Umeandika pumba tupu ila tambua kuwa Hauna hoja za kupinga Aya za Quran iwe kwa kutumia Bibilia, Mahakamani au kwa kutumia akili yako ya kibinaadamu
Mimi nakujibu pumba yako Moja tu
YESU AMEZALIWA WAPI?
Hakuna andiko lolote katika Bibilia lililotaja sehemu alipozaliwa Yesu Yani (Lebor ya Yesu)
Luka 2 (KJV)
6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,
7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Hili andiko halisemi kama Yesu amezaliwa katika hori la ngombo linasema amevikwa nguo akalazwa katika hori tena amelazwa hapo baada ya Mariam kukosa nafasi nyumba ya wageni inamaana wangepata nafasi nyumba ya wageni hapo katika hori la ngombo wasingefika
Yani kama hospital hapo katika hori ni warding sehemu ambayo wazazi wanaenda kupumzika na watoto wao baada ya kutoka Labor
Sasa je Lebor ya Yesu ili kuwa wapi ? Kwa mujibu wa Quran Lebor ya Yesu ni chini ya Shina la mtende
Quran 19:23.
Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
24.
Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!
25.
Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
Hamuna uwezo wa kuipinga Quran kwa hoja na ndio maana Allah aliwambia asiye itakata Quran na achukue kamba AJINYONGE
Kwamba Yesu alizaliwa nje si ndio maana yake.
Biblia ipo wazi kuwa Yesu kazaliwa kwenye Zizi la ng'ombe na imetoa sababu ya Kwa nini Jambo Hilo limetokea.
Lakini Quran haijatoa sababu kwanini huyo Issa anayenasibishwa na Yesu alizaliwa chini ya mtende
Haya ukasome hapa,
Biblia ni kitabu kikubwa Kama jina lake lilivyo.
Usiseme kitu hakipo kabla hujauliza,
Haya soma;
Mathayo 2:1
Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
Mathayo 2:2
Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
Mathayo 2:3
Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
Mathayo 2:5
Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, <br>Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; <br>Kwa kuwa kwako atatoka mtawala <br>Atakayewachunga watu wangu Israeli.
Mathayo 2:7
Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.
Mathayo 2:8
Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.
Mathayo 2:9
Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.
Mathayo 2:11
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.
Umejua ni wapi Yesu amezaliwa?
Na alizaliwa katika utawala upi? Na Mfalme alikuwa Nani?
Msimuliaji hapo ni mathayo mwanafunzi WA Yesu MWENYEWE.
Haya Quran anayesimulia ni Nani? Anamahusiano na Yesu Kwa namna ipi?
Je aliwahi kuonana na Yesu au kuonana na watu walioishi na Yesu?
Je aliwahi kufika nchi na eneo alilozaliwa Yesu ili ahoji watu waeneo Hilo?
Jibu ni hakuna mahusiano yoyote baina ya Muhammad na Yesu.
Hivyo Stori yoyote atakayoitoa haiwezi kutiliwa maanani.