Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Kwema Wakuu!

Kutokana na mjadala fulani uliokuwa unaendelea katika Jukwaa la Intelligence nimeona nianzishe uzi huu kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia kupima katika mizania ya kimahakama/kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.

Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?

Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi, bali nipo kujadili nani mkweli kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama, majaji mtakuwa ninyi wasomaji.

Mahakamani siyo kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa sheria, hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.

Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema kwa vile mambo haya yanagusa imani za watu jambo hilo linaweza kuwa gumu.

Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa rejea kuu zaidi ya Quran, kwa sababu;

1. Biblia kwa sehemu kubwa haina maneno ya 'Hearsay' wakati Quran kwa 90% maneno yake ni 'Hearsay'. Kimahakama maneno ya 'hearsay' hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu. Hoja hii ndiyo hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.

a) Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, Yona n.k.

Wakati msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo. Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita. Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.

Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, Mathayo na Yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu waliyoshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya. Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka kwa sababu yeye alisimuliwa.

Hata hivyo ulikuwa ni wakati ule ule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka. Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.

2. Waandishi wa Biblia walikuwepo maeneo tajwa kwenye Biblia, lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika maeneo anayoyasimulia. Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na Waisrael ambapo hajawahi kufika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.

Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman halafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman, wakati Suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.

Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia. Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.

3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.

Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo!😀😀

Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.

Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi kwasababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni kama vile kitabu cha Mzee wetu Mwinyi au Mzee wetu Mengi.

Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay), kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa ukweli na ikachukuliwa kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.

4. Biblia imeandikwa na Wayahudi kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu kwa lugha ya Kiarabu lakini inasimulia habari za wasiyo Waarabu, inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.

Yaani mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo. Hivi ninyi mtanisikiliza mimi Mpare ninayesimulia habari za kale za Wasukuma au mtasikiliza Wasukuma wenyewe?

Muhammad Muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo halafu yeye anakwambia alizaliwa kwenye mtende halafu kuna mtu Myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye hori la ng'ombe.

Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni Myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza nani?

Haya Quran na hadithi za Kiyahudi kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji wa Daudi na mwanaye Suleiman, hajui Kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.

Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini, lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo majini. Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika vitabu vyake vilivyopo katika Biblia? Jibu utabaki nalo.

5. Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa Waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah, Mungu wa Waarabu wa kabila la Wakurdi wa zamani lakini cha ajabu huyo Allah, ati huyo Allah kuna sehemu anamuagiza kina Musa (Myahudi na dini yake Uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.

Hata hivi leo Mungu wa Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu wa waarabu hajabadilika ni yule yule Allah. Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa Muarabu.

Wahusika kuanzia kwa Yakobo mpaka kwa Yesu ni Wayahudi na dini yao ni Uyahudi na Mungu wao ni Yahweh, lakini Quran imepuyanga katika eneo hilo.

6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran, siyo ajabu Quran yenyewe ndiyo imenakili baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.

Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndiyo baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovinakili kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya Kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile.

Quran ambacho ingefanya ni kutoa nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na siyo kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo. Mbona Injili haujarudia visa? Quran haiwezi kuchukuliwa kama rejea kuu kuzidi Biblia kwa sababu nilizozitaja hapo juu.

Majaji mjadili kwa hoja.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Kwanza hujui lolote kuhusu Uislamu Sasa kukuelimisha ni kumpigia mbuzi gitaa.

Mosi hizo heresay ukisoma OT nani aliyekuwa ana mrekodi Yahweh ad verbaun neno kwa neno kama secretary wake.

Nani alimuona Mungu akijifanya John Cena na kutandikwa vibaya na Yahudi mmoja.

Wenye Tourati ambayo ndio msingi wa biblia yaani wayahudi sio tuu hawamtambui/kumkubali Yesu kuwa lolote zaidi ya mtoto wa haramu wa askari wa Kirumi mpaka leo watatoa ushahidi gani kwenye kesi yako ya kihabithi?
 
Naheshimu mawazo yako mengi na kuyaunga mkono ila kwa hili umepotoka[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16].

Ni vizuri kufahamu vitu vingi ila sio kujua kila kitu[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35].

Uyahudi ndio ukristo?

Iweje Mungu wa Wayahudi ndio unamclarify kuwa ndio Mungu wa Wana wa kristo?

Unafahamu Wakurdi na Wakuraishi ni jamii mbili tofauti?

Unaijua historia ya Allih na Illah kabla ya uislamu?

Unatambua Yale mawe pale Maka watu walikwenda hija kabla ya uislamu kuwepo?

Waswahili wanasema kila zama na kitabu chake?
Mtume alikuja na Quraan tu?
Hivyo vitabu vingine vina mitume yake.
Tofauti ya Mussa
Injili ya yesu

Unafahamu tofauti ya nini kipo kwenye Quraan na tofauti ya hadithi zake?

Moja kati ya maandiko yako ulikiri wazi wazi Yesu hawezi kuwa Mungu[emoji16][emoji16][emoji16]
Hawa yehova wametoka wapi?

Vitabu vyote viwili vina hearsay za kutosha na logical inconsistent.
Alipanda juu ya mlima wanafunzi wake aliwaacha chini ikawaje ikawaje wakasema wale ni Nabii Eliya na Musa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] hiyo Ina tofauti gani na Imani ya Mizimu.

Alivyofariki kila mtu aliona wazi wazi, kwa nini alivyofufuka ni watu wachache waliona Tena wanafunzi wake[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] huu ushahidi kuwa alifufuka na kupaa umetokea wapi?
Kwa nini asiende sokoni?
Sasa ana tofauti gani na Babu yangu aliyefariki miaka mingi lakini nikiwa kwenye shida unamuona au unamuota na tatizo lako limekwisha? Nayo ni hearsay tu.

N.B Siamini kwenye hayo mambo ya dini
 
Acha kudanganya watu hata akili ya kuhoji huna..hayo mavazi yalivaliwa huko middle east kwasababu ya hali ya hewa ya joto na jangwa..hivyo nguo kama kanzu zilikuwa zinavaliwa ili kupunguza kuweka mwili cool..sasa wewe mmatumbi wa dubai kavae kipendo chako njombe kama utatoboa na vazi lako la imani.

Mavazi ni tamaduni husika na wala sio imani...jitambue wewe usikaririshwe kila kitu ukabeba kama kilivyo.

#MaendeleoHayanaChama
Unajiona mjanja kweli, hivi unafikiri huku kuna Baridi kuliko middle East? Au sababu umesikia kuna jangwa na Joto basi unafikiri kuna joto all time?

Jangwa ni Eneo lina joto kali na baridi kali, kuna Nchi kibao za Kiarabu middle east zina hadi snow

Pengine umesoma shule ya Msingi Atlas mountain ipo North Africa, hii ni Hali ilivyo Tunisia snow kila sehemu, Jangwa na lina Barafu
images (9).jpg

Hizi ni picha za Jerusalem alipoishi Yesu
F220126YS131-640x400.jpg

Hapa Masjid Al Aqsa Jerusalem ikiwa na snow
F2220127NRF53-640x400.jpg

Sasa huko Kuna baridi hadi snow utafananisha na Njombe?

Na Kama umesoma vizuri comment yangu watu walikuwa wanavaa mavazi marefu ila Yesu hakutaka kuvaa mavazi marefu kujitofautisha nao.
 
