QURAN 10: 37-44
37. "Na haiwezekani Qur'ani hii kuwa imetungwa na haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Lakini hii inathibitisha (vitabu) vilivyotangulia; na ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
38. Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni na nyie japo sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli(kwamba Muhammad kaizua hii Quran).
39. Bali wameyakanusha wasio yaelewa elimu yake kabla hayajawajia maelezo yake. Kadhalika walio kabla yao walikanusha vile vile. Basi angalia jinsi ulivyo kuwa mwisho wa madhaalimu hao.
40. Na miongoni mwao wapo wanao iamini, na miongoni mwao wapo wasio iamini. Na Mola wako Mlezi anawajua vyema mafisadi.
41. Na wakikukanusha wewe, sema: Mimi nina matendo yangu, na nyinyi mna matendo yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa niyatendayo, wala mimi sina jukumu kwa myatendayo.
42. Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza. Je, wewe unaweza kuwafanya viziwi wasikie ijapo kuwa hawafahamu?
43. Na wapo miongoni mwao wanao kutazama. Je, wewe utawaongoa vipofu ingawa hawaoni?
44. Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote; lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao."