Kwanza niwashukuru kaka zangu kwa ushauri mzuri mlonipa kwenye uzi wangu kuikataa misri ya u singo maza.
Pili naomba niwape mrejesho au matokeo mazuri ya ushauri wenu.Yote mlonishauri ambayo ni HESHIMA,KUTUNZA AMANI,UPOLE na UNYENYEKEVU tayari vilikua vinatamalaki nyumbani kwetu kasoro kimoja.KUTOA MBUSUSU BILA KUSUASUA.
Niwe mkweli sipendi mizagamuo😭.
Sio kama sinogewi ila huwa natamanigi zile siku za ovulation au siku nyingine mara chache so mizagamuo ya mara kwa mara ni kero kwangu jambo ambalo lilifanya mume wangu awe analalamika sana.
Hata hivyo,baada ya kuona kaka zangu wote mkihimiza kugawa kila inqpohitajika nikaiona hatari nikaamua kubadilika na sasa natoa as much as posipo na sisubiri anianze.Naona kaanza ku glow kwa furaha na mood nzuri kila siku.Naona kazidi na kunipenta.Vijizawadi kama vyote..
ASANTENI SANA.🙏🙏
Sasa tuachane na hayo.
Mimi leo naomba kuwauliza na mnijibu bila upendeleo.
Kaka zangu,mlinihimiza sana kuwa hampendi MAKELELE.
Mnapenda mkirudi nyumbani nyumba iwe na AMANI na UTULIVU.
Sasa naomba mniambie.
Ikitokea nimejua kwa hakika kuwa mume wangu ananisaliti na hasira,uchungu na huzuni vitanitamalakia.
Je,nyie katika serikali yenu isiyotaka makelele na gubu huku ikihitaji amani na utulivu ili penzi lidumu mna muongozo gani wa reaction sahihi ya vipi mwanamke anapaswa kuwakablii pale anapowakamata katika maufuska yenu?
Nimeandika haya baada ya kushuhudia mbeijing mwenzangu akiwa kamkamata mumewe na mchepuko ikawa analalamika sana.Malalamiko yalivyozidi baba yule akahamia mazima kwa mchepuko huku akijitetea kuwa kakimbia makelele ya wife wake nyumbani.
Hivi kweli umenisaliti halafu utegemee niendelee kuwa kwenye peacefully love mood?
NB;Sijasalitiwa.(bado)