inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 20,344
- 21,967
Wewe umerukwa akili,mwanzo ulisema mungu Hana muda wa kuandika, akiongea Musa akaandika, nimekupa andiko mungu kampa Musa torati(law) ambayo kaiandika mwenyewe mungu kwa kidole chake, unaanza kuleta ngonjera, kwanza Kiri mungu aliandika kwa kidole chake na anao huo muda, Kisha tuendelee na hoja zingine.Kwa hiyo hivyo vibao viwili ndio Torati?
Unajua hivyo vibao vilivunjwa na Musa mwenyewe?
Kwamba Yesu alizaliwa nje si ndio maana yake.Umeandika pumba tupu ila tambua kuwa Hauna hoja za kupinga Aya za Quran iwe kwa kutumia Bibilia, Mahakamani au kwa kutumia akili yako ya kibinaadamu
Mimi nakujibu pumba yako Moja tu
YESU AMEZALIWA WAPI?
Hakuna andiko lolote katika Bibilia lililotaja sehemu alipozaliwa Yesu Yani (Lebor ya Yesu)
Luka 2 (KJV)
6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,
7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Hili andiko halisemi kama Yesu amezaliwa katika hori la ngombo linasema amevikwa nguo akalazwa katika hori tena amelazwa hapo baada ya Mariam kukosa nafasi nyumba ya wageni inamaana wangepata nafasi nyumba ya wageni hapo katika hori la ngombo wasingefika
Yani kama hospital hapo katika hori ni warding sehemu ambayo wazazi wanaenda kupumzika na watoto wao baada ya kutoka Labor
Sasa je Lebor ya Yesu ili kuwa wapi ? Kwa mujibu wa Quran Lebor ya Yesu ni chini ya Shina la mtende
Quran 19:23.
Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
24.
Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!
25.
Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
Hamuna uwezo wa kuipinga Quran kwa hoja na ndio maana Allah aliwambia asiye itakata Quran na achukue kamba AJINYONGE
Wewe umerukwa akili,mwanzo ulisema mungu Hana muda wa kuandika,akiongea Musa akaandika,nimekupa andiko mungu kampa Musa torati(law) ambayo kaiandika mwenyewe mungu kwa kidole chake,unaanza kuleta ngonjera,kwanza Kiri mungu aliandika kwa kidole chake na anao huo muda,Kisha tuendelee na hoja zingine
Taurati ni kiebrania ikiwa na maana ya lawa,jibu swali langu,kutoka 31:18 mungu kaandika kwa kidole chake,hivyo anao muda wa kuandika na wewe na dhana zako ni potofu?Ndio nikakuuliza swali hivyo vibao viwili ndio Torati?
Urudia kosa lile ukisoma maelezo ya Yohana hakuna popote alipoonyesha ya kuwa amemuona Yesu, labda unionyesha.Kitabu cha Yohana, kimeandikwa na Mwanafunzi wa Yesu aitwaye Yohana.
Huyu ndio mwanafunzi WA mwisho wa Yesu kufa, kitabu kingine alichoandika ni kitabu cha Ufunuo,
Msikilize Yohana;
Ufunuo wa Yohana 1:9
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
Ufunuo wa Yohana 1:10
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
Ufunuo wa Yohana 1:11
ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Ufunuo wa Yohana 1:12
Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
Ufunuo wa Yohana 1:13
na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
Yupo mathayo;
Yupo Petro;
Msikilize Petro
1 Petro 3:18
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,
1 Petro 2:21
Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
1 Petro 2:22
Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.
1 Petro 2:23
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.
1 Petro 2:24
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
1 Petro 2:25
Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.
Huyo ni Petro mwanafunzi namba moja WA Yesu. Anashuhudia.
Hata jibu hoja za andiko alafu Kama unataka kuanzisha hoja mpya tutafanya hivyo baadaye.
Alafu ingekuwa vizuri hiyo hofu uliyonayo kuhusu Biblia ndio ingetakiwa maradufu kwenye Quran ambayo inasimulia habari za Wayahudi ilhali muandishi ni muarabu ambaye hajui waisrael hata mmoja anayemsimulia, hajawahi kufika Israel, hajakuwepo wakati hayo yanatokea hata Kwa ukaribu wa miaka 100 tuu.
Hizo ndio hoja, naona unataka kuanzisha mjadala mpya
Unachekesha!!!🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Hiyo inaitwa "Royal We" yaani respect and glorification na sii PLURAL au UWINGI.....
Majestically Allah anaposema "Tume.." au "We" ni respect and glorification of the CREATOR na wala siyo UWINGI....
Toka nijiunge JF sijawai kumtukana mtu lakini Leo wewe mwanangu utanisamehee wewe ni mpumbavu ,mjinga ,una akilli na umejaa sana na udini sasa unataka tujadili nini wakati wewe umeshaonyesha ni upande gani uliopo?Kwema Wakuu!
Kutokana na mjadala fulani uliokuwa unaendelea katika Jukwaa la Intelligence nimeona nianzishe uzi huu kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia kupima katika mizania ya kimahakama/kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.
Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?
Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi, bali nipo kujadili nani mkweli kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama, majaji mtakuwa ninyi wasomaji.
Mahakamani siyo kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa sheria, hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.
Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema kwa vile mambo haya yanagusa imani za watu jambo hilo linaweza kuwa gumu.
Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa rejea kuu zaidi ya Quran, kwa sababu;
1. Biblia kwa sehemu kubwa haina maneno ya 'Hearsay' wakati Quran kwa 90% maneno yake ni 'Hearsay'. Kimahakama maneno ya 'hearsay' hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu. Hoja hii ndiyo hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.
a) Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, Yona n.k.
Wakati msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo. Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita. Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.
Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, Mathayo na Yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu waliyoshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya. Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka kwa sababu yeye alisimuliwa.
Hata hivyo ulikuwa ni wakati ule ule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka. Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.
2. Waandishi wa Biblia walikuwepo maeneo tajwa kwenye Biblia, lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika maeneo anayoyasimulia. Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na Waisrael ambapo hajawahi kufika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.
Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman halafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman, wakati Suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.
Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia. Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.
3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.
Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo![emoji3][emoji3]
Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.
Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi kwasababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni kama vile kitabu cha Mzee wetu Mwinyi au Mzee wetu Mengi.
Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay), kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa ukweli na ikachukuliwa kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.
4. Biblia imeandikwa na Wayahudi kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu kwa lugha ya Kiarabu lakini inasimulia habari za wasiyo Waarabu, inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.
Yaani mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo. Hivi ninyi mtanisikiliza mimi Mpare ninayesimulia habari za kale za Wasukuma au mtasikiliza Wasukuma wenyewe?
Muhammad Muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo halafu yeye anakwambia alizaliwa kwenye mtende halafu kuna mtu Myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye hori la ng'ombe.
Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni Myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza nani?
Haya Quran na hadithi za Kiyahudi kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji wa Daudi na mwanaye Suleiman, hajui Kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.
Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini, lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo majini. Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika vitabu vyake vilivyopo katika Biblia? Jibu utabaki nalo.
5. Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa Waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah, Mungu wa Waarabu wa kabila la Wakurdi wa zamani lakini cha ajabu huyo Allah, ati huyo Allah kuna sehemu anamuagiza kina Musa (Myahudi na dini yake Uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.
Hata hivi leo Mungu wa Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu wa waarabu hajabadilika ni yule yule Allah. Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa Muarabu.
Wahusika kuanzia kwa Yakobo mpaka kwa Yesu ni Wayahudi na dini yao ni Uyahudi na Mungu wao ni Yahweh, lakini Quran imepuyanga katika eneo hilo.
6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran, siyo ajabu Quran yenyewe ndiyo imenakili baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.
Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndiyo baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovinakili kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya Kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile.
Quran ambacho ingefanya ni kutoa nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na siyo kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo. Mbona Injili haujarudia visa? Quran haiwezi kuchukuliwa kama rejea kuu kuzidi Biblia kwa sababu nilizozitaja hapo juu.
Majaji mjadili kwa hoja.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Kwanza si mitume yote ni wayahudi, mitume wanatoka race mbalimbali na wameingiliana sana.Ila tunaweza kuishtaki Kenya Kwa kutumia Majina ya watu wetu au kuiba Stori zetu na kuzifanya ni zao.
