Uthibitishe kutoka popote unapo weza wewe Kisha ujibu maswali haya :
Habari za Yesu kusulubiwa na kufa na kufufuka, zimeandikwa kwenye kitabu gani ? Kisha muandishi wa kitabu hicho alimuona Yesu au aliwaona wanafunzi wa Yesu ? Yeye hizo habari amezipata wapi ?
Nitajie watu hao walio kuwepo na Yesu japo watu Kisha utuambie waliandika kitabu gani ?
Kingine Mtume hakumuona Yesu yeye alikuwa anafunuliwa hizo habari na yule aliye mtuma Yesu na wengine. Hii si hoja kijana.
Kwanza kabla hatujafika huko unapo taka, nionyeshe nani alikuwepo katika eneno la tukio na ututhibitishie huyo aliyekuwepo kwenye tukio aliandika wapi hizo habari na mpaka zinawafikia nyinyi zimetoka wapi ?
Nataka niwafundishe namna habari zinavyochukuliwa na kuhakikiwa.
Yaani Wakristo laiti kama m gekuwa mnahakiki habari kama tunavyozihakiki sisi Waislamu hakuna hata neno Moja lingesalia katika Biblia isipokuwa yale ambayo yanaenda sawa na Qur'aan.
Kitabu cha Yohana, kimeandikwa na Mwanafunzi wa Yesu aitwaye Yohana.
Huyu ndio mwanafunzi WA mwisho wa Yesu kufa, kitabu kingine alichoandika ni kitabu cha Ufunuo,
Msikilize Yohana;
Ufunuo wa Yohana 1:9
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
Ufunuo wa Yohana 1:10
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
Ufunuo wa Yohana 1:11
ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Ufunuo wa Yohana 1:12
Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
Ufunuo wa Yohana 1:13
na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
Yupo mathayo;
Yupo Petro;
Msikilize Petro
1 Petro 3:18
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,
1 Petro 2:21
Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
1 Petro 2:22
Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.
1 Petro 2:23
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.
1 Petro 2:24
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
1 Petro 2:25
Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.
Huyo ni Petro mwanafunzi namba moja WA Yesu. Anashuhudia.
Hata jibu hoja za andiko alafu Kama unataka kuanzisha hoja mpya tutafanya hivyo baadaye.
Alafu ingekuwa vizuri hiyo hofu uliyonayo kuhusu Biblia ndio ingetakiwa maradufu kwenye Quran ambayo inasimulia habari za Wayahudi ilhali muandishi ni muarabu ambaye hajui waisrael hata mmoja anayemsimulia, hajawahi kufika Israel, hajakuwepo wakati hayo yanatokea hata Kwa ukaribu wa miaka 100 tuu.
Hizo ndio hoja, naona unataka kuanzisha mjadala mpya