Attachments

  • images (9).jpg
    images (9).jpg
    34.3 KB · Views: 5
Kwa hiyo wewe unaamini na inakuingia akilini kwamba baada ya alah kuona watu/viumbe aliowaumba mwenyewe wanamtungia ”WINGI" ambao yeye hana akaona awarudie kwa maandishi yakiwa bado na kile kile alochozushiwa nacho?...”WINGI”
Wanamtungiaje "Wingi" wakati hiyo na matumizi yake ni sehemu ya kawaida ya Lugha na Allah ndie kazileta hizi Lugha. Na Lugha; ule uzuri wake, utamu wake na ufasaha wake ni katika Ajabu za Uumbaji wake Allah.
Well,mie kiarabu sikifahamu
Nimefurahi kusoma hili. Hii ni hatua nzuri katika kuelekea kujifunza. Allah akuongoze.
ila wewe uniambie hapa ktk lugha ya kiarabu hakuna msamiati ”MIMI"?,kwanini azidi kuweka mazingira magumu kutambulika asiweke mazingira rahisi hata aliyeambiwa yupo "WENGI" ajue ni uwongo yupo "MMOJA"?
"MIMI" ipo katika Lugha ya Kiarabu na Allah ameitumia sana. Na akajizungumzia mwenyewe kuwa yuko mmoja tu Pekee
asiye na mshirika.

Na hiyo "SISI" aliyoitumia ni "SISI" ya kujitukuza sababu Yeye ni Mkuu aliye juu. Hivyo ametumia "SISI" kujitukuza. Sababu katika Kiarabu "SISI" huweza kutumika kwa mmoja kujitukuza, ukiachana na "SISI" ya wingi. Ndio maana wenyewe walioelewa Lugha haikuwasumbua. Ni katika ufasaha wa Kiarabu;

74_11.gif

11.Niache peke yangu na niliye muumba; 11

74_12.gif

12.Na nikamjaalia awe na mali mengi, 12

74_13.gif

13. Na wana wanao onekana, 13

74_14.gif

14.Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa. 14

74_15.gif

15.Kisha anatumai nimzidishie! 15

74_16.gif

16.Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu! 16

74_17.gif

17.Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana. 17

(Qur'an 74: 11-17)

51_56.gif

56. Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.56
(Qur'an 51: 56)

1.Surat Al-Ikhlas

Imeshuka MakkaIna aya 4

1_0.gif

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

112_1.gif

1. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. 1

112_2.gif

2. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. 2

112_3.gif

3. Hakuzaa wala hakuzaliwa 3

112_4.gif

4. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. 4
(Qur'an 112:1-4)

Allah Yeye ni Mmoja tu. Hiyo kutumia "SISI" ya kujitukuza ni katika ufasaha wa Lugha ya Kiarabu. Ndio maana Waarabu wenyewe kwa sababu wanaijua Lugha wala halikuwasumbua hilo. Ukifahamu hili halitakuchanganya.

Allah Mwenyewe amewaambia Waja wake kuwa Yeye ni Mmoja tu.

20_14.gif

14. Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.
(Qur'an 20:14)
Pale juu kwenye bold,kawaida yenu kum-provoke mpinzani wenu,sitalitilia maanani sana hilo.
Ukweli ni kwamba wewe hujui na unatakuwa kujifunza. Jifunze.

Allah akuongoze.
 
Bado hunishawishi!!!

Mawazo ya Kimungu hayawezi kujificha kwenye uchochoro wa lugha kama hivi na kwanini ajitengenezee mazingira tata kila wakati,kwamba angesema ”nikamuumba,nilimuumba” hadhi yake ingeshuka?kama kweli Mungu ndiye alishusha mistari hii huyo Mungu mimi nina mashaka nae,kwanza kwanini aendelee kutengeneza sintofahamu kwa viumbe wake baada ya sintofahamu aliyoitengeneza mwanzo kuonekana imewapoteza?

Kwa mujibu wa uislam hauutambui UTATU MTAKATIFU ambao wakristo wanaamini ni MUNGU MMOJA KTK NAFSI TATU (kwa upande mmoja tunaweza kusema ni maneno ya Mungu kabla watu hawajakengeuka na kujitungia uwongo wao dhidi yake)yumkini huoni kama kweli allah angekuwa na maono sahihi na ulimwengu ya kurekebisha hayo maneno baada ya kuona yaliyotokea hapo juu angeiweka clearly mistari ktk kitabu chake kinachoaminika ni cha kweli na cha mwisho kwa kuondoa haya mambo ya wingi ili isitokee tena sisi leo kuulizana hapa?

Nikisema mwandishi wa kuruan alijifