Ndio maana mwanzo kabisa nilikwambia kuwa biblia haijawaelezea hao majini na wakristo uelewa wao kuhusu majini hutumia vyanzo vya waislamu, wakristo wanazungumzia malaika waliyoasi wakati waislamu wanazungumzia majini kama viumbe vilivyoumbwa ambao ni tofauti na malaika.
Kwahiyo point sio majini kuwa wazuri au wabaya bali point ni asili ya hao majini kwamba ni malaika au ni viumbe vilivyoumbwa ambavyo na Mungu ni tofauti na malaika na binaadamu?
Majini kwa lugha nyingine ni pepo wachafu na wameongelea sana kwenye Biblia hasa katika Agano Jipya.
Mathayo 10:1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Mathayo 12:22 Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.
Mathayo 17:18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
Marko 1:32 Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo.
Mathayo 10:8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Hao hapo hawana ushirika kabisa na Mwenyezi Mungu.
Wala Yesu hakuwa na msahaha nao kila walipompagawa mtu kwa ajiri ya kumtesa aliwatoa ili wasiendelee kumdhuru.
Wenzetu mnasema wapo kati yao wema.
Habari yenu inaenda kinyume kabisa na Mafundisho ya Yesu Kristo.
Je Mapepo sio viumbe wa Mungu ?
Je hawakuumbwa ili wamwabudu ?
Mbona Yesu hana uhusiano mwema nao ?
Yalikosea wapi ?
Kwanini hawana nafasi ya kutubu ?
Unaweza kuyajibu hayo maswali ?