Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Wewe unamuamini Yesu gani?

Maana katika Bibilia Kuna Yesu wawili

Yesu wa kwanza ni yule nabii aliyetumwa na Mungu kwa ajili ya wana wa Israel

Yohana 17:3 (KJV)
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Na Yesu wa pili ni yele Yesu wa Paulo ambayo aliwadanganya watu kuwa Yesu ni Mungu ili yeye ajipe utume

Tito 2:13 (KJV)
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

Huyo Yesu mtume wa Mungu ni wa kweli ila huyo Yesu wa Paulo ni garasa ambalo halijawahi kuwepo duniani
 
Hivi unajua kwamba watu wengi waliyozungumziwa kwenye biblia hawatambuliki uhalisia wa kuwahi kuwepo kwao duniani katika historia ya dunia?

Unalijua hilo?

Kama yupi hatambuliki?
Kwa Sisi tuliosoma elimu za juu tunajua wanatambulika kihistoria,

Advance ulisomea mchepuo upi?
 
Kisa cha Yesu ndio kimewekwa baada ya Yesu kuondoka.
Lakini vitabu vingine hata Yesu alivitumia katika mahubiri take, na alivisoma kwenye madhahabu.
Nadhani hujanielewa, nazungumzia hicho kitabu biblia hakikuwepo na vitabu vyengine vimewekwa mara vyengine havijawekwa na hakuna sababu ya msingi katika kufanya huo uchaguzi wa kuweka na kutokuweka hivyo vitabu yani mvurugo tu.
 
Nadhani hujanielewa, nazungumzia hicho kitabu biblia hakikuwepo na vitabu vyengine vimewekwa mara vyengine havijawekwa na hakuna sababu ya msingi katika kufanya huo uchaguzi wa kuweka na kutokuweka hivyo vitabu yani mvurugo tu.

Hata Quran haikuwepo Muhammad alipokuwa hai.
Kwa upande wa Yesu, vitabu vilivyokuwepo ni Torati, Zaburi na vitabu na vyuo vya manabii waliomtangulia.

Injili yeye ndiye aliyeileta hivyo hakuisoma/hapakuwa na kitabu cha injili
 
Usikimbilie tu kumtaja huyo Joshua na kudhani ndio atakuwa jibu kwa utata wote, bado kuna vitu vimezungumziwa ambapo hata huyo Joshua wakati huo hakuwepo na ajabu vitu hivyo vimezungumziwa katika hali ambapo hivyo vitu vimeshapita.
Itabidi utaje waandishi tena huyo Joshua hatoshi.
 

Joshua ndiye aliyekabishiwa majukumu na Musa na ndiye kiongozi aliyefuata baada ya Musa, na ndiye aliyewafikisha Waisrael Canaan,
Na ndiye muisrael pekee akiwa na Kalebu waliotoka Misri mpaka Kanaani wengine wote walikufa njiani.
Na katika HAO yeye ndiye aliyeandika habari zilizoendelea baada ya Musa kufa, iweje yeye asitoshe kuulizwa?

Unataka aulizwe Nani?
Wakati yeye ndio muda mwingi alikuwa na Musa
 
Hata Quran haikuwepo Muhammad alipokuwa hai.
Kwa upande wa Yesu, vitabu vilivyokuwepo ni Torati, Zaburi na vitabu na vyuo vya manabii waliomtangulia.

Injili yeye ndiye aliyeileta hivyo hakuisoma/hapakuwa na kitabu cha injili
Mimi nakuelekeza sitokwambia haujaenda shule, ukisema Qur'an haikuwepo wakati wa Muhammad sasa sijui hizo tuhuma Muhammad kukopy kwenye Biblia zimejengewa kwenye msingi gani kama sio kwenye Qur'an? Wakati wa Muhammad Qur'an haikuwa imekusanywa pamoja na kuandikwa sehemu moja na kama ilivyo sasa.
 

Nakupa mfano;
Yesu wakati anatoa hotuba zake yeye alitoa nukuu na kutoa Credit sehemu alipozichukulia hizo nukuu.
Mfano anasema wazi kuwa, Kama ilivyaoandikwa na Nabii Isaya.........
Hiyo ni kwamba anatambua kuwa maneno hayo sio Yake bali ya mtu mwingine.
Au akitoa kisa kama katoa kisa cha Waisrael basi atasema Kama ilivyoandikwa kwenye Torati ya Musa .................

Lakini Kwa Muhammad na wenzake wao wamefanya wizi wa kazi, visa na wahusika tena WA taifa jingine bila kutoa Credit alafu wakafanya Forgeries za kutosha. Hiyo ni moja ya hoja nilizowasilisha hapo juu.

Nikasema maneno mengi ya Quran ni Hearsay tofauti ni Biblia ambayo 75% maandiko yake ni matukio halisi 15% ni unabii, alafu 10% ndio hearsay kama za kitabu cha Mwanzo
 
Kitabu pekee Cha Mungu ambacho kipo hapa duniani kwa Sasa na hakijatiwa mikono na watu ni Quran pekee na nahisi ndio maana ambao hamjawahi kusoma vitabu original vya Mungu mnaishangaa Quran vitabu vilivyobaki vyote vimechakachuliwa

Taurati haipo lipo kumbukumbu la taurati na maneno kibao yamechakachuliwa

Yeremia 8:8 (KJV)
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.


Na Injili original pia haipo ila Kuna makapi ya Injili

Luka 1:1-2 (KJV)
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,

Lazima nyinyi wagalatia muishangae Quran kwa sababu mnasoma vitabu vya Mungu vilivyochakachuliwa tena walichakachua makusudi ili wakupoyezeni watu kama wewe ROBERT HERIEL mwenye mtindio wa ubongo
 
Mbona hujajibu point hata moja
 
Mbona hujajibu point hata moja
Quran ni kitabu original tokea alivyofunuliwa mtume Muhammad hakuna aliyeongeza Wala kupunguza hata nukta Moja

Sasa na nyinyi leteni taurati original na Injili original ili tuangalie je ni kweli Aya za hivi vitabu vinatofautoana sio mnaleta Injili iliyoandikwa na waganga wa kienyeji akina Luka alafu ndio mlinganishe na Quran Hilo haliwezekani

Weka hapa
Taurati original na Injili original
 
Unaelewa kweli mada iliyopo mezani

Wahusika wa vitabu vya biblia walifikaje kwenye koran? Embu elezea

Kwa Nini Muhammad hakuja na character wa uarabuni?
 
Weka hapa
Taurati original na Injili original
Tulivyo navyo ndio original
Kama wewe unasema sio original kazi inarudi kwako kuleta unayosema original tulinganishe na tuliyonayo
 
Tulivyo navyo ndio original
Kama wewe unasema sio original kazi inarudi kwako kuleta unayosema original tulinganishe na tuliyonayo
Siku zote kafiri ni kafiri tu na kazi yake kupinga maandiko mmeanza kupinga mandiko ya Quran na Sasa mnapingana na Bibilia mbachodai ndio kitabu chenu

Bibilia lenyeww linasema limechakachuliwa alafu wewe unapinga tukufae wewe au tufuate yanavyosema maandiko ya Bibilia

Yeremia 8:8 (KJV)
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.


Luka 1:1-2 (KJV)
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,

Injili mliyonayo ni imechakachuliwa na Taurati mliyonayo pia imechakachuliwa

Lete hapa vitabu original ili tukuonyeshe kuwa hivyo vitabu vyote vilifundisha uislam
 
Kwa hiyo walichakachua, halafu walipofika kwenye Yeremia 8:8 (uliyoinukuu na unayoiamini) ndio wakaacha hapo kupachakachua?

Yaani walichakachua Biblia yote, halafu walipofika hapo kwenye hiyo Yeremia 8:8 hapo wakapaacha?

Au na hapo walipachakachua?
 
Wewe ndio unadai imechakachuliwa, halafu tena unasema mimi nilete original?

Hivi unajielwea au ndio yaleyale ya kwenye mihadhara?

Wewe unayedai imechakachuliwa unapaswa kuthibitisha hoja yako kwa kuleta original.
 
Injili mliyonayo ni imechakachuliwa na Taurati mliyonayo pia imechakachuliwa

Lete hapa vitabu original ili tukuonyeshe kuwa hivyo vitabu vyote vilifundisha uislam
Wewe unaedai imechakachuliwa bila shaka unayo original

Ni kazi ndogo Sana weka original tulinganishe na hii unayodai tumechakachua

Kama huna original na unadai iliyopo imechakachuliwa lazima utakuwa ni psychopath
 
Aliyeandika mambo ambayo hata Joshua alikuwa hayupo wakati huo ni nani? Huo uandishi uliendelea hata baada ya Joshua kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…