathematics basi wewe utakuwa haupo sawa.
 
Hakuna mwanaume ana mwanamke Mmoja Hilo ni swala la kuelewa

Kwahiyo wewe hakuna MTU amekuchiti

Kama mnashindwa kuelewa hiyo simple mathematics basi wewe utakuwa haupo sawa.
Hiyo umesema wewe mkuu.
Mbona mimi ndie mwanamke pekee kwa mume wangu@@
 
Mkuu, kama nimefikia hatua ya kumsababishia mume wangu achepuke,maana yake sifai kuwa mkewe. Mahusiano yetu yafike mwisho ili akakae kwa uhuru na huyo mwanamke mwingine ambaye hatampa sababu ya kuchepuka.
Mambo ya mguu nje mguu ndani hapana na hakuna ndoa inayohusisha strangers.
Wanao sema hivi waga wanajuta Vibaya.
 

Nyie mnajiitaga strong lady wengi wenu hujifanyisha strong mwisho wa siku mnabaki mnalia
 
Msaliti hua hasamehewi,haijalishi huyo msaliti ni wa jinsia gani,ukisha salitiwa unatakiwa uchukue maamuzi magumu ambayo huko mbeleni yatakupa amani,

Narudia tena Msaliti hua hasamehewi hata siku moja,

Trust is often compared to a fragile bond,
once shattered, the foundation of safety is gone and hard to rebuild.
Asante Sana Nime bold kuleta msisitizo
 
Sometimes hawa viumbe wanachit pasi ya sababu yeyote zaidi ya tamaa za mwili tu.

Na tena amini nakwambia love wangu ,hata uwe mke mwema vp,hata nyumba iwe na amani na utulivu kuliko ngomeni mwa Bwana na hata uwe mrembo kuliko Cleopatra, Beyonce na Nerfetitti siku tamaa zikimuwaka atakuchit tu. Na cha ajabu anaweza akakuchit na pisi mbovu inazidiwa mvuto na hata na mzee wetu Staphano wazirya.Ukabaki unajiuliza huyu kalogwa au.?Au akakuchit na pisi kali anayojua wazi hawezi kuifanya mke.

Hata hivyo kuchepuka iwe mwanaume au mwanamke haifai na kamwe haipaswi kuhalalishwa.Ni kitu kibaya sana.

Mume wangu kila mara ananiambia mke wangu tutulie,kila wakikutongoza kumbuka kuwa hapa tu hatuna maradhi lakini mapambano ni magumu je tukianza kugawana kipato chetu kidogo na watu wa Pharmacy itakuaje??
Kabisa mkuu,wanachit bila sababu ya msingi.
 
acha kuweka upendo na tamaa kama kapu moja
Unaweza kumpenda mtu na bado ukamchiti
Umpende mtu halafu umchit😂😂😂😂😂. Yaani mfano mimi hapa nianze kumchit mume wangu halafu hapo hapo niwe nampenda? 🤣🤣🤣. Yaani niwe nampenda mtu wakati huo huo nafanya jambo ambalo najua litamuumiza moyo wake? . Huo upendo utakuwa unatoka sayari ya Jupiter.
 
Niende moja kwa moja kwenye Ushauri;
Ukiwa na hakika mume wako anacheat; mpikie chakula kizuri anachokipenda hasa wikiendi. Akisha kula akashiba kabisa;
Mueleze hizo taarifa kwa upole na jinsi zinavyo kuumiza.
Lakini pia mueleze kuwa hayo mahusiano yake mapya yatakavyo weza kuharibu malezi ya watoto. Mwambie kuwa hukutamani kabisa hayo yawe mjadala kwenye mahusiano yenu, ILA umeumia sana na kushindwa kuvumilia kwa muda ukaona useme. Kama una uhakika, wala usimuambie ajitetee...labda aaumue mwenyewe...

Baada ya hapo, timiza majukumu yako kawaida ila usiongelee tena hata wiki nzima.
Amini usiamini...dawa ya moto ni maji... Anaweza kubadilika na kuwa mzuri kama siku mliyofunga ndoa.
Msaliti anaongeleshwa kwa upole😂😂😂😂🤣🤣🤣. Msaliti anakumbushwa kwamba mahusiano yake mapya yanaharibu malezi ya watoto wakati anavyoenda kufanya usaliti wake anajua kabisa madhara ya anachokifanya😂😂😂😂. Hii mioyo mliyonayo jamani bakini nayo tu nyie,msituambukizeee.
 
Wanao sema hivi waga wanajuta Vibaya.
Yaani nijutie kuachwa na mtu ambaye kashapata mpenzi mwingine huko nje?😂😂😂😂. Loool. Moyo huo sina,mi mapenzi silazimishi,kama mtu kapata mwingine ambaye ni bora zaidi yangu akakae nae kwa amani sio mimi kuwa kwenye mahusiano yenye third party.
 
Asante kwa somo.
Akiongea mwanaume kuhusu uanamme nasikiluza kwa makini.

Ujue mkuu hakuna binadamu me au ke anapenda kusalitiwa.Inauma sana ila mimi naamini kuna aina mbili za usaliti upande wa wanaume.

1)Mwanaume anasaliti sbb ana tabia mbaya tu za kimalaya.
2)Usaliti wa kuzidiwa kwa sababu za kimaumbile.

Pamoja na kwamba usaliti ni usaliti tu hata uwe wa aina gani ni mbaya ila mimi naona kuna kitu hakipo sawa(kwa sisi wanawake) kuhusu maumbile ya mwanaume.Sijui sayansi inasemaje kuhusu hili ila naamini wakristo na waislamu walipaswa kuruhusiwa kuwa na masuria kutokana na maumbile yao na kama sayansi inadhibitisha hili wanawake tueleweshwe kuwa wanaume wetu ndivyo walivyoumbwa.Pawepo na utaratibu mzuri wa wao kuwa na masiria ambao hautaumiza moyo wa mwanamke wa kwanza.Kwa sasa roho zinatuchoma sababu tunaamini mume akitoka nje maana yake hanipendi tena.Maana yake hathamini yote ninayomfanyia.

Pamoja na kuwa huyu baba akichit atapata tabu sana ila nitamsamehe kwa sababu yeye ni nani aishinde tamaa ya kuonja asali ya nje iwapo mfamlme Daudi kipenzi cha Mungu alishindwa,Samson na miguvu yake alishindwa,Suleiman na hekima zake alishundwa akakusanya pisi kama zote,mtume Nuhamad nae pia alishindwa akajiolea pisi zaidi ya moja na manabii wengine weengi wa kwenye biblia nao walishindwa na tamaa za mwili.

Nitamsamehe kwa sababu kama Hilary Cliton na Beyonce walisalitiwa ila wakaelewa na leo wanazeeka na waume zao mimi ndo niwe mjinga nimuache wangu.HAPANA.Nitazeeka nae kama Hillary alivyozeeka na Bill wake.
Mkuu,hakuna sayansi yoyote inayohalalisha kucheat haijalishi ni kwa me au ke. Hiyo sayansi labda uje nayo wewe. Ni kwamba tu jamii zetu zina mfumo dume kwahiyo inatafutwa sababu ya kuhalalisha mwanaume kuwa na wanawake wengi ndo utasikia kauli za mwanaume kaumbiwa tamaa sijui what what as if wanawake huwa hawatamani.
 
Nyie mnajiitaga strong lady wengi wenu hujifanyisha strong mwisho wa siku mnabaki mnalia
Na wanajiofanyaga wafia ndoa nao hulia machozi ya damu baada ya kupewa UKIMWI na PID kama malipo ya kuwavumilia wanaume wazinifu.
 
Kwanza niwashukuru kaka zangu kwa ushauri mzuri mlonipa kwenye uzi wangu kuikataa misri ya u singo maza.

Pili naomba niwape mrejesho au matokeo mazuri ya ushauri wenu.Yote mlonishauri ambayo ni HESHIMA,KUTUNZA AMANI,UPOLE na UNYENYEKEVU tayari vilikua vinatamalaki nyumbani kwetu kasoro kimoja.KUTOA MBUSUSU BILA KUSUASUA.

Niwe mkweli sipendi mizagamuo😭.
Sio kama sinogewi ila huwa natamanigi zile siku za ovulation au siku nyingine mara chache so mizagamuo ya mara kwa mara ni kero kwangu jambo ambalo lilifanya mume wangu awe analalamika sana.

Hata hivyo,baada ya kuona kaka zangu wote mkihimiza kugawa kila inqpohitajika nikaiona hatari nikaamua kubadilika na sasa natoa as much as posipo na sisubiri anianze.Naona kaanza ku glow kwa furaha na mood nzuri kila siku.Naona kazidi na kunipenta.Vijizawadi kama vyote..
ASANTENI SANA.🙏🙏

Sasa tuachane na hayo.
Mimi leo naomba kuwauliza na mnijibu bila upendeleo.

Kaka zangu,mlinihimiza sana kuwa hampendi MAKELELE.
Mnapenda mkirudi nyumbani nyumba iwe na AMANI na UTULIVU.

Sasa naomba mniambie.
Ikitokea nimejua kwa hakika kuwa mume wangu ananisaliti na hasira,uchungu na huzuni vitanitamalakia.

Je,nyie katika serikali yenu isiyotaka makelele na gubu huku ikihitaji amani na utulivu ili penzi lidumu mna muongozo gani wa reaction sahihi ya vipi mwanamke anapaswa kuwakablii pale anapowakamata katika maufuska yenu?

Nimeandika haya baada ya kushuhudia mbeijing mwenzangu akiwa kamkamata mumewe na mchepuko ikawa analalamika sana.Malalamiko yalivyozidi baba yule akahamia mazima kwa mchepuko huku akijitetea kuwa kakimbia makelele ya wife wake nyumbani.

Hivi kweli umenisaliti halafu utegemee niendelee kuwa kwenye peacefully love mood?

NB;Sijasalitiwa.(bado)
Huyo aliyekimbilia kwa mchepuko alikuwa anatafuta sababu tu🤣 tatizo letu sisi tunatamani tupate chombo kipya kila siku ukishakizoea kimoja hamasa inapungua ,, vijana acheni zinaa
 
Back
Top Bottom