Nina wasiwasi sana na elimu yako ya uhifadhi.
Unaposema masikini alienda kujitafutia chochote hifadhini maana yake unahalalisha watu masikini kuingia hifadhini kujutafutia, well watanzania karibu 90% ni masikini, tungeruhusu kila mwananchi masikini "kujitafutia chochote" hifadhini leo hii tusingekuwa na hifadhi hata moja. Wake up.
Pili, hifadhi zinalindwa kwa faida ya watanzania wote. Mapato yanayotokana na uhifadhi yanaingia serikalini na kumsaidia kila mtanzania hata asiye jirani na hifadhi.
Ni kweli jamii jirani ni vizuri ikashirikishwa kwenye uhifadhi, lkn hii haimaanishi lazima kuwe na direct flow ya mapato kutoka hifadhini kwenda vijijini. Faida za uhifadhi sio pesa tu, hata faida za kiikolojia ni muhimu. Leo hii tunalalamika mvua hakuna ni sababu ya matendo yetu wenyewe ya uharibifu wa mazingira.
So, jaribu kuwaza holistically utaona sio busara kutumia neno masikini anajitafutia chochote. Mbona mtu haendi kuvunja duka la mtu kuiba kwa kigezo cha yeye masikini anajitafutia chochote? Sheria za kuhifadhi zimetungwa wakijua kuna watu masikini!