huyu ukweli anaujua ila anajitia ufyatu kwamba haelewi na anajifanya anahoja Sana kumbe nihoja zakitototu.Jamaa kaleta madai na tuhuma zake halafu anataka kujadiliwe kwanini hayo anayotuhumu yamefanyika na sio kutaka kuhakiki ukweli wa anayo tuhumu. Mfano kaja anadai Qur'an imeiba maandiko kutoka kwenye biblia hivyo anataka ajibiwe kwanini Qur'an iibe maandiko kwenye biblia na hataki kuwlezwa tofauti na hayo madai yake ndio maana hata ukimjibu ila tofauti na kumwambia kwanini Qur'an iibe maandiko basi hatambui kama umemjibu kabisa.
nimekupata hapa Bali ninaswali moja naomba unijibu Kama unaamini kua kiladini inamungu wake na kitabu chake sasanataka kujua dunia tunayo ishi nakilakitu chake ninani kaiumbaKila taifa lilikuwa na Mungu wake na sio kila taifa tuu Bali kila kabila.
Sasa Jambo dogo Kama hilo ulikuwa haulijui?
Kwa hiyo Kwa Uelewa wako Waarabu walimvyomleta Allah huku Afrika unafikiri hawakukuta Waafrika tukiwa tunaabudu miungu yetu?
Au unafikiri tulikuwa tunamuabudu Allah au Yehova?
Elewa kuwa, Hata hapa Tanzania kila kabila lilikuwa na mungu wake.
Na tofauti ya miungu ndio huzaa tofauti za Mila na desturi na miiko.
Elewa kuwa kila taifa au kila kabila wanaamini mungu wao ndio aliumba dunia,
Elewa kuwa kila taifa linaloamini katika mungu wao huamini miungu mingine kuiabudu ni upagani na ukafiri.
Elewa kuwa Biblia na Quran sio kwamba zilipoletwa Afrika basi Waafrika walizikubali Kwa hiyari isipokuwa walipigwa wakateswa na wengine kuuawa mpaka wakazikubali hizo dini, hiyo miungu ya kigeni pamoja na vitabu vyao hizo Quran na Biblia.
Kwa hiyo kamwe usijesema Allah au Yehova ndio mungu wa Dunia au mungu wa wote. Anayesema hivyo yeyote asiye muarabu au myahudi kuna mahala atakuwa Hana Uelewa na mambo ya kihistoria na Kidini.
Ndio maana hapa tunapojadili vitabu hivyo, tunajadili katika muktadha wa kimahakama baina ya vitabu hivyo kuwa Nani kamuibia mwenzake materials kwani hizo jamii ni mbili tofauti zenye miungu miwili tofauti, zenye tamaduni tofauti na historia tofauti.
Bado tuu hujaelewa mantiki ya andiko hili.
Haina haja ya kujibu nishaelewa kwamba kila taifa lina Mungu wake, hiyo ndio point ya msingi.
Asante sana kwa kunipa elimu hiyo msomi nilikuwa sijui.
Kwema Wakuu!
Kutokana na mjadala fulani uliokuwa unaendelea katika Jukwaa la Intelligence nimeona nianzishe uzi huu kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia kupima katika mizania ya kimahakama/kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.
Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?
Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi, bali nipo kujadili nani mkweli kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama, majaji mtakuwa ninyi wasomaji.
Mahakamani siyo kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa sheria, hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.
Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema kwa vile mambo haya yanagusa imani za watu jambo hilo linaweza kuwa gumu.
Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa rejea kuu zaidi ya Quran, kwa sababu;
1. Biblia kwa sehemu kubwa haina maneno ya 'Hearsay' wakati Quran kwa 90% maneno yake ni 'Hearsay'. Kimahakama maneno ya 'hearsay' hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu. Hoja hii ndiyo hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.
a) Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, Yona n.k.
Wakati msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo. Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita. Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.
Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, Mathayo na Yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu waliyoshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya. Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka kwa sababu yeye alisimuliwa.
Hata hivyo ulikuwa ni wakati ule ule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka. Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.
2. Waandishi wa Biblia walikuwepo maeneo tajwa kwenye Biblia, lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika maeneo anayoyasimulia. Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na Waisrael ambapo hajawahi kufika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.
Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman halafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman, wakati Suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.
Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia. Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.
3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.
Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo!😀😀
Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.
Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi kwasababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni kama vile kitabu cha Mzee wetu Mwinyi au Mzee wetu Mengi.
Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay), kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa ukweli na ikachukuliwa kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.
4. Biblia imeandikwa na Wayahudi kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu kwa lugha ya Kiarabu lakini inasimulia habari za wasiyo Waarabu, inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.
Yaani mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo. Hivi ninyi mtanisikiliza mimi Mpare ninayesimulia habari za kale za Wasukuma au mtasikiliza Wasukuma wenyewe?
Muhammad Muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo halafu yeye anakwambia alizaliwa kwenye mtende halafu kuna mtu Myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye hori la ng'ombe.
Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni Myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza nani?
Haya Quran na hadithi za Kiyahudi kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji wa Daudi na mwanaye Suleiman, hajui Kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.
Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini, lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo majini. Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika vitabu vyake vilivyopo katika Biblia? Jibu utabaki nalo.
5. Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa Waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah, Mungu wa Waarabu wa kabila la Wakurdi wa zamani lakini cha ajabu huyo Allah, ati huyo Allah kuna sehemu anamuagiza kina Musa (Myahudi na dini yake Uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.
Hata hivi leo Mungu wa Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu wa waarabu hajabadilika ni yule yule Allah. Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa Muarabu.
Wahusika kuanzia kwa Yakobo mpaka kwa Yesu ni Wayahudi na dini yao ni Uyahudi na Mungu wao ni Yahweh, lakini Quran imepuyanga katika eneo hilo.
6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran, siyo ajabu Quran yenyewe ndiyo imenakili baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.
Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndiyo baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovinakili kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya Kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile.
7. Mtiririko na visa na matukio ya Kihistoria.
Biblia ni kitabu ambacho kimeandikwa Kwa kufuata mtiririko wa visa na matukio unaoleweka. Kuanzia kisa cha Adamu mpaka Yusufu anachosimulia Musa, Kisha tawala za dunia kama Tawala la Nimrodi, kisha tawala la mafarao, kisha tawala la Waashuru na Wakaldayo, kisha wakafuata Waajemi na Wamedi, kisha wakafuata Wayunani/wagiriki, kisha wakafuata Warumi ndipo alipozaliwa Yesu.
Lakini Quran haina mtiririko wa visa na matukio, kumaanisha haiwezi kutumika hata shuleni Kama rejea za kihistoria kuhusu tawala, au mambo ya kuitawala au Kisiasa kwani Quran haijui wapi dunia imetoka ilipo na wapi inapoenda. Wakati Biblia inaeleza wapi Dunia ilipotoka na wapi ilipo na inapokwenda.
Quran inaweza kuulizwa swali, Yesu alizaliwa wakati WA utawala gani na wanani na ukashindwa kujibu?
Kimahakama Quran kama haijui baadhi ya taarifa muhimu kama Zama na Maeneo husika ya tukio lilipotukia haiwezi kutumika kama Rejea au ushahidi muhimu katika mambo ya Kidini.
Kwa mfano; Issa kazaliwa kwenye mtende Kwa mujibu wa Quran lakini haielezi ni eneo gani au nchi gani Issa alizaliwa, hata Hapa Tanzania ipo mitende, hii ni tofauti na Biblia inataja na kuelezea visa katika mtiririko uliokamilika.
8. KUjitosheleza, kujitegemea na kutoa taarifa zote muhimu.
Biblia inajitosheleza na kujitegemea Biblia kuhusisha kitabu kingine. Msomaji yeyote wa Biblia akimaliza kuisoma hatahitaji rejea za kitabu kingine.
Mfano msomaji akisoma kisa cha Yakobo, atajua Yakobo alizaliwa wapi, ndugu yake ni Nani, Routes zake zote, wake zake, watoto wake na umri wake mpaka anakufa. Kwa nini aliitwa Yakobo, ikawaje akabadilishwa jina n.k
Lakini Quran haijitoshelezi haina hizo taarifa muhimu. Hivyo kuifanya Quran kuwa tegemezi Kwa vitabu vingine.
Quran ambacho ingefanya ni kutoa nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na siyo kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo. Mbona Injili haujarudia visa? Quran haiwezi kuchukuliwa kama rejea kuu kuzidi Biblia kwa sababu nilizozitaja hapo juu.
Majaji mjadili kwa hoja.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
nimekupata hapa Bali ninaswali moja naomba unijibu Kama unaamini kua kiladini inamungu wake na kitabu chake sasanataka kujua dunia tunayo ishi nakilakitu chake ninani kaiumba
Mbona wewe unamfuata Paulo aliyemgeuza Yesu kuwa Mungu kwa wewe kumwabudu yesu Kama Mungu?Kumbukumbu la Torati 6:14
Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;
Ukitaka kujua majina(proper name/personal name) ya miungu ya mataifa kama Misri, Kanaani, Yordan, Moabu, Waajemi, Wamedi, warumi yote ipo Kwa Majina ninaweza kukutajia with Reference.
Na pia ukitaka kujua mungu wa waarabu nitakutajia achilia mbali huyo Yehova Mungu wa Wayahudi.
Ndio maana watu wote wenye maarifa, ufahamu, elimu na Ujuzi watashangaa wakisikia wakisema Allah akamuambia Musa au Daudi au Yesu ilhali Allah sio Mungu wa Wayahudi. Huo utakuwa ni uongo mkubwa ambao hautavumiliwa.
Au mtu aseme Torati, injili, Zaburi na maandiko yote ya kiyahudi ati yawe yametoka Kwa Allah, huo ni upotoshaji na wanaopotoshwa na watu wasioelimika au walioamua kupotoka.
Au Yehova amuagize Muhammad muarabu yaani huo utakuwa uongo mkubwa
Huu udini unakusaidia nini?
Mimi mbona nakuelewa vizuri tu na si ndio maana toka mwanzo nilikwambia kuwa Qur'an na Biblia ni vitabu vya dini kwa maana vya kiimani hivyo hakuna namna unaweza kujadili hivyo vitabu kwa kuweka pembeni msingi wa hivyo vitabu kwamba ni imani.Kila taifa lilikuwa na Mungu wake na sio kila taifa tuu Bali kila kabila.
Sasa Jambo dogo Kama hilo ulikuwa haulijui?
Kwa hiyo Kwa Uelewa wako Waarabu walimvyomleta Allah huku Afrika unafikiri hawakukuta Waafrika tukiwa tunaabudu miungu yetu?
Au unafikiri tulikuwa tunamuabudu Allah au Yehova?
Elewa kuwa, Hata hapa Tanzania kila kabila lilikuwa na mungu wake.
Na tofauti ya miungu ndio huzaa tofauti za Mila na desturi na miiko.
Elewa kuwa kila taifa au kila kabila wanaamini mungu wao ndio aliumba dunia,
Elewa kuwa kila taifa linaloamini katika mungu wao huamini miungu mingine kuiabudu ni upagani na ukafiri.
Elewa kuwa Biblia na Quran sio kwamba zilipoletwa Afrika basi Waafrika walizikubali Kwa hiyari isipokuwa walipigwa wakateswa na wengine kuuawa mpaka wakazikubali hizo dini, hiyo miungu ya kigeni pamoja na vitabu vyao hizo Quran na Biblia.
Kwa hiyo kamwe usijesema Allah au Yehova ndio mungu wa Dunia au mungu wa wote. Anayesema hivyo yeyote asiye muarabu au myahudi kuna mahala atakuwa Hana Uelewa na mambo ya kihistoria na Kidini.
Ndio maana hapa tunapojadili vitabu hivyo, tunajadili katika muktadha wa kimahakama baina ya vitabu hivyo kuwa Nani kamuibia mwenzake materials kwani hizo jamii ni mbili tofauti zenye miungu miwili tofauti, zenye tamaduni tofauti na historia tofauti.
Bado tuu hujaelewa mantiki ya andiko hili.
Hilo ni swali gumu Sana Kwa sababu kila mungu wa kila jamii anatamba kuwa ndiye muumbaji.
Ukienda Kwa Wachina wao wanaamini Mungu wao ndiye kaumba dunia, alafu wao hawana Stori ya Adamu na Hawa.
Stori ya Adamu na Hawa zipo Kwa hizi Dini zenye Asili ya Abrahamu ambazo ni Ukristo, uislam na uyahudi na Dini zingine ndogondogo ambazo sio maarufu.
Ukizisoma Kwa kina hizo dini zote utakuja kugundua kuwa miungu hiyo ndio inafanya uwepo wa atheist kwani miungu hiyo kuna mahali pengi imeonyesha ubinadamu zaidi kuliko uungu.
Hata hivyo Kwa Uelewa wangu naamini,
Kama kila mtu alivyo na Baba yake mzazi ndivyo kila jamii ilivyo na Baba yake Kiroho yaani mungu wa jamii Fulani.
Na yupo Mungu wa miungu ambaye ndiye aliyeumba wote na vyote.
Ila yeye haonekani na hatakuja aonekane.
Ninaamini kila jamii inamungu wake.
Aliyepewa majukumu ya kuwalinda watu wa jamii hiyo na MUNGU MKUU asiyeonekana.
Ila Allah na Yehova wote ni miungu lakini sio Yule Mungu Mkuu
Mtoa mada nimjuaji asie jua chochote tumuache ajifurahishe asongeshe sikuzake zakuishi sikuyake iwadie akakutane na mashangazo ndio atakapo jilaumu lakini itakua ashachelewa.
Kuamini nako kuna sababu, sasa wewe mwenzetu unaamini kwa sababu zipi?Hilo ni swali gumu Sana Kwa sababu kila mungu wa kila jamii anatamba kuwa ndiye muumbaji.
Ukienda Kwa Wachina wao wanaamini Mungu wao ndiye kaumba dunia, alafu wao hawana Stori ya Adamu na Hawa.
Stori ya Adamu na Hawa zipo Kwa hizi Dini zenye Asili ya Abrahamu ambazo ni Ukristo, uislam na uyahudi na Dini zingine ndogondogo ambazo sio maarufu.
Ukizisoma Kwa kina hizo dini zote utakuja kugundua kuwa miungu hiyo ndio inafanya uwepo wa atheist kwani miungu hiyo kuna mahali pengi imeonyesha ubinadamu zaidi kuliko uungu.
Hata hivyo Kwa Uelewa wangu naamini,
Kama kila mtu alivyo na Baba yake mzazi ndivyo kila jamii ilivyo na Baba yake Kiroho yaani mungu wa jamii Fulani.
Na yupo Mungu wa miungu ambaye ndiye aliyeumba wote na vyote.
Ila yeye haonekani na hatakuja aonekane.
Ninaamini kila jamii inamungu wake.
Aliyepewa majukumu ya kuwalinda watu wa jamii hiyo na MUNGU MKUU asiyeonekana.
Ila Allah na Yehova wote ni miungu lakini sio Yule Mungu Mkuu
Jamaa kaleta madai na tuhuma zake halafu anataka kujadiliwe kwanini hayo anayotuhumu yamefanyika na sio kutaka kuhakiki ukweli wa anayo tuhumu. Mfano kaja anadai Qur'an imeiba maandiko kutoka kwenye biblia hivyo anataka ajibiwe kwanini Qur'an iibe maandiko kwenye biblia na hataki kuwlezwa tofauti na hayo madai yake ndio maana hata ukimjibu ila tofauti na kumwambia kwanini Qur'an iibe maandiko basi hatambui kama umemjibu kabisa.
kwahio huyo mungu mkuu ndio kaumba dunia nakilakitu ikiwemo sisi?na hakutuwekea sheria yoyote?walahakuandika kitabu chochote kitakacho tuongoza? kamahawa miungu wengine walivyo fanya kutuandikia vitabu vyao ambavyo vinatuongoza sisi tunao waamini.Hilo ni swali gumu Sana Kwa sababu kila mungu wa kila jamii anatamba kuwa ndiye muumbaji.
Ukienda Kwa Wachina wao wanaamini Mungu wao ndiye kaumba dunia, alafu wao hawana Stori ya Adamu na Hawa.
Stori ya Adamu na Hawa zipo Kwa hizi Dini zenye Asili ya Abrahamu ambazo ni Ukristo, uislam na uyahudi na Dini zingine ndogondogo ambazo sio maarufu.
Ukizisoma Kwa kina hizo dini zote utakuja kugundua kuwa miungu hiyo ndio inafanya uwepo wa atheist kwani miungu hiyo kuna mahali pengi imeonyesha ubinadamu zaidi kuliko uungu.
Hata hivyo Kwa Uelewa wangu naamini,
Kama kila mtu alivyo na Baba yake mzazi ndivyo kila jamii ilivyo na Baba yake Kiroho yaani mungu wa jamii Fulani.
Na yupo Mungu wa miungu ambaye ndiye aliyeumba wote na vyote.
Ila yeye haonekani na hatakuja aonekane.
Ninaamini kila jamii inamungu wake.
Aliyepewa majukumu ya kuwalinda watu wa jamii hiyo na MUNGU MKUU asiyeonekana.
Ila Allah na Yehova wote ni miungu lakini sio Yule Mungu Mkuu
Sawa mkuu kwa kuwagea waarabu Mungu wa asili kwamba ni sawa na kabila huchagui.Kumbukumbu la Torati 6:14
Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;
Ukitaka kujua majina(proper name/personal name) ya miungu ya mataifa kama Misri, Kanaani, Yordan, Moabu, Waajemi, Wamedi, warumi yote ipo Kwa Majina ninaweza kukutajia with Reference.
Na pia ukitaka kujua mungu wa waarabu nitakutajia achilia mbali huyo Yehova Mungu wa Wayahudi.
Ndio maana watu wote wenye maarifa, ufahamu, elimu na Ujuzi watashangaa wakisikia wakisema Allah akamuambia Musa au Daudi au Yesu ilhali Allah sio Mungu wa Wayahudi. Huo utakuwa ni uongo mkubwa ambao hautavumiliwa.
Au mtu aseme Torati, injili, Zaburi na maandiko yote ya kiyahudi ati yawe yametoka Kwa Allah, huo ni upotoshaji na wanaopotoshwa na watu wasioelimika au walioamua kupotoka.
Au Yehova amuagize Muhammad muarabu yaani huo utakuwa uongo mkubwa
Kuamini nako kuna sababu, sasa wewe mwenzetu unaamini kwa sababu zipi?
Labda nikuulize mkuu msomi wangu, wewe umesoma hizo dini zote mbili au tuseme una elimu ya Qur'an na Biblia?Wewe huwezi elewa Kwa sababu huna elimu ya Historia.
Ushaambiwa Yehova ni Allah ni miungu wawili tofauti kutoka jamii mbili tofauti wewe bado hauoni kina wizi umefanyika?
Ndio maana nikakushauri ni Bora ukajielimishe Kwanza mambo ya Historia kisha mambo ya Dini ili unapojadili ujadili Kama mtu mwenye Uelewa na sio kama mwanafunzi anayetafuta Uelewa
Sawa mkuu kwa kuwagea waarabu Mungu wa asili kwamba ni sawa na kabila huchagui.
Labda nikuulize mkuu msomi wangu, wewe umesoma hizo dini zote mbili au tuseme una elimu ya Qur'an na Biblia?