Kwema Wakuu!
Kutokana na mjadala Fulani uliokuwa unaendelea katika jukwaa la intelligence nimeona nianzishe Uzi huu Kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia Kupima katika mizania ya kimahakama/ kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.
Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?
Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi Bali nipo kujadili Nani mkweli Kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama.
Majaji mtakuwa ninyi wasomaji;
Mahakamani sio kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa Sheria, Hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani Kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.
Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema Kwa vile mambo haya yanagusa Imani za watu Jambo hilo linaweza kuwa gumu.
Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa Rejea kuu zaidi ya Quran. Kwa sababu;
1. Biblia Kwa sehemu kubwa haina maneno ya Hearsay wakati Quran Kwa 90% maneno yake ni Hearsay.
Kimahakama maneno ya hearsay hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa Kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu.
Hoja hii ndio hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.
i. Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, yona n.k.
Wakati Msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo.
Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita.
Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.
Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, mathayo na yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu walioshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya
Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka Kwa sababu yeye alisimuliwa.
Hata hivyo ulikuwa ni wakati uleule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka.
Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.
2. Waandishi WA Biblia walikuwepo Maeneo tajwa kwenye Biblia.
Lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika Maeneo anayoyasimulia.
Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na waisrael ambapo hajawahi kupafika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.
Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman alafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman.
Wakati suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.
Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea Kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia.
Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.
3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa Kwa manabii tofauti tofauti Kwa nyakati tofauti tofauti wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshishiwa Muhammad.
Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu, kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha yakobo na yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu.
Na visa vyote hakuwepo[emoji3][emoji3].
Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha yona kaandika Yoña mwenyewe, Kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu(wanafunzi waliomshuhudia)
Kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.
Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi Kwa sababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni Kama vile kitabu cha Mzee wetu mwinyi au Mzee wetu MENGI.
Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay) kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa Fact na ikachukuliwa Kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.
4. Biblia imeandikwa na Wayahudi Kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu Kwa lugha ya kiarabu lakini inasimulia habari za wasiowaarabu. Inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.
Yaani Mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo.
Hivi ninyi mtanisikiliza Mimi mpare ninayesimulia habari za kale za wasukuma au mtasikiliza wasukuma wenyewe?
Muhammad muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo alafu yeye anakuambia alizaliwa kwenye mtende alafu kuna mtu myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye Hori la ng'ombe. Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza Nani?
Haya Quran na hadithi za kiyahudi Kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga Majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji WA Daudi na mwanaye Suleiman, hajui kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.
Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini.
Lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu Kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo Majini.
Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika Vitabu vyake vilivyopo katika Biblia?
Jibu utabaki nalo.
5 Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah mungu wa waarabu wa kabila la wakurdi wa zamani lakini chaajabu huyo Allah ati huyo Allah kunasehemu anamuagiza kina Musa (myahudi na Dini yake uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.
Hata hivi leo Mungu WA Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu WA waarabu hajabadilika ni yuleyule Allah.
Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa muarabu
Wahusika kuanzia Kwa Yakobo mpaka Kwa Yesu ni Wayahudi na Dini Yao ni uyahudi na Mungu wao ni Yahweh.
Lakini Quran imepuyanga katika eneo Hilo.
6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo Kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran sio ajabu Quran yenyewe ndio ime-copy baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.
Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndio Baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovi-copy kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile. Quran ambacho ingefanya ni Kutoa Nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na sio kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo.
Mbona Injili haujarudia visa,
Quran haiwezi kuchukuliwa Kama rejea kuu kuzidi Biblia Kwa sababu nilizozitaja hapo juu.
Majaji mjadili Kwa hoja.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam