Kaka zetu, hayo mabegi ni vipi kwani?

Kaka zetu, hayo mabegi ni vipi kwani?

Nilisikia tetesi zinatengenezwa hapa hapa bongo na wachina kariakoo. Sijui ni kweli au laah
Msema kweli mpenzi wa Mungu,Hilo sijui kwa kweli!Ila inawezekana kwa asimilia nyingi Sana coz Kuna viwanda vingi vya kichina vinafanya kazi hapa,viatu vingi vya kike vinatengenezwa hapa so hawawezi kushindwa kutengeneza begi
 
Begi la Biowang linaficha mengi mkuu ikiwemo kuwa apeche alolo[emoji38][emoji38][emoji38]
Mmmh Sasa unafichaga mkate wa lunch mle au linafichaje umaskini?au ndio Kama mdau mmoja kasema kikontena Cha ubwabwa?
 
Ahh kuna cha kubisha hapo, hizo pochi si ni dressing table assistant 😄😄. Kinachonifurahisha zaidi utakuta umepewa documents Ila bado utaibeba bahasha na pochi mikono tofauti
😂😂😂😂Hili dongo la bahasha na pochi mikono tofauti limepenyaaa...utasema umeniona..huwa tunaogopa kuchafua bahasha na lipsticks ikifunguka bahati mbaya na pochi zetu siku hizi ndogondogo
 
Mmmh Sasa unafichaga mkate wa lunch mle au linafichaje umaskini?au ndio Kama mdau mmoja kasema kikontena Cha ubwabwa?

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]si unajua njaa ya mjini posta ukiongezea hamna vibanda vya mama ntilie ni tabu tupu
 
Huwa mnaoneka yamewalemea,mnachoka Sana...haki badilisha tu utaona nafuu
Kuna laptop na adaptor yake, kuna Biblia kubwa, kuna kitabu kimoja cha maarifa cha kila mwezi, kuna note book.

Kweli tuweke hivi vyote kwenye mkoba Johannah?

Yaani hata nikishuka kwenye gari naingia ofisini najiskia nimebeba kitu.
 
Cattigo Biblia kubwa unaenda nayo kazini ya nini?kwa nini usiamke nyumbani ukatafakari katika kabla hujaondoka?wewe muda wa kusoma kitabu cha maarifa na Bible na kazi za kwenye laptop Unaupata wapi?wewe utakuwa unapenda tu mizigo
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]si unajua njaa ya mjini posta ukiongezea hamna vibanda vya mama ntilie ni tabu tupu
Ila hapa umeongea kitu very sensitive sana,nikiweka maskhara pembeni serikali imeamua kutesa watu wenye kipato kidogo huko posta. sio Kilauea mtu ana afford kula kule migahawani kwenye mabei.... dah hapo nitaakuvumilia tu na Biowang lako
 
Ukitaka kujua mabegi angalia mabasi ya Goba na Tegeta na wanaopanda na mabegi wananukia mafuta ya Rays. Wengi wao ni mafundi ujenzi utakutana nao mara nyingi wakitoka site. Ukweli mabegi ni kero sana kwenye usafiri wa umma.
 
Rays jamaniii!mbona haipo siku hizi😂.... sasa na wa ofisini wameshayarukia kaka ni hatari na nusu
 
Rays jamaniii!mbona haipo siku hizi[emoji23].... sasa na wa ofisini wameshayarukia kaka ni hatari na nusu
Najua hakuna YOLANDA ila Rays yapo. Ushamba tu unatembea mgongo umebeba mzigo. Kuigaiga tu.
 
Cattigo Biblia kubwa unaenda nayo kazini ya nini?kwa nini usiamke nyumbani ukatafakari katika kabla hujaondoka?wewe muda wa kusoma kitabu cha maarifa na Bible na kazi za kwenye laptop Unaupata wapi?wewe utakuwa unapenda tu mizigo
Nina manage kuvitumia vyote kila siku na kila kimoja kikaingia sehemu yake katika ubongo na moyo!

Na majukumu yangu ya kazi yanafikiwa kabla ya muda wa kazi kuisha[emoji3]

Labda Nina uwezo WA tofauti kidogo.
 
Ila hapa umeongea kitu very sensitive sana,nikiweka maskhara pembeni serikali imeamua kutesa watu wenye kipato kidogo huko posta. sio Kilauea mtu ana afford kula kule migahawani kwenye mabei.... dah hapo nitaakuvumilia tu na Biowang lako

Yah ndio maisha yalivyo mkuu
At least kipindi kile chakula hadi cha 2000 unapata ila sasa hivi hali ni tete
Acha tu wabebe mabegi kiroho safi
 
Najua hakuna YOLANDA ila Rays yapo. Ushamba tu unatembea mgongo umebeba mzigo. Kuigaiga tu.
Yolanda kwenye kimkebe!long time.wamegoma wadogo zako humu wamesema niwaache na mabegi Yao.
 
Nina manage kuvitumia vyote kila siku na kila kimoja kikaingia sehemu yake katika ubongo na moyo!

Na majukumu yangu ya kazi yanafikiwa kabla ya muda wa kazi kuisha[emoji3]

Labda Nina uwezo WA tofauti kidogo.
Eeeeeeh!wewe ndio wale watu wamekaa kimyaaa ofisini?basically una? uwezo mkubwa
 
Yah ndio maisha yalivyo mkuu
At least kipindi kile chakula hadi cha 2000 unapata ila sasa hivi hali ni tete
Acha tu wabebe mabegi kiroho safi
Kama kweli wanawekaga ubwabwa mle kwenye mabegi,basi kiroho safi tu. Alluta continua!
 
Back
Top Bottom