Waarabu wameiba Stori na Majina ya Wayahudi alafu wanajitia wao ndio wawe Reference wakati dunia nzima inajua walifanya plagiarism
Usijiaibishe mkuu lugha zote kongwe "we" inaweza isimaanishe wingi bali utukufuUnachekesha!!!
Kwa hiyo hata mimi leo nikivumbua kitu kwenye intro nikasema nilikigundua peke yangu kisha kwenye uzinduzi nikasema ”tulikaa tukagundua,tukaunda” still utanielewa?kwa line hizo nitakuwa na akili kweli?
Au kwa sababu itakuwa mimi sikuandikwa au kusimuliwa kwenye hadithi basi siyo kweli!!!hizi ni blah blah blahs aliyeandika hiko kitabu kuna hesabu zilimchanganya akaficha ficha kwamba ni heshima ya kifalme.
Wanataka tu kudhihaki watu, mtu akiishiwa hoja anatafuta dhihakaSasa hizo sendos mbona tuna vaa hadi tusio waislamu lakini when it comes to religion debate kubazi zinakuwa kama ni utambulisho wa waislamu pekee?
Hakuna balaa lolote chizi huyu anafahamikaBalaa zito unalileta
Kwa hiyo kwaajili yako mungu wa waarabu/Allah ili aonyeshe utukufu na nguvu zake ndio maana anatumia wingi katika kujieleza? 😀😀
Naomba usijibu swali hili maana najua huna maarifa nalo,
Nilikuuliza swali kwenye Uzi wa Jana, kabla Muhammad hajawa Mtume alikuwa anaabudu mungu yupi?
Hukunijibu,
Wakati bi. Khadija anaenda Kwa padri walaga unafikiri hapakuwa na vitabu vinavyosimulia habari za Kina
Hakuna says yoyote kwenye QUR'AN smbayo MUHAMMAD Rehema na amani ziwe juu yake anasimulia au kuzungumza kama YEYE...Kwa hiyo kwaajili yako mungu wa waarabu/Allah ili aonyeshe utukufu na nguvu zake ndio maana anatumia wingi katika kujieleza? 😀😀
Naomba usijibu swali hili maana najua huna maarifa nalo,
Nilikuuliza swali kwenye Uzi wa Jana, kabla Muhammad hajawa Mtume alikuwa anaabudu mungu yupi?
Hukunijibu,
Wakati bi. Khadija anaenda Kwa padri walaga unafikiri hapakuwa na vitabu vinavyosimulia habari za Kina Musa, Yesu, Yusuf, Daudi na Suleiman?
Maana ni kosa kubwa kudhani Muhammad ndiye mtu wa Kwanza kuzungumza visa vya Wayahudi ilhali vilikuwepo na yeye ni mtu wa Mbali mno kinasaba na kisimulizi Kwa habari za visa alivyosimulia.
Hujajibu hoja hata Moja, yaani Uzi huu bado hajatokea anayejibu hoja zilizotolewa, kila mmoja akija anakuja na mambo yake mapya ambayo hayajaletwa kwenye Baraza.
Safi kabisa, kwanza naomba uthibitishe ya kuwa Waraqah alikuwa Padri ?! Kisha uniambie mambo ya Upadri yalianza lini ?Mtume Muhammad anafunuliwa mambo ambayo Padri walaga jirani yake anayo?
Hapa sijaelewa hoja yako Iko wapi ? Sababu Mtume alitumwa kwa Makufari wa Kiarabu na watu baadhi kama vile kina Waraqah ambao walikuwa na ujuzi wa vitabu vya kale.Yaani ni Sawa atokee mtu sasa hivi ajifanye anafunuliwa habari za Quran ilhali Waislam mpo na mnajua habari zote za Quran.
Mtu huyo mtamchukuliaje?
Safi kabisa, ufunuo ni nini ? Waraqah una uhakika alikuwa anayajua yote ya vitabu vya kale ? Jibu si sahihi sababu hawakuwa na matini ya vitabu hivyo vya Bali ni kumbukumbu za hizo habari tu.Yaani Muhammad anafunuliwa Stori za kina Musa, sijui Ibrahimu, sijui Yusufu ilhali tayari wapo Wakristo kina Padri Walaga wanazo alafu mnaita ufunuo😀😀.
Naendelea kusubiri majibu majibu ya maswali yangu.Yaani majaji/wasomaji ambao hawana ushabiki wataelewa na kuamua wenyewe Kwa hoja unazozitoa.
