Wanaitwa hivyo kutokana uovu wao na si kuwapanda watu kichwani tu bali hutumika kwenye uchawi na hadi kuabudiwa, na ndio maana majini wabaya huitwa mashetani. Hapo ndio maana nikauliza wewe unaelewa vp kuhusu mashetani katika wingi au bado unaona anayefaa kuitwa shetani ni huyo huyo malaika aliyeasi tu?jamaa unachekesha haina mantiki swali lako hapa dunia hawa wanawapanda mpaka watu wanawehuka watu wanaita ''Mashetani " ila sio ni majini.
Hapo wametumia kama sifa ya shetani ila yule shetani mwenyewe dhambi zake sio za kawaida yule ni special kesi.Wanaitwa hivyo kutokana uovu wao na si kuwapanda watu kichwani tu bali hutumika kwenye uchawi na hadi kuabudiwa, na ndio maana majini wabaya huitwa mashetani. Hapo ndio maana nikauliza wewe unaelewa vp kuhusu mashetani katika wingi au bado unaona anayefaa kuitwa shetani ni huyo huyo malaika aliyeasi tu?
Ndio maana mwanzo kabisa nilikwambia kuwa biblia haijawaelezea hao majini na wakristo uelewa wao kuhusu majini hutumia vyanzo vya waislamu, wakristo wanazungumzia malaika waliyoasi wakati waislamu wanazungumzia majini kama viumbe vilivyoumbwa ambao ni tofauti na malaika.Tuwaulize nyinyi wenzetu ambao mnaundugu nao wa damu kabisa.
Sisi tunajua pia kwa kuona kuwa Majini wote ni viumbe waovu. Wakimpagawa mtu ni kumtesa tu na kumharibia mipango yake.
Sasa ninyi wenzetu mtuambie hao Majini wema mnafanyiana wema upi ?
Majini mema wanafanya wema upi? Maana wenzetu mpo karibu nao, mtuambie.
Hata huyo unayemwita shetani mwenyewe nae ameitwa hivyo kutokana tu na sifa la hilo neno la shetani.Hapo wametumia kama sifa ya shetani ila yule shetani mwenyewe dhambi zake sio za kawaida yule ni special kesi.
Unaweza kuwa sahihi kwa sababu majini na binadamu ndo viumbe vimetajwa kwa pamoja vikiwa na lengo moja la kuabdu.
kama binadamu anaweza kuambia una tabia za kishetani hata jini basi ni sawa
Ila hyo sifa ukifuatia kabisa japo kweye lugha unaweza kumpa yeyote ila kwa kiumbe amnacho hakijalaaliniwa sioni kama ni sawa maana kinaweza kutubu .Hata huyo unayemwita shetani mwenyewe nae ameitwa hivyo kutokana tu na sifa la hilo neno la shetani.
Majini kwa lugha nyingine ni pepo wachafu na wameongelea sana kwenye Biblia hasa katika Agano Jipya.Ndio maana mwanzo kabisa nilikwambia kuwa biblia haijawaelezea hao majini na wakristo uelewa wao kuhusu majini hutumia vyanzo vya waislamu, wakristo wanazungumzia malaika waliyoasi wakati waislamu wanazungumzia majini kama viumbe vilivyoumbwa ambao ni tofauti na malaika.
Kwahiyo point sio majini kuwa wazuri au wabaya bali point ni asili ya hao majini kwamba ni malaika au ni viumbe vilivyoumbwa ambavyo na Mungu ni tofauti na malaika na binaadamu?
Mkuu Robert,Kwema Wakuu!
Kutokana na mjadala fulani uliokuwa unaendelea katika Jukwaa la Intelligence nimeona nianzishe uzi huu kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia kupima katika mizania ya kimahakama/kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.
Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?
Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi, bali nipo kujadili nani mkweli kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama, majaji mtakuwa ninyi wasomaji.
Mahakamani siyo kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa sheria, hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.
Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema kwa vile mambo haya yanagusa imani za watu jambo hilo linaweza kuwa gumu.
Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa rejea kuu zaidi ya Quran, kwa sababu;
1. Biblia kwa sehemu kubwa haina maneno ya 'Hearsay' wakati Quran kwa 90% maneno yake ni 'Hearsay'. Kimahakama maneno ya 'hearsay' hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu. Hoja hii ndiyo hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.
Baada sasa ya wewe kutambua kuwa Qur'an ni maneno ya Allah yaliyoshushwa kwa Mtume Muhammad, unapaswa pia kutambua kuwa Muhammad ni Mtume wa mwisho aliyetumwa baada ya Mitume wengi waliopita kabla yake mfano wa Ibrahim, Ismail, Ishaqa, Yaakub, Zakaria, Yahya, Issa (Yesu), Mussa, Haarun, Daud, Suleiman (Amani ziwe juu yao).a) Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, Yona n.k.
Wakati msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo. Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita. Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.
Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, Mathayo na Yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu waliyoshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya. Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka kwa sababu yeye alisimuliwa.
Hata hivyo ulikuwa ni wakati ule ule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka. Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.
Hii ni katika dalili za wazi pia kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hakujua kusoma wala kuandika lakini alitoa habari zilizopita kabla yake. Na utambue kuwa sehemu ya habari hizo alizosimulia ni Mayahudi wasomi wa Taurat ya Mussa walitumia nafasi hiyo kumuuliza Mtume Muhammad baadhi ya mambo yaliyopita ambayo Mtume hakuwepo ilhali wao Mayahudi wanafahamu kupitia kitabu chao cha Taurat.2. Waandishi wa Biblia walikuwepo maeneo tajwa kwenye Biblia, lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika maeneo anayoyasimulia. Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na Waisrael ambapo hajawahi kufika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.
Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman halafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman, wakati Suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.
Jibu hilo hapo juu.Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia. Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.
3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.
Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo!😀😀
Nakusahihisha Robert,Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.
Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi kwasababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni kama vile kitabu cha Mzee wetu Mwinyi au Mzee wetu Mengi.
Muhammad hajashushiwa 'vitabu' bali ameshushiwa 'kitabu' nacho ni Qur'an. Ndani ya Qur'an hakuna kitabu cha Injili, Taurat wala Zabur bali kuna habari zote za Mitume wote waliotumwa kabla yake. Alichokifanya Muhammad hakimo kwenye Qur'an kwa sababu Qur'an si maneno ya Muhammad bali Muhammad ameishi kwa kuifuata na kuifundisha Qur'an kama muongozo kwa watu. Hilo litambue Robert.Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay), kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa ukweli na ikachukuliwa kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.
Robert,4. Biblia imeandikwa na Wayahudi kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu kwa lugha ya Kiarabu lakini inasimulia habari za wasiyo Waarabu, inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.
Ah! Taikun wa Fasihi umepatwa na nini?Yaani mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo. Hivi ninyi mtanisikiliza mimi Mpare ninayesimulia habari za kale za Wasukuma au mtasikiliza Wasukuma wenyewe?
Kuwa Myahudi na rafiki wa Yesu hakuashirii kuwa ndio ukweli wa anachosema. Kwani Yuda alikuwa nani kwa Yesu?Muhammad Muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo halafu yeye anakwambia alizaliwa kwenye mtende halafu kuna mtu Myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye hori la ng'ombe.
Rafiki wa Yesu hawezi kuwa na maarifa zaidi kumzidi Mwenyezi Mungu, neno la Mwenyezi Mungu ndilo sahihi kuliko neno la Yohana.Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni Myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza nani?
Nakusahihisha ndugu Robert,Haya Quran na hadithi za Kiyahudi kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji wa Daudi na mwanaye Suleiman, hajui Kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.
Huo ni upungufu uliomo katika kitabu chako unachokiamini. Pia hakuna Mtume aliyejiandikia hadith zake. Yesu alijiandikia hadith gani? Yesu alipewa Injili ikiwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu. Injili sio hadith za Yesu alizojiandikia, Iweje useme Suleiman na mwanawe wamejiandikia hadith? Kama kitabu chako ndio kimeandika hivyo basi huo ni upotevu na upungufu mkubwa.Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini, lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo majini. Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika vitabu vyake vilivyopo katika Biblia? Jibu utabaki nalo.
5. Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa Waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah, Mungu wa Waarabu wa kabila la Wakurdi wa zamani lakini cha ajabu huyo Allah, ati huyo Allah kuna sehemu anamuagiza kina Musa (Myahudi na dini yake Uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.
Jibu la hoja hii limejibiwa hapo juu.Hata hivi leo Mungu wa Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu wa waarabu hajabadilika ni yule yule Allah. Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa Muarabu.
Qur'an iko sawa, haijapuyanga kama usemavyo Robert.Wahusika kuanzia kwa Yakobo mpaka kwa Yesu ni Wayahudi na dini yao ni Uyahudi na Mungu wao ni Yahweh, lakini Quran imepuyanga katika eneo hilo.
Kama unavyidai wewe pamoja na wengine wengi kuwa Qur'an imenakili visa vya biblia, inawezekanaje Mtu (Muhammad) anakili visa wakati Muhammad hakujua kusoma wala kuandika?6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran, siyo ajabu Quran yenyewe ndiyo imenakili baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.
Qur'an chanzo chake sio Biblia Robert.Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndiyo baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovinakili kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya Kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile.
Qur'an haijaja kukueleza eti tawala za watu zilifuatana vipi. Qur'an ni muongozo kamili wa maisha ya mwanadamu.7. Mtiririko na visa na matukio ya Kihistoria.
Biblia ni kitabu ambacho kimeandikwa Kwa kufuata mtiririko wa visa na matukio unaoleweka. Kuanzia kisa cha Adamu mpaka Yusufu anachosimulia Musa, Kisha tawala za dunia kama Tawala la Nimrodi, kisha tawala la mafarao, kisha tawala la Waashuru na Wakaldayo, kisha wakafuata Waajemi na Wamedi, kisha wakafuata Wayunani/wagiriki, kisha wakafuata Warumi ndipo alipozaliwa Yesu.
Lakini Quran haina mtiririko wa visa na matukio, kumaanisha haiwezi kutumika hata shuleni Kama rejea za kihistoria kuhusu tawala, au mambo ya kuitawala au Kisiasa kwani Quran haijui wapi dunia imetoka ilipo na wapi inapoenda. Wakati Biblia inaeleza wapi Dunia ilipotoka na wapi ilipo na inapokwenda.
Qur'an hakuna ilichoacha katika kutoa muongozo wa maisha ya mwanadamu. Na nyingi katika hoja zenu zimejibiwa ndani ya Qur'an yenyewe.Quran inaweza kuulizwa swali, Yesu alizaliwa wakati WA utawala gani na wanani na ukashindwa kujibu?
Kimahakama Quran kama haijui baadhi ya taarifa muhimu kama Zama na Maeneo husika ya tukio lilipotukia haiwezi kutumika kama Rejea au ushahidi muhimu katika mambo ya Kidini.
Kwahiyo Taikun wewe kwa Mtazamo wako unaona alipozaliwa Yesu kwenye Mtende huo Mtende ni wa pale Tandale kwa Tumbo? Acha masihara kwenye mambo ya msingi Taikun.Kwa mfano; Issa kazaliwa kwenye mtende Kwa mujibu wa Quran lakini haielezi ni eneo gani au nchi gani Issa alizaliwa, hata Hapa Tanzania ipo mitende, hii ni tofauti na Biblia inataja na kuelezea visa katika mtiririko uliokamilika.
Kwani Yakobo alikuwepo wakati wa Yesu!? Habari za Yakobo Yesu alizitoa wapi? Kama Qur'an imeielezea Taurat na Injil ndani yeke itaacheje kumtaja Yakobo na watoto wake? Soma Surah ya Al Imraan Aya ya 84, Al Baqarah aya 136, An Nisaa aya ya 163 kisha malizia na Al Baqarah aya ya 140 uone sio watoto tu wa Yakobo bali mpaka wajukuu zake wametajwa humo.8. KUjitosheleza, kujitegemea na kutoa taarifa zote muhimu.
Biblia inajitosheleza na kujitegemea Biblia kuhusisha kitabu kingine. Msomaji yeyote wa Biblia akimaliza kuisoma hatahitaji rejea za kitabu kingine.
Mfano msomaji akisoma kisa cha Yakobo, atajua Yakobo alizaliwa wapi, ndugu yake ni Nani, Routes zake zote, wake zake, watoto wake na umri wake mpaka anakufa. Kwa nini aliitwa Yakobo, ikawaje akabadilishwa jina n.k
Lakini Quran haijitoshelezi haina hizo taarifa muhimu. Hivyo kuifanya Quran kuwa tegemezi Kwa vitabu vingine.
Qur'an ina nondo zote, zilizopita na zijazo. Hata zile zilizopita ambazo zimepotoshwa au kufichwa Qur'an imezibanisha. Na imepambanua haki na baatil. Na imekuja kusafisha yote yaliyopotoshwa ambayo Yesu aliyafundisha kisha baadaye yakapotoshwa kwa makusudi. Mojawapo kubwa na baya zaidi ni kumfanya Yesu kuwa ni Mungu wakati yeye ni Mtume tu na mitume wengi wamepita kabla yake.Quran ambacho ingefanya ni kutoa nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na siyo kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo. Mbona Injili haujarudia visa? Quran haiwezi kuchukuliwa kama rejea kuu kuzidi Biblia kwa sababu nilizozitaja hapo juu.
Utaikon wako ungejikita zaidi kudadavua pale ambapo Yesu mwenyewe anasema kwenye hiyo ambayo ninyi mnaiita Biblia kuwa yeye ametumwa tu, na aliyemtuma ni Mungu. Kisha mkamfanya tena yeye ndio Mungu muabudiwa badala ya kumuabudu yule ambaye amemtuma Yesu kama alivyomtuma Mussa na mitume wengineo.Majaji mjadili kwa hoja.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Sasa hayo unayosema ni mtazamo wako binafsi ambao umeujenga kwa fikra za neno shetani ni kama jina la huyo Ibilisi na sio kama sifa, na unalihusisha neno shetani na kutokutubu ili hali havihusiani.Ila hyo sifa ukifuatia kabisa japo kweye lugha unaweza kumpa yeyote ila kwa kiumbe amnacho hakijalaaliniwa sioni kama ni sawa maana kinaweza kutubu .
sifa ya shetani mbaya sana hata kumtamkia binadamu mwenzio kheri hata umuite "kafiri"
Bado haujaeleza pepo wachafu ndio nini? Qur'an inaeleza majini ni viumbe vilivyoumbwa na moto hivyo si katika malaika wala binaadamu, ila wakristo mnasema majini ni katika malaika waliyoasi hali ambayo inaleta utofauti mkubwa.Majini kwa lugha nyingine ni pepo wachafu na wameongelea sana kwenye Biblia hasa katika Agano Jipya.
Mathayo 10:1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Mathayo 12:22 Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.
Mathayo 17:18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
Marko 1:32 Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo.
Mathayo 10:8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Hao hapo hawana ushirika kabisa na Mwenyezi Mungu.
Wala Yesu hakuwa na msahaha nao kila walipompagawa mtu kwa ajiri ya kumtesa aliwatoa ili wasiendelee kumdhuru.
Wenzetu mnasema wapo kati yao wema.
Habari yenu inaenda kinyume kabisa na Mafundisho ya Yesu Kristo.
Je Mapepo sio viumbe wa Mungu ?
Je hawakuumbwa ili wamwabudu ?
Mbona Yesu hana uhusiano mwema nao ?
Yalikosea wapi ?
Kwanini hawana nafasi ya kutubu ?
Unaweza kuyajibu hayo maswali ?
Hapana hilo jina sio zuri kumuita mwenzio .Sasa hayo unayosema ni mtazamo wako binafsi ambao umeujenga kwa fikra za neno shetani ni kama jina la huyo Ibilisi na sio kama sifa, na unalihusisha neno shetani na kutokutubu ili hali havihusiani.
Hilo sio jina, Ibilisi ana jina lake kabisa. We mwenyewe umeeleza maana ya hilo neno shetani sasa ajabu hutaki litumike kwa kiumbe mwenye sifa hizo.Hapana hilo jina sio zuri kumuita mwenzio .
Haifai sio zuri kabisa kumpa binadamu mwenzio.Hilo sio jina, Ibilisi ana jina lake kabisa. We mwenyewe umeeleza maana ya hilo neno shetani sasa ajabu hutaki litumike kwa kiumbe mwenye sifa hizo.
Naona umeishiwa hoja.Haifai sio zuri kabisa kumpa binadamu mwenzio.
Hoja zipo uliza swali ila siwez kumuita mtu shetani ,mbwa hata jina la mnyama ni forbidden kwa imani yangu sijasema Uislamu ila imani yangu binafsi.N
Naona umeishiwa hoja.
Majini kwa lugha nyingine ni pepo wachafu na wameongelea sana kwenye Biblia hasa katika Agano Jipya.
Mathayo 10:1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Mathayo 12:22 Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.
Mathayo 17:18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
Marko 1:32 Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo.
Mathayo 10:8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Hao hapo hawana ushirika kabisa na Mwenyezi Mungu.
Wala Yesu hakuwa na msahaha nao kila walipompagawa mtu kwa ajiri ya kumtesa aliwatoa ili wasiendelee kumdhuru.
Wenzetu mnasema wapo kati yao wema.
Habari yenu inaenda kinyume kabisa na Mafundisho ya Yesu Kristo.
Je Mapepo sio viumbe wa Mungu ?
Je hawakuumbwa ili wamwabudu ?
Mbona Yesu hana uhusiano mwema nao ?
Yalikosea wapi ?
Kwanini hawana nafasi ya kutubu ?
Unaweza kuyajibu hayo maswali ?
Kwan binadamu akifanya mema tu anakua malaika ? Uwe unaelewa bas majin ni viumbe kama viumbe vingine. Allah anasema leng la kuwaumba binadam na majin ni waje wamuabudu. Kwaio binadam wapo wanaomuabud na wapo wanaomkufuru. Na majin pia wanaomuabud na wapo wanaomtii.Kwa mafunzo ya uislamu yanasema malaika hufanya mema tu hawamuasi Mungu, ndio nauliza kama majini wamegawanyika kwa makundi mawili wema na waovu je, hao majini wema wanakuwa kama malaika ambao hufanya mema tu?
Sawa kafiriIla hyo sifa ukifuatia kabisa japo kweye lugha unaweza kumpa yeyote ila kwa kiumbe amnacho hakijalaaliniwa sioni kama ni sawa maana kinaweza kutubu .
sifa ya shetani mbaya sana hata kumtamkia binadamu mwenzio kheri hata umuite "kafiri"
Mkuu wewe unaamini kabisa kuna majini?Kwan binadamu akifanya mema tu anakua malaika ? Uwe unaelewa bas majin ni viumbe kama viumbe vingine. Allah anasema leng la kuwaumba binadam na majin ni waje wamuabudu. Kwaio binadam wapo wanaomuabud na wapo wanaomkufuru. Na majin pia wanaomuabud na wapo wanaomtii.
Wote majin na binadam wanaomuabud kwa haki basi watalipwa na wanaomuasi watalipwa kwa mujib wa matendo yao.
Na Allah ni mjuzi zaidi.