Kaliba ya Ualimu lazima iheshimiwe

Kaliba ya Ualimu lazima iheshimiwe

Usijizime data, walimu ndio wamekua wasimamizi wakuu katika vituo vya kura au ulikua hujazaliwa, na huez iba kura bila kushirikiana na msimamizi mkuu wa kituo cha kura. Ninaongea ninachokijua
Kuna siku kada ya ualimu itasimama na kuheshimika tena!
 
Usijizime data, walimu ndio wamekua wasimamizi wakuu katika vituo vya kura au ulikua hujazaliwa, na huez iba kura bila kushirikiana na msimamizi mkuu wa kituo cha kura. Ninaongea ninachokijua
Narudia tena wanajamii forum wa Sasa mmelifanya likawa jukwaa la hovyo Sana Sana!! Na kama wewe ni msomi!? Dah!!ndio tunaambiwa wasomi watz hawaajiriki!!
1) ni hivi!??mwalimu hahusiki na chochote kwenye wizi wa kura!! Mimi sio mwalimu ila nimesimamia chaguzi mara mbili!! .walimu KAZI zao ni kukata kura ( Ile karatasi ) kujaza takwimu kutoka kitambulisho Cha taifa kwenye karatasi!!
,Kisha,kumuelekeza mpiga kura namna ya kutumbukiza (ballot paper) kwenye box husikia!!
2) baada ya kura kupigwa na kituo kufungwa ,kura huhesabiwa na watu kutoka nec na mawakala wa vyama!!
3) matokeo ya kituo hujazwa kwenye form na mawakala wa vyama husaini!!
4) matokeo hubandikwa na raia hapata mrejesho!! Wa kituo husikia!!
5) matokeo mengine nakala hupeleka hukoo halmashauri!! Kwa majumuishi ili kutangaza washindi!!
Swali langu !! Hapa mwalimu anaibaje kura!?? Hebu tueleze mwalimu anawezaje kukisaidia CCM!!
Narudia kusema jamii forum imepoteza sifa!! Wanajukwaa wanaulewa mdogo mnooo!! Mpaka Huwa nashangaa Sana!!
 
Hebu usiandike mengi ukaonesha jinsi usivyojua kitu, hivi unajua michongo ilikua inafanyika wakati gani, unajua kwann walimu ndo walikua wanachaguliwa kuwa wasimamizi wakuu. Siendelei tena ili usipate faida ila jua tu ili waalimu wapate heshima yao waache kujifanya wao ni tawi la chama
 
Mtu ni mwalimu analipwa chini ya laki 5,hapo hajakopa,madeni kibao kitaa,mwalimu anakopa Kwa Kila mtu
Toa data Mzee huyu ni WA level Gani!? Je kada nyingine zenye level kama hiyo ya mwalimu wanalipwaje!??
Mfano twambie mwenye certificate ya maendeleo ya jamii ,mwenye certificate ya Uhasibu analipwaje!? ,Mwenye certificate ya mifugo analipwaje!!,mwenye certificate ya kilimo analipwaje!?? Je kama wote ni watumishi wa umma wanatofauti na mwalimu mwenye certificate!??
Narudia,Kuna uelewa mdogo mno humu kwenye jukwaaa watu wengi hawajui kitu Wana urge kitoto sana!!!!
 
Hebu usiandike mengi ukaonesha jinsi usivyojua kitu, hivi unajua michongo ilikua inafanyika wakati gani, unajua kwann walimu ndo walikua wanachaguliwa kuwa wasimamizi wakuu. Siendelei tena ili usipate faida ila jua tu ili waalimu wapate heshima yao waache kujifanya wao ni tawi la chama
Hahaha aisee !?? Pole Sana Kwa staili hii kweli hamuajiriki!! Lakini kuniambia mwalimu anaiba kura hapana hapa mnawaonea hawahusiki kabisa kabisa !! Nakwambia nimeona mwenyewe kama ni kuibuwa ni kwingine sio kituoni
 
Mshana utakuwa ni miongoni mwa wale walokomba mamilioni benk ya walimu🤣🤣 (natania)
Kuna muda people must learn in a hard way, haya mambo ya kurembana rembana na kukosoana Kwa staha ndo yametufikisha hapa tulipo, Hadi Leo ripoti ya CAG ni kichefu chefu, watu wanajipigia tu.

Sasa ina maana gani kumsifia mwalimu na kumremba huku maslahi yake ni duni na hamna mpango wa kumboreshea....hayo mambo ya ualimu ni wito yalikuwa enzi ya ujamaa, sasa ni ubepari, capital ndo kila kitu....Mwalimu alipwe vizuri kuendana na hali ya maisha....sifa hazipeleki chakula mezani.

Katika ulimwengu wa kibepari pesa ndiyo kila kitu, lipa walimu vizuri heshima irudi, nidhamu ya wanafunzi irudi, watoto wafaulu taifa lisonge mbele.....Nani atamuheshimu mwalimu anayevaa suruali ya njano, mkanda uliopauka na Shati la kitenge mpauko?
Walimu woteeee ni malofa hakuna mwenye ahueni.
 
Nakuheshimu sana bro, ila unadhani ni uongo katika yote yaliyoongelewa? Sema mada ziliwasilishwa katika lugha zisizo za staha. Lakini ni ukweli asilimia 100 waalimu wetu wana changamoto nyingi na hata wewe hujataja hata moja, zaidi umezunguuka tu.
Unamuheshimu mlevi?
Oyaaa hastahili hiyo kitu
 
Kusema ualimu ni kazi ya laana ndio ukweli?
Tena ni kazi ya kiduanzi mno kwa hapa bongo.
Wewe una nini hapo ulipo zaidi ya ulevi na kushinda JF yani wewe ni sawa na ma-jobless umebakisha uchawa wa kuwasifia wenye JF

Ndo tabia za walimu hizo full kujishobokesha, maisha magumu, vimikopo vingiii, biashara za kiduanzi kibaooo na wewe unatabia ya kuombea sana watu ban SIJAKUSAHAU sijui platform unahisi iko hii tu 🚮
 
Tena ni kazi ya kiduanzi mno kwa hapa bongo.
Wewe una nini hapo ulipo zaidi ya ulevi na kushinda JF yani wewe ni sawa na ma-jobless umebakisha uchawa wa kuwasifia wenye JF

Ndo tabia za walimu hizo full kujishobokesha, maisha magumu, vimikopo vingiii, biashara za kiduanzi kibaooo na wewe unatabia ya kuombea sana watu ban SIJAKUSAHAU sijui platform unahisi iko hii tu [emoji706]
Wewe una nini hapo ulipo zaidi ya ulevi na kushinda JF yani wewe ni sawa na ma-jobless umebakisha uchawa wa kuwasifia wenye JF [emoji3][emoji3][emoji3]
What a wasted manii..[emoji848][emoji2827]
 
Maslahi yangu: Mimi ni mwalimu kwa kusomea.

Nimefarijika na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa JamiiForums kwa kuondoa/kufuta mada zote zinazowadhalilisha walimu na kada nzima ya ualimu na kuwapa adhabu stahiki wale wote waliokuwa vinara kwenye hilo.

Kuna mahali tuliyumba na tukakosea sana, tukakosea pakubwa napo ni pale tulipoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma. Kwamba mwanasiasa hohehahe wa elimu ana thamani kubwa na heshima stahiki kuliko mtu mwenye ujuzi wa elimu ya kusomea kama mwalimu, ama kama daktari. Haya yanayotokea sasa ni madhara ya matokeo ya kuwatukuza na kuwakweza wanasiasa.

Mwalimu ndio msingi wa maarifa yote ya ulimwengu na hapa nazungumzia walimu katika hatua ile ya awali/msingi ya kufundishwa kuumba herufi, kusoma, kuandika nk. Huko mbeleni hakuna changamoto kama hii hatua hii ya awali. Hivyo kumheshimu mwalimu sio jambo la hiari bali ni jambo la lazima.

Rais wa kwanza mweusi wa Tanganyika ni hayati Julius Kambarage Nyerere, lakini jina hilo halina ladha kabisa bila kutanguliza neno MWALIMU. Huyu alikuwa ni mwalimu kwa ujuzi na Marais wengine waliofuatia karibia wote walitokea kwenye ualimu. Ualimu ndio msingi wa maarifa yote.

Baada ya vita ya Kagera 1977-1979 nchi iliyumba kwenye nyanja nyingi na kaliba ya ualimu haikuachwa nyuma. Kufikia mwanzoni mwa miaka ya 80, Mwalimu katika kuhangaika huku na kule kutafuta usaidizi wa kielimu kiuchumi nk ndio akapata usaidizi wa UNESCO waliokuwa na program ya UPE (Universal Primary Education) Elimu ya Msingi kwa Wote.

Kufanikisha hili ikabidi kuwe na program ya kuwachukua watu wazima na kuwapiga brush ya elimu ya ualimu ili waweze kufidia nakisi ya walimu wa elimu ya awali kutokana na watoto kuandikishwa kwa wingi sana.

Program ya UPE kwa bahati mbaya ikapewa jina la dhihaka na waswahel waliooita Ualimu Pasipo Elimu.. Hili nalo lilikuwa kosa ambalo madhara yake yalikuja kuonekana baadae. Program ya UPE ilikuja kufutwa na Mzee Ruksa kama sio Mkapa.

Kiasili kaliba ya ualimu ni kaliba iliyokuwa inaheshimika sana. Maana mwalimu alichukuliwa kama kiumbe aliyeelimika kuliko wengine, mwenye maarifa mengi, ujuzi hekima, ufahamu mkubwa na jasiri muongoza njia. Mwalimu ndio aliaminiwa kwa kazi kubwa kubwa za kitaifa kama sensa, takwimu, chaguzi mbalimbali nkn.

Wakati huo kuitwa mwalimu ama kuwa mtoto wa mwalimu ilikuwa ni heshima sana kutokana na umuhimu wake kwenye jamii.

Vipaumbele na maono ya taifa ndio vilikuja kuitia doa kubwa kabila ya ualimu hasa pale walipoamua kuipa thamani kubwa siasa na kuisahau taaluma.. Kuteuliwa kwa wanasiasa kuongoza taasisi nyeti kama ELIMU ilikuwa kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la walimu.

Zikaanza sarakasi kipindi cha Mkapa kuelekea Kikwete. Kukaletwa program kama za UPE lakini kipindi hiki wakiwachukua vijana waliofeli kidato cha nne, zile program zikapewa majina ya dhihaka kama voda fasta nk.

Kumpika mtu mpaka aje kuiva kuwa mwalimu si jambo dogo, sasa wale walimu wa miezi sita na mwaka mmoja tena waliofeli kidato cha nne sijui walifundishwa nini kwakuwa hata ukiwauliza haiba ni kitu gani ama misingi na falsafa ninini hawajui.

Kufikia hapa ndio kaliba ya ualimu ikawa imepoteza heshima, mvuto ustaarabu. Vijana barobaro wasioiva kihaiba ndio wakawa walimu, wanasiasa wakaanza kuwatumia kwa manufaa yao. Ualimu ikawa ni kichochoro cha kutumika na wanasiasa.. Wakaleta chama cha walimu na bank ya walimu. Yaliyofuatia yote ni msiba wa kuhuzunisha.

Hawa vijana wa sasa wanaokosoa na kudhihaki hii kaliba ni kizazi kile cha walimu wa mwendokasi na vodafasta. Ualimu ni Wito sio mbadala wa ajira. Hawa walienda kwenye ualimu kama mbadala baada ya kufeli na kukosa kaliba ya ndoto zao.

Hawa hawajapikwa wakaiva maana hata hivyo hawana wito ni makanjanja wa maisha wenye kinyongo kikubwa na kushindwa kwenye mengi. Wana nyongo za kutapika lakini wameshindwa kufanya hivyo kwenye mitandao mingine kwakuwa watatumia utambulisho binafsi na ni rahisi kujulikana.

Hawa walitaka kuitumia JF kama uchochoro wa kutoa hasira zao na kuidhalilisha kada ya ualimu kwa kutumia faida ya utambulisho bandia bila kujali kwamba kwa kufanya hivyo wanaishushia hadhi forum na kuwapa shida wamiliki wanaojulikana kwa majina, sura na hata mawasiliano yao.

Hata mitume wengi kwenye imani zetu walikuwa ni walimu. Ualimu ni kazi ya kiroho na ni kazi ya wito. Iheshimiwe, itambuliwe, ithaminiwe na kupewa hadhi inayostahili. Wanasiasa walione hili na kulifanyia kazi.

Mungu ibariki JamiiForums
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu wabariki Walimu
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom