Kaliba ya Ualimu lazima iheshimiwe

Uko sahihi kabisa.. Mwanasiasa mpungukiwa wa taaluma na maarifa mengi yeye ni mtafuta sifa za kisiasa kwa manufaa binafsi. Bado nalia na wote walioamua kuipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma
Leo hii mwanasiasa anachojua ni idadi ya vitu kwakuwa hapa ndio kikomo cha maarifa yake
Atakupa idadi ya madarasa yaliyojengwa
Atakupa idadi ya vyumba vya hospital nknk
Lakini kamwe hawezi kukupa idadi ya vyuo vya ualimu vilivyojengwa ama kuboteshwa
Hawezi kukupa idadi ya walimu walioenda kuongeza maarifa
Huwezi kukupa mipango endelevu ya kuboresha maslahi ya mwalimu na mazingira yake

Nina heshima kubwa kwa mwalimu fukara kuliko mwanasiasa maana hawa wamejaa ufedhuli, ujivuni ni wezi wapiga dili, wanyonyaji na wahujumu uchumi wakubwa
 
Walimu wanawekewa makorokoro mengi sana na kila mkubwa akiwatembelea anataka matokeo mazuri kwa Mwl. ambaye anamadai yake kibao na mshahara duni sasa hapo unategemea Mwl. atafanya kazi kwa moyo?
 
Walimu waache kutumika na Serikali

Walimu wajitambue, wajiheshimu
 
Nakuheshimu sana bro, ila unadhani ni uongo katika yote yaliyoongelewa? Sema mada ziliwasilishwa katika lugha zisizo za staha. Lakini ni ukweli asilimia 100 waalimu wetu wana changamoto nyingi na hata wewe hujataja hata moja, zaidi umezunguuka tu.
 
Nakuheshimu sana bro, ila unadhani ni uongo katika yote yaliyoongelewa? Sema mada ziliwasilishwa katika lugha zisizo za staha. Lakini ni ukweli asilimia 100 waalimu wetu wana changamoto nyingi na hata wewe hujataja hata moja, zaidi umezunguuka tu.
Asante kwa heshima[emoji1545][emoji1752]
 
Halafu mtu akisema ukweli mnafuta uzi wake. Hao jamiiforums wenyewe nao ni walewale tu. Hivi unadhani utakwenda twitter ukatoe mawazo huru? Fanyieni kazi mawazo ya mtu, angalieni je yasemwayo yapo? Siyo kumuwajibisha mtu.
Mpwayungu nilikuwa sipendi uwasilishaji wake lakini ni kweli alikuwa na hoja, tena za msingi kabisa.
 
Nasikitika kama kuita Walimu Malofa' nao ni Ukweli.
 
[mention]Mshana Jr [/mention] uzi wako umeuandika vizuri sana.

Ila kitu ambacho sikubaliani na wewe ni kuwa umeongea sweet talk ambayo imekuwa ikiongelewa miaka yote, nadhani ni muda wa hard talk, bila kuvaa buti hao wanasiasa na wachumia tumbo hawawez kuthamini ualimu.

Ni heri tusemwe ili walimu tuamke na hata KUGOMA mbeleni huko ili haki zetu zizingatiwe
 
True

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Msifanye hayo gizani na nyuma ya pazia.. Jitokezeni live tuwaunge mkono
 
Walimu wanahitaji kuboreshewa maslahi yao ili waondokane na fedheha pamoja na frustration mbalimbali zinazopelekea wakose matumaini katika maisha yao.
MUHIMU
serikali iweke teaching allowance teaching allowance

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Mshahara mdogo kazi kama zote, kwa kipindi hiki ukinunua mchele kilo ishirini, korie litre 5 unga, maharage mshahara wote umekwisha...unaanza kuzihesabu siku.... Kiukweli Kuna kitu kipo moyoni mwangu Mungu azidi kunipa utulivu na uvumilivu....nimepanga kutokomea mashambani huko nikachimbe visima yawe maisha yangu kwa uhuru.
 
Mpwayungu hakua na Maana ya kuwatukana au kuwadhalilisha, Mpwayungu alikua anawatia Hasira ili muamke, mjue mnachotaka maishani .

Wee ukiwa Masikin, mtu akikutukana, Masikin mkubwa weee..,..... Hajakuonea na Wala wewe kukataa kua sio Masikin ,hakukufanyi uwe mwenye Kipato !!.



Msijifariji Walimu !!!!

Nadhan mnahaja ya kuungana kudai Masilahi yenu.


Hamna watu wenye Maisha magumu Tanzania hii kama Walimu, Wana Maisha magumu mnoo kwelikweli.


Hii mitandao na ID fake, zisiwaondoe kwenye uhalisia wa Maisha, tunaishi nanyinyi huku mitaani na tunawaona mnavyoishi.


Kujifanya mmeridhika na hali zenu, ni kujilisha upepo.

Mimi Binafsi, Haitokaa kamwe itokee Mwanangu asome Ualimu Kwa hali hii nayoiona na kama itaendelea hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…