Wapi katika Qur'aan au Hadithi Mtume amesema nabii Suleyman alikuwa anafuga Majini ? Wakristo kwanini mnakuwa wajinga kiasi hiki hata kufanya utafiti mnashindwa ?Muhammad anafunuliwa ati Suleiman alikuwa anafuga majini.
Hajui hata Utamaduni wa Suleiman ukoje, hajui Mungu WA Suleiman/Wayahudi aitwaye Yahwe anakataza kutumia maruhani/majini,
Muhammad hajui kuwa Suleiman hajawahi kumjua Allah mungu wa waarabu.
Shida hujengi hoja na huna hoja Bali unalalama. Jaribu kutulia ujenge hoja kama navyo Jenga Mimi.Hivi kweli bado unaona Quran iko makini?
Ni akheri wakati ina-copy wahusika wakiyahudi inge-copy na Mungu WA kiyahudi ingekuwa angalau kuna Ukweli.
Yani kweny arguments za dini unaleta clip ya watu wanaotukana matusi kuzungumzia dini hapo kuna shida. Wakristo hawawezi shiriki mjadala kama huo maan Bible inakataza.
Hapana sijakusudia kudhihaki dini yoyote, niliamini kuna point tunaweza kujifunza. Kama umeielewa vinginevyo NAOMBA RADHI. Muungwana akiombwa radhi HUSAMEHEYani kweny arguments za dini unaleta clip ya watu wanaotukana matusi kuzungumzia dini hapo kuna shida. Wakristo hawawezi shiriki mjadala kama huo maan Bible inakataza.
Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
kaka ni chaguo lako tu UIPENDE DUNIA UIACHE AKHERA AU UIPENDE AKHERA UIACHE DUNIAUtata ni mwingi sana.
Mungu wa kweli kama yupo na anapatikana kwenye vitabu hivi vya dini kwanini aliruhusu kitabu kingine kije ambacho ni cha uongo mfano kama bible ni ya kweli kwanini aliruhusu Quran ije ambayo inapotosha au kama Quran ni kweli Mungu kwa nini alishindwa kuiteketeza bible ambayo ni uongo!?
Licha ya hayo Mtu pekee anayeeeza kukwambia Mungu wangu ni wa kweli ni mwanadamu ambaye naye anasoma kitabu kinacho jieleza kuwa kimetokana na Mungu wa kweli iwe bible au Quran nje ya vitabu hivyo sina hakika kama kunasehemu unaweza kuthibitisha kuwa vitabu hivo ni kweli.
Ajabu nyingine pia katika vitabu vyote huwa kuna inaibuka makundi(watu) ambayo yana tafasri kwa hivyo vitabu kwa mtazamo tofauti na ule wa wengine na makundi hayo yakipata wafuasi yanakuwa madhehebu iwe kwenye ukristo au uislam ni maajabu.
Nacho fikiri kwa sasa huenda watu walionyuma ya hizi dini ambao ndio waanzilishi wa hizi dini wakirudi leo hii pengine kunavitu vingi wangebadilisha au ķuvipinga kwan vitakuwa tofauti na mitazamo yao au mitazamo yao itakuwa imebadilika.
Pia wafuasi wengi wa hizi dini hawajui hata misingi ya imani zao naona dini ni silaha hatari zaidi kuwahi kutokea.
Nime fuatilia kwanini afrika tuko tulivo hasa Tanzania sababu ni dini waislam wanawakaririsha Quran watoto wakristi wanawakaririsha biblia watoto na mwisho wa siku watoto waanamini sehemu pekee yenye umuhim ni mbinguni huko kuna raha zote na dunia ni sehemu sawa tu kwa chochote kitakachotokea.
Kwa wenzetu wanasayansi wakubwa wote tunaowasoma waliofanya makubwa ni watu waliokuwa wanashinda maabara au pengine kusoma kwao ndio ilikuwa tumaini lao la kwanza.
Naahangaa sana watu ambao wanaona kuwekeza katika sayansi ni kama kumkana Mungu wakati huo huo wanatumia technologia zilizo tengenezwa kwa kiasi kikubwa na wanasansi ambao wengi wao hawaamini katika hizi dini.