Kaliba ya Ualimu lazima iheshimiwe

Sjui umetumia kigezo gani, ila hakuwa sahihi. Ipo namna, ila sio ile.
Kwa upande mmoja mpwayungu binafsi nimefahamu kwenye ajira za Ualimu mwaka Jana walipotangaza alikua anakesha mpka saa 8 kuvizia mtandao. Tokea ameanza mada za kuponda ualimu/walimu nilikua najua ni Mwalimu. Lakini mpwayungu ni Mwalimu ambae ana exposure ya maisha anajua scale ya mishahara ya kada nyingine na kada hii ya ualimu na ugumu wa kazi anauona, Lakini moyo kubalance kuukubali ndio hana, mada Nyingi ameongea kwa kuamsha hisia/hasira ya upambanaji. Mimi nilipo nadhani siwezi kupata ofa za kwenda kusimamia/kusahisha mitihani kwa sababu ya kupishana na viongozi kwenye haki yangu wanabaki kuweka vinyongo tu, ndio kada tuliyonayo.
 
Mshana utakuwa ni miongoni mwa wale walokomba mamilioni benk ya walimu🤣🤣 (natania)
Kuna muda people must learn in a hard way, haya mambo ya kurembana rembana na kukosoana Kwa staha ndo yametufikisha hapa tulipo, Hadi Leo ripoti ya CAG ni kichefu chefu, watu wanajipigia tu.

Sasa ina maana gani kumsifia mwalimu na kumremba huku maslahi yake ni duni na hamna mpango wa kumboreshea....hayo mambo ya ualimu ni wito yalikuwa enzi ya ujamaa, sasa ni ubepari, capital ndo kila kitu....Mwalimu alipwe vizuri kuendana na hali ya maisha....sifa hazipeleki chakula mezani.

Katika ulimwengu wa kibepari pesa ndiyo kila kitu, lipa walimu vizuri heshima irudi, nidhamu ya wanafunzi irudi, watoto wafaulu taifa lisonge mbele.....Nani atamuheshimu mwalimu anayevaa suruali ya njano, mkanda uliopauka na Shati la kitenge mpauko?
 
Umeongea ukweli mtupu, just imagine mpaka mwanafunzi anajua Mwalimu wake hana hela, utamsikia Mwanafunzi anasema Mwalimu hivi unaweza kununua pikipiki kweli? Unajua kwanini? Kwa sababu anaona Mwalimu anaingia shuleni na baiskeli kweli?
 
Ndio maana nikasema sio kosa la walimu bali wanasiasa waliojikasimisha madaraka na heshima zote.. Kisha wakaingiza kanuni ya divide n rule kwenye kada ya ualimu
 
Umeongea ukweli mtupu, just imagine mpaka mwanafunzi anajua Mwalimu wake hana hela, utamsikia Mwanafunzi anasema Mwalimu hivi unaweza kununua pikipiki kweli? Unajua kwanini? Kwa sababu anaona Mwalimu anaingia shuleni na baiskeli kweli?
Kwakuwa kwa mwanafunzi kumiliki pikipiki kwake ni mafanikio makubwa sana .. Je hapo mwalimu ana kosa gani?
 
Ndio maana nikasema sio kosa la walimu bali wanasiasa waliojikasimisha madaraka na heshima zote.. Kisha wakaingiza kanuni ya divide n rule kwenye kada ya ualimu
Acheni Mpwayungu aseme ukweli halisi, hao wanasiasa na viongozi wamefumbia macho madhila ya walimu, hebu Fikiria kila siku wanakuja na mpango ya ujenzi wa madarasa lakini ujenzi wa nyumba za walimu ni mwendo wa jongoo.....hawana haja hata ya kujua hao walimu wanaishi wapi, ukizingatia hawana house allowance.
Uzuri mama kasema anapitiaga humu, Kina Tulia wanapita humu.....hebu waone hali halisi.
 
Huyo mtu si kwamba anasema ukweli bali anatusi na kudhalilisha walimu.. Hivi kusema kazi ya ualimu ni laana ni kusema kweli ama ni kudhalilisha kada ya watu inayotegemewa na mamilioni? Yeye kama sio walimu hao hao anaowatusi leo angekuwa hapo alipofikia?
Tusisahau tulikotoka na tusiwadharau waliotutoa huko tulikotoka
 
Habari mwl mshana. Sijui niseme nini ila, wapo wanaowaza wajenge madarasa wapeleke watoto humo ila hawawazi wapeleke ofisi mwl akajipange humo.
Kifupi ni kuwa mwalimu ni wa muhimu sana ila UALIMU umeepuuzwa mno ndo maana kila siku siku hizi hayaishi MAELEKEZO kwa hao walimu. Mwalimu asimamie majengo (sijui ndo haiba yenyewe?), Mwl apangiwe cha kufundisha( rejea ratiba mpya toka TAMISEMI) mwaka jana. Mwalimu aelekezwe namna ya kumtathimini mwanafunzi wake (rejea mtihani wa ku assess kidato cha kwanza mwaka huu), mwalimu anafungiwa mkataba mpya kazini afaulishe kila mwanafunzi ( sijui ndo somo la falsafa au maadili?) nk. Hata baada ya pasaka hii huenda kuna MAELEKEZO mapya tena.
HATA TUSEMEJE, UALIMU SIKU HIZI UPO HUKO TAMISEMI NA HUKU CHINI WALIMU NI KAMA VIRANJA TU.
 
Tunarudi kulekule kwa wanasiasa.. Mtu asiye mweledi wa taaluma anapewa jukumu la kusimamia taaluma.. Mtu aiyejua lolote kuhusu mitaala, kanuni, sheria na taratibu za elimu ndio anapeaa jukumu la kuleta maono mapya...
Siku tutakapoiondolea siasa thamani na hadhi tuliyoipa mambo mengi yatabadilika
 
Hatukatai maelekezo, Ila maelekezo yaendane na maslahi.
Sasa hivi wanataka walimu mahiri wafundishe English madarasa ya chini, hii inakuja kufatia kufeli Kwa watoto katika Hilo somo, Ila tujiulize hawa walimu mmewapa semina? Kuna motisha kwao? Utasikia serikali haina pesa, Ila pesa za kudouble pay ndege zipo.....halafu yakitoka kugawana cha juu huko yanasimama majukwaani walimu waheshimiwe, Nye, Nye Nye!
Jamani heshima pesa, Walimu nao wanastahili kulipwa vizuri.
 
halafu yakitoka kugawana cha juu huko yanasimama majukwaani walimu waheshimiwe, Nye, Nye Nye! [emoji23]
 
Ni sahii umeongea kweli 100%, hiyo pressure inayotoka juu ndio inawafanya wakuu wa shule wachanganyikiwe na kutoa maagizo Kila wakati kwa kigezo Cha kutokupanda daraja maana wanamjua ndio roho ya Kila Mwalimu, Mfano juzi kulikua Kuna semina ya walimu wa science jina langu alikuepo (mkuu hakutuma) unajua kwanini? Kwa sababu aliagiza walimu kubaki mpaka saa 11:00 jioni hakuna posho Wala chakula unajitegemea, nikamwambia siwezi kufanya hiyo natimiza majukumu yote yanayohitajika, mda wa serikali ni saa 9 naondoka, Nilimwambia wewe unalipwa hiyo posho ya madaraka kwa kazi wanazozifanya walimu, yeye hafundishi ni vikao na kukaa ofisini, kinyongo kikaanza hapo, acha tu Mpwayungu aseme, serikali inabidi ifanye mambo yafuatayo kupanda daraja iwe ni haki ya Kila mtumishi akifikisha muda sahii wa kupanda daraja apande tena barua itoke moja kwa moja utumishi, walipwe stahiki zao kwa wakati, sio likizo Leo wanalipwa baada ya miaka miwili, Masters itambulike kwenye madaraja. N.k
 
Kwa kusema hivi ndo wengine wanasema UALIMU umegeuka kuwa laana (japo mimi sikubaliani na dhana hii) ila sio mwalimu kama mwalimu. Na kwa mtizamo wako mwanasiasa ameharibu UALIMU wa mwalimu! Maana amefikiri kujenga majengo mapya nchi nzima na kuyaita shule/madarasa, lakini hakuna anayewaza shule mpya ngapi zinahitaji walimu wapya wangapi? Madarasa mapya mangapi yanahitaji walimu wapya wangapi? Lakini inaonekana mwalimu yule yule aliyelemewa na mzigo wa wanafunzi ataongezewa mzigo tena (na kwa kuwa ni ualimu ni WITO) basi hawezi kutusumbua atakubali tu. (Kumbuka mimi ni mwalimu na moja kati ya maudhi nifundishayo kwa wanafunzi wangu ktk somo langu ni kupinga uonevu 'protesting'), hapa wakija hawa kina village sijui wakisema mwalimu mwenye kukubali kufanyiwa haya basi ana laana tunawashindaje ktk hali hii?
 
Kutumika na wanasiasa ni moja ya vitu vili/navyowashusha hadhi.

Lakini pia umoja tepetepe pia, walimu ni wengi nchini, matatizo yao yanafanana almost nchi nzima. Ni ajabu kutokua na umoja thabiti kutetea maslahi yao.
Wazo zuri watalitazama
 
halafu yakitoka kugawana cha juu huko yanasimama majukwaani walimu waheshimiwe, Nye, Nye Nye! [emoji23]
In negative cheque, huwa naona mtizamo wa hao wanasiasa juu ya shule na mwalimu ni ' shule ni vituo vya kukusanya na kukuza watoto pamoja badala ya kuzagaa tu mitaani chini ya walezi wajulikanao kama walimu' . Ila zipo zilizokusudiwa kuwa shule na kutoa elimu na hizo ndizo hupokea watoto wa hawa wapiga cha juu.
 
Walimu wenyewe wanatakiwa wabadilike, la sivyo wataendelea kudharaulika. Haiwezekani ishu za kuandikisha ugawaji wa mahindi Mwalimu anaomba, kuandikisha kupiga kura wanagombania. Mambo mengine acheni jobless huko kujenga heshima yenu.
Haina sababu ya wao kulazimishwa na mtu kubadilika. Kila mtu na style yake ktk maisha, kuwalizimisha kubadilika ni kuingilia maisha yao binafsi ambavyo hayakuhusu. vipi na wewe wakijua kazi yako wakaidharau wakakwambia ubadilike utafrahi.

Kuwaambia kubadilika ni kuwatusi. Mbona kada zingine km askari hawasemwi km Walimu kwa hiyo huko ndiyo hakuitajiki mabadiliko. Sema tulishawachukulia hawa ndugu zetu Walimu km watu wapole wasio na makuu. Wangekuwa wanashika bunduki haya matusi na dhihaka usingeziskia.

Maisha ni ya mtu mwingine na familia yake iweje iwe kero kwa mwingine wakati havunji sheria za nchi Wala kumsema mtu. Nahisi huu ni wivu tu. Tuache kuwashambulia wanatusaidia kutufundishia watoto wetu.

Unaweza kuwaza, hivi hao wanaowashambulia Walimu ni watu wazima kweli. Je wana watoto kweli. Je watoto wao wanafundishwa au watafundishwa na askari au Walimu. Km ni Walimu inakuwaje unawadharau. Hivi pili pili usiyo ila inakuwasha nini.
 
Hii kada ili iheshimike kwanza bajeti yake inapaswa iwe kubwa na kuwe na malipo ya ziada kwa walimu. Posho ni muhimu sana ili kuwapunguzia walimu stress hii kada ni ngumu mtu kuiba au kufanya ufisadi.

Waalimu wanamambo mengi sana yanayowasumbua ila hawana pakuyasemea. Embu fikiria Mwl. anaomba likizo mwaka huu na malipo yake yanakuja mwakani tena kwa kuyafuatilia fuatilia kila siku. Wanadai malimbikizo ya muda hawapewi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…