Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani "lofa" ni tusi? Mbona Marehemu Mkapa alituita watanzania wote malofa, ulofa ni sifa ya mtu asiyejielewa, ni kivumishi tu Kama ilivyo mjinga....sa mtu awe lofa umuite mjanja?Nasikitika kama kuita Walimu Malofa' nao ni Ukweli.
Mkuu hawa wanasema ukweli kwamba ualimu ulikua ni wito zamani sio sasa hivi kwa sababu maisha yamebadilika.Haina sababu ya wao kulazimishwa na mtu kubadilika. Kila mtu na style yake ktk maisha, kuwalizimisha kubadilika ni kuingilia maisha yao binafsi ambavyo hayakuhusu. vipi na wewe wakijua kazi yako wakaidharau wakakwambia ubadilike utafrahi.
Kuwaambia kubadilika ni kuwatusi. Mbona kada zingine km askari hawasemwi km Walimu kwa hiyo huko ndiyo hakuitajiki mabadiliko. Sema tulishawachukulia hawa ndugu zetu Walimu km watu wapole wasio na makuu. Wangekuwa wanashika bunduki haya matusi na dhihaka usingeziskia.
Maisha ni ya mtu mwingine na familia yake iweje iwe kero kwa mwingine wakati havunji sheria za nchi Wala kumsema mtu. Nahisi huu ni wivu tu. Tuache kuwashambulia wanatusaidia kutufundishia watoto wetu.
Unaweza kuwaza, hivi hao wanaowashambulia Walimu ni watu wazima kweli. Je wana watoto kweli. Je watoto wao wanafundishwa au watafundishwa na askari au Walimu. Km ni Walimu inakuwaje unawadharau. Hivi pili pili usiyo ila inakuwasha nini.
Sasa Kazi ngumu ambayo malipo yake hayatoshelezi basic needs za huyo Mtumishi Kwa mwezi iitweje?Kusema ualimu ni kazi ya laana ndio ukweli?
Wamekosea sana, tena sanaaaa. Wajifunze kule Quora dijest, ni huru kweliUkiruhusu uhuru wa kutoa maoni, kubali kusikia ukweli usioupenda....JF wamekosea..warudishe hizo nyuzi
Ni Laana kweli, wanifungie na mimi. Tatizo ni ukweli unaumaKusema ualimu ni kazi ya laana ndio ukweli?
KabisaKwani "lofa" ni tusi? Mbona Marehemu Mkapa alituita watanzania wote malofa, ulofa ni sifa ya mtu asiyejielewa, ni kivumishi tu Kama ilivyo mjinga....sa mtu awe lofa umuite mjanja?
Eti wanachuja ukweli....ukiamua kusikia ukweli uwe na roho ngumu....Wamekosea sana, tena sanaaaa. Wajifunze kule Quora dijest, ni huru kweli
Dah! Hapo mwishoni nimefarijika sana uliposema Mungu ibariki Tanganyika. Am proud to be Mtanganyika, from Tanga.Maslahi yangu: Mimi ni mwalimu kwa kusomea.
Nimefarijika na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa JamiiForums kwa kuondoa/kufuta mada zote zinazowadhalilisha walimu na kada nzima ya ualimu na kuwapa adhabu stahiki wale wote waliokuwa vinara kwenye hilo.
Kuna mahali tuliyumba na tukakosea sana, tukakosea pakubwa napo ni pale tulipoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma. Kwamba mwanasiasa hohehahe wa elimu ana thamani kubwa na heshima stahiki kuliko mtu mwenye ujuzi wa elimu ya kusomea kama mwalimu, ama kama daktari. Haya yanayotokea sasa ni madhara ya matokeo ya kuwatukuza na kuwakweza wanasiasa.
Mwalimu ndio msingi wa maarifa yote ya ulimwengu na hapa nazungumzia walimu katika hatua ile ya awali/msingi ya kufundishwa kuumba herufi, kusoma, kuandika nk. Huko mbeleni hakuna changamoto kama hii hatua hii ya awali. Hivyo kumheshimu mwalimu sio jambo la hiari bali ni jambo la lazima.
Rais wa kwanza mweusi wa Tanganyika ni hayati Julius Kambarage Nyerere, lakini jina hilo halina ladha kabisa bila kutanguliza neno MWALIMU. Huyu alikuwa ni mwalimu kwa ujuzi na Marais wengine waliofuatia karibia wote walitokea kwenye ualimu. Ualimu ndio msingi wa maarifa yote.
Baada ya vita ya Kagera 1977-1979 nchi iliyumba kwenye nyanja nyingi na kaliba ya ualimu haikuachwa nyuma. Kufikia mwanzoni mwa miaka ya 80, Mwalimu katika kuhangaika huku na kule kutafuta usaidizi wa kielimu kiuchumi nk ndio akapata usaidizi wa UNESCO waliokuwa na program ya UPE (Universal Primary Education) Elimu ya Msingi kwa Wote.
Kufanikisha hili ikabidi kuwe na program ya kuwachukua watu wazima na kuwapiga brush ya elimu ya ualimu ili waweze kufidia nakisi ya walimu wa elimu ya awali kutokana na watoto kuandikishwa kwa wingi sana.
Program ya UPE kwa bahati mbaya ikapewa jina la dhihaka na waswahel waliooita Ualimu Pasipo Elimu.. Hili nalo lilikuwa kosa ambalo madhara yake yalikuja kuonekana baadae. Program ya UPE ilikuja kufutwa na Mzee Ruksa kama sio Mkapa.
Kiasili kaliba ya ualimu ni kaliba iliyokuwa inaheshimika sana. Maana mwalimu alichukuliwa kama kiumbe aliyeelimika kuliko wengine, mwenye maarifa mengi, ujuzi hekima, ufahamu mkubwa na jasiri muongoza njia. Mwalimu ndio aliaminiwa kwa kazi kubwa kubwa za kitaifa kama sensa, takwimu, chaguzi mbalimbali nkn.
Wakati huo kuitwa mwalimu ama kuwa mtoto wa mwalimu ilikuwa ni heshima sana kutokana na umuhimu wake kwenye jamii.
Vipaumbele na maono ya taifa ndio vilikuja kuitia doa kubwa kabila ya ualimu hasa pale walipoamua kuipa thamani kubwa siasa na kuisahau taaluma.. Kuteuliwa kwa wanasiasa kuongoza taasisi nyeti kama ELIMU ilikuwa kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la walimu.
Zikaanza sarakasi kipindi cha Mkapa kuelekea Kikwete. Kukaletwa program kama za UPE lakini kipindi hiki wakiwachukua vijana waliofeli kidato cha nne, zile program zikapewa majina ya dhihaka kama voda fasta nk.
Kumpika mtu mpaka aje kuiva kuwa mwalimu si jambo dogo, sasa wale walimu wa miezi sita na mwaka mmoja tena waliofeli kidato cha nne sijui walifundishwa nini kwakuwa hata ukiwauliza haiba ni kitu gani ama misingi na falsafa ninini hawajui.
Kufikia hapa ndio kaliba ya ualimu ikawa imepoteza heshima, mvuto ustaarabu. Vijana barobaro wasioiva kihaiba ndio wakawa walimu, wanasiasa wakaanza kuwatumia kwa manufaa yao. Ualimu ikawa ni kichochoro cha kutumika na wanasiasa.. Wakaleta chama cha walimu na bank ya walimu. Yaliyofuatia yote ni msiba wa kuhuzunisha.
Hawa vijana wa sasa wanaokosoa na kudhihaki hii kaliba ni kizazi kile cha walimu wa mwendokasi na vodafasta. Ualimu ni Wito sio mbadala wa ajira. Hawa walienda kwenye ualimu kama mbadala baada ya kufeli na kukosa kaliba ya ndoto zao.
Hawa hawajapikwa wakaiva maana hata hivyo hawana wito ni makanjanja wa maisha wenye kinyongo kikubwa na kushindwa kwenye mengi. Wana nyongo za kutapika lakini wameshindwa kufanya hivyo kwenye mitandao mingine kwakuwa watatumia utambulisho binafsi na ni rahisi kujulikana.
Hawa walitaka kuitumia JF kama uchochoro wa kutoa hasira zao na kuidhalilisha kada ya ualimu kwa kutumia faida ya utambulisho bandia bila kujali kwamba kwa kufanya hivyo wanaishushia hadhi forum na kuwapa shida wamiliki wanaojulikana kwa majina, sura na hata mawasiliano yao.
Hata mitume wengi kwenye imani zetu walikuwa ni walimu. Ualimu ni kazi ya kiroho na ni kazi ya wito. Iheshimiwe, itambuliwe, ithaminiwe na kupewa hadhi inayostahili. Wanasiasa walione hili na kulifanyia kazi.
Mungu ibariki JamiiForums
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu wabariki Walimu
Wala hatugombani mkuu, sorry kama nimekukwaza. Ila ukweli lazima usemweSio kosa lako
Kaza hapo hapo, huwezi kubaki kazini Hadi saa 11 tena bila kwenda lunch, halafu bila motisha yoyote....muda wa serikali ukiisha sepa....muhimu umetimiza majukumu yako ya siku.Ni sahii umeongea kweli 100%, hiyo pressure inayotoka juu ndio inawafanya wakuu wa shule wachanganyikiwe na kutoa maagizo Kila wakati kwa kigezo Cha kutokupanda daraja maana wanamjua ndio roho ya Kila Mwalimu, Mfano juzi kulikua Kuna semina ya walimu wa science jina langu alikuepo (mkuu hakutuma) unajua kwanini? Kwa sababu aliagiza walimu kubaki mpaka saa 11:00 jioni hakuna posho Wala chakula unajitegemea, nikamwambia siwezi kufanya hiyo natimiza majukumu yote yanayohitajika, mda wa serikali ni saa 9 naondoka, Nilimwambia wewe unalipwa hiyo posho ya madaraka kwa kazi wanazozifanya walimu, yeye hafundishi ni vikao na kukaa ofisini, kinyongo kikaanza hapo, acha tu Mpwayungu aseme, serikali inabidi ifanye mambo yafuatayo kupanda daraja iwe ni haki ya Kila mtumishi akifikisha muda sahii wa kupanda daraja apande tena barua itoke moja kwa moja utumishi, walipwe stahiki zao kwa wakati, sio likizo Leo wanalipwa baada ya miaka miwili, Masters itambulike kwenye madaraja. N.k
Sawa mkuu. Tuko pamojaTuko pamoja niliposema hivyo nilimaanisha ni kosa la wanasiasa walioamua kuipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma
Unaogopa ban mkuuSiku nilipoona humu watu wanashindanisha bodaboda na waalimu nafsi yangu ilisononeka sana japo maadui zangu wengi ni waalimu
Mkuu unamawazo mazuri sana ila anza ukiwa kazini yakitiki kopa wekeza mifugo yako na mashamba then timua. Kuna watu wanamake hela mashambani na hata hawa habari na ajira ila sema mtu ukiajiriwa unahofia kupoteza ajira.Mshahara mdogo kazi kama zote, kwa kipindi hiki ukinunua mchele kilo ishirini, korie litre 5 unga, maharage mshahara wote umekwisha...unaanza kuzihesabu siku.... Kiukweli Kuna kitu kipo moyoni mwangu Mungu azidi kunipa utulivu na uvumilivu....nimepanga kutokomea mashambani huko nikachimbe visima yawe maisha yangu kwa uhuru.
Hiyo Iko wazi viongozi wa juu wanaweka vikao Kila siku posho kibaoo wanajibebea, kada zingine akiongeza muda ambao hupo kisheria ana demand malipo na analipwa, kuja kwetu sisi mkuu anataka akutumie to the maximum mfukoni hakuna kitu, Mwalimu aliyenifundisha Niko secondary mpaka Leo Nimekua Mwalimu maisha yake mpaka Leo yako vilevile, kwa kifupi walimu ni daraja la watu kwenda sehemu nyingine wakati huko palepale.Kaza hapo hapo, huwezi kubaki kazini Hadi saa 11 tena bila kwenda lunch, halafu bila motisha yoyote....muda wa serikali ukiisha sepa....muhimu umetimiza majukumu yako ya siku.
Kwa mshahara gani hasa wa kujitafutia vidonda vya tumbo? Unajitoa Kwa watoto ambao wao na wazazi wao wanakudharau.....huu ni uzwazwa.