Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Waislamu mmeangukia pua
Tukiangalia dini za uongo na imani mbalimbali za upotovu duniani, na moyo wa kuzipenda unaowafanya wafuasi wake waziunge mkono imani hizo, inaonesha ushahidi madhubuti kuwa watu hao hawawezi kuugundua ukweli kwa sababu ya upofu wa misimamo yao juu ya imani zao.
Ufuasi wao king`ang`anizi, kwa kawaida hauegemei ufahamu wa kiakili juu ya mafundisho, bali unategemea utamaduni wenye nguvu na vishawishi vya kihisia.
Kwa kuwa walilelewa katika familia au jamii maalum, wao wanashikamana madhubuti na imani ya jamii hizo, wakiamini kuwa, wanauunga mkono ukweli.
Katika gazeti la kimataifa la, Newsweek, December 18, 1995, , lililobeba makala yenye kichwa 'Oo Bwana, Nani Aliyeandika Dua hii?'
kikosi cha wanatiolojia kutoka katika dhehebu kuu la kiporestanti, pamoja na Wasomi muhimu wa Biblia wa Kikatoliki nchini Marekani, baada ya ukaguzi wa kina wa miswada ya mwanzo kabisa ya Agano Jipya, wamehitimisha kuwa maneno pekee ya "Dua ya Bwana" ambayo yanaweza kunasibishwa barabara na Yesu Kristo ni "baba".
Na hilo, ni kwa mujibu wa wasomi hao wa kanisa, maneno yote yaliyokuja baada ya ibara ya kwanza, "Baba yetu", ambayo ni dua muhimu sana ya Kikristo, yaliongezwa karne nyingi na waandishi wa kanisa walionukuu miswada ya mwanzoni ya Injili.
Shirika la U.S News & World Report, linanukuu zaidi kuwa, kikundi cha wasomi kilisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maneno yaliyoandikwa katika Injili kumhusu Yesu huenda ni ya kubuniwa
Miongoni mwa hayo likiwemo neno la Ekaristi ya Yesu katika Karamu ya Mwisho ("Chukua, kula. Huu ni mwili wangu…") na kila neno aliloambiwa kuwa amelitamka toka msalabani.