Mnakurupukaga Sana
Biblia inatoa maana na asili Hadi kupatikana neno ISRAEL
Nimeomba Quran itueleze neno ISRAEL maana yake Nini , unanijia juu, Quran imeiba neno ISRAEL kwenye BIBLIA , Sasa ninaomba inisaidie ISRAEL ni Nini
Utunzi
Kwa mujibu wa wasomi wa Biblia, hata utunzi wa vitabu vya Agano la Kale na Injili zenyewe una mashaka.
Torati Vitabu vitano vya kwanza katika Biblia (Vitabu vya Musa) kimapokeo vinahusishwa na Mtume Musa, hata hivyo, kuna mistari mingi ndani ya vitabu hivi inayoashiria kuwa Mtume Musa hana uwezekano wa kuandika kila kitu kilichomo katika vitabu hivyo.
Kwa mfano, Kumbukumbu la Torati 34:5-8 inasema: "Basi Musa, mtumishi wa BWANA, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la BWANA. Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peroi; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo.
Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu zake hazikupunguka. Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha."
Ni wazi kuwa mtu mwingine ameandika mistari hii inayohusu kifo cha Musa.
Baadhi ya wasomi wa Kikristo wamezifafanua hitilafu hizi kwa kupendekeza kuwa Musa ndiye aliyeandika vitabu vyake, lakini mitume ya baadaye pamoja na waandishi waliofunuliwa, wameweka nyongeza iliyotajwa hapo mbele.
Kwa hiyo, kwa mujibu wa wasomi hao, matini,kwa ukamilifu wake, inabakia kuwa ni Maandiko ya ufunuo wa Mungu.
Hata hivyo, ufafanuzi huu hauwezi kukubalika katika uchunguzi makini, kwa sababu mtindo na fasihi ya wahusika wa mistari iliyotomewa ni sawa sawa na ule wa matini iliyobakia.
Katika karne ya kumi na tisa, wasomi wa Biblia wa Kikristo wameanza kujadili maana ya “kujirudiarudia mara mbili mbili” kulikotokea katika Torati.
Hivi ni visa vilivyotokea mara mbili mbili, na kila mara kinakuwa na maelezo tofauti.
Miongoni mwa visa hivyo ni visa viwili vya agano la Mungu na Ibrahimu, linalohusu Mungu kubadilisha Jina la Yakobo na kuwa Israeli pia na kisa cha Musa kupata maji kutoka katika mwamba.
Watetezi wanaotetea utunzi wa Musa wamesema kuwa “kujirudiarudia mara mbili mbili” hakukuwa na kupingana, bali ni kuleta faida.
Dhamiara zao zilikuwa ni kutufundisha undani, na maana ndogo juu ya Torati.
Hata hivyo, madai haya yalifagiwa haraka haraka na wasomi walio na moyo wa uadilifu, walioona kuwa, sio tu baadhi ya vifungu vilikuwa vinapingana kwa uwazi kabisa, lakini pia wakati kule “kujirudiarudia mara mbili mbili” kulipotenganishwa na kuwa vifungu viwili, kila kifungu kwa uthabiti kilitumia jina la Mungu lilotofauti.
Siku zote mtu anaweza kumchukulia Mungu kuwa ni Yahweh au Jehovah, andiko hili liliitwa “J”. Na lingine, siku zote, linamchukulia Mungu kuwa ni Elohim, na liliitwa “E”.
Kulikuwa na sifa za kifasihi zilizopatwa kuwa ni moja kwa waraka mmoja au mwingine