Kaliba ya Ualimu lazima iheshimiwe

Hao sio walimu kwa wito
Hao sio walimu waliopikwa wakaiva
Hao sio walimu waliokomaa kiakili na kifikra
Hao sio walimu waliosoma na kufaulu masomo ya haiba, misingi na falsafa
Kuna wale walimu wa Voda fasta, na wale waliopata mafunzo meaka mmoja. Wameteuliwa kuwa maafisa Elimu taaluma na takwimu wapo mikoani huko wanavaa vitenge. Na ni wakina mama na matacle makubwa ukimkuta utaamini tu lipo jambo. Wale waliomaliza Cuba watakuwa wamenielewa
 
Mkuu hao waliopo kwenye kada zingine kuna mianya ya Rushwa,semina ,overtime allowance kwaio anaweza kulipwa Tsh 300,000/= lakini maisha yake yasifanane kabisa na Mwl.kwaio hapa point ni mwl aboreshewe maslahi kidogo ili asiishi kinyonge.Hili litampa motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na hatimae tutajenga taifa imara lenye watu wenye maarifa,maadili na uzalendo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Ualimu ni kazi achana na bla bla za wito.

Pamoja na kufanga thread za Mpwayungu na wengine wako sahihi kabisa. Bila kelele kudai haki kamwe wasitegemee maboresho ya maana.
Wito ni karama .. Ile ni ajira kwahiyo hakuna niliposema kwakuwa ni wito basi wafanye kazi katika mazingira magumu
 
Kwanza uwalimu sio wito tuache kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa taaluma za watu tulizoshindwa kuziboresha kwa visingizio vya kishenzi kama hivyo.

WITO huwa haujali maslahi ya pesa wala aina ya mazingira ya kazi zaid ya kujali lengo la kazi tu.

Niwaambieni enyi walimu nyie hamna wito wowote bali mnatimiza wajibu wenu kwa serikali na kupata haki zenu za mishahara baada ya kuhitimisha kazi za kila mwezi, pia niwaambien nyie wanasiasa na raia achen kuwapotosha walimu kwa majina mengi ya kuwapamba, wao hawana uspecial wowote wa kuwapa hayo majina mnayotumia kuwadanganya ili muwanyonye, kuna kada nyingi ambazo ni muhimu kwa jamii kama vile Utabibu, ulinzi, na zinginezo za muhimu na mnaishi sababu ya uwepo wa hawo je kwann hamuwaiti na hawa kuwa wana Wito zaid ya kuwapamba walimu?

Kazi ya wito ni ile ambayo malipo yake ni sawa na = 0'' yaan mfanyakazi hatak malipo yoyote zaid ya kutimiza majukumu, hivyo basi tuhitimishe kwa kuwaita walimu wote ni wafanyakazi wa kawaida sana kama walivyo wafanyakazi wengine.

Wito hapa dunian ni kujitoa kwaajili ya manufaa na maendeleo ya wengine bila kujali maslahi ya kiuchumi,

Serikali ingekuwa makini walimu wangeheshimika kulko hata hao wabunge ambao hawana manufaa kwa taifa zaid ya kuharibu hii nchi kwa kukosa misimamo.
 
Wito ni karama .. Ualimu ni ajira kwahiyo hakuna niliposema kwakuwa ni wito basi wafanye kazi katika mazingira magumu
 
Umeongea maneno kuntu.

Ualimu siyo wito, "is a professional job" yenye kufuata kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Tukisema ualimu ni wito maana yake Mwalimu hapasi kusurutishwa na kanuni zozote zile (mtazamo wangu). Lakini, Mwalimu huyo huyo Kila kukicha maazimio na miongozo kede kede Kutoka Kwa Wakubwa/wanene inapelekwa kwake Kwa ajili ya kumsurutisha ktk kazi yake ya ualimu.

Changamoto ziko nyingi sana katika kada ya ualimu; hivyo, ni jukumu la Serikali kuwatazama walimu Kwa muktadha chanya na si kuwafanya wanyonge kila kukicha. Na ndiyo sababu ya jamii Pana ya Watanzania kuendelea kuwadharau/kutudharau.

Nampongeza mleta mada (Mshana Jr ) kaja na mada ya kuwapooza Walimu (Kwa maneno matamu) Kwa kuwa yeye kama yeye anatambua thamani ya ualimu na Walimu kiujumla (tumpongeze Kwa hili). Lakini bado ukweli uko pale pale Walimu wanakabiliwa na changamoto lukuki ambazo nyingine nyingi tu zinasababishwa na mabosi wa Walimu.

Nawasilisha. [emoji1812][emoji3578] Mwalimu Blue Bahari
 
Asante Mwalimu Blue Bahari kwa uchambuzi mzuri[emoji1545][emoji1752]
 
Asante Mwalimu Blue Bahari kwa uchambuzi mzuri[emoji1545][emoji1752]
Nawe pia ubarikiwe [emoji120][emoji120][emoji120] Kwa kujaribu kutuheshimisha sisi Walimu. Ila Bahati mbaya tafsi ya heshima Kwa Mwalimu ni tofauti na jamii inavyotafsiri.

Kinachoheshimika siku hizi ni Pesa na si mtu au mtaalamu wa fani. Wewe mtaalamu wa fani flani, watu watakuuliza una nini?, Nazungumzia "material things".
Haujakosea kabisa kuleta uchambuzi murua wa thamani ya Mwalimu na ualimu kiujumla, ila tatizo ni nyakati.
 
 
Kwani "lofa" ni tusi? Mbona Marehemu Mkapa alituita watanzania wote malofa, ulofa ni sifa ya mtu asiyejielewa, ni kivumishi tu Kama ilivyo mjinga....sa mtu awe lofa umuite mjanja?
Mkapa hajawahi kutuita Watanzania wote Malofa.
 
Ukiruhusu uhuru wa kutoa maoni, kubali kusikia ukweli usioupenda....JF wamekosea..warudishe hizo nyuzi
Hapo ndio utafahamu kuwa democrasia huwa ni ngumu sana. Ukipenda democrasia na uhuru wa maoni ni lazima uwe tayari kusikia ukweli usio upenda au la sivyo ukubali kuitwa dictator.
 
Hapo ndio utafahamu kuwa democrasia huwa ni ngumu sana. Ukipenda democrasia na uhuru wa maoni ni lazima uwe tayari kusikia ukweli usio upenda au la sivyo ukubali kuitwa dictator.
Mimi nashangaa JF kuziacha zile nyuzi zinazomkashfu JPM mtu ambae hawezi kujitetea na kuzifuta za walimu ambao wanaweza kuja kukanusha kama yanayosemwa ni ukweli au uongo
 
Waulize vizuri watakwambia ukweli !! Sisi tupo huko Hali haiko kama mnavyodhani!! Niambie mtu yupo maendeleo ya jamii Kuna rushwa Gani na shiling ngapi!??hizo simina ni lini na lini!? Overtime lini na lini!?allowance zipi!? Mara ngapi zipo!?! .
Nasema tena jamii forum uelewa wa watu ni finyu mno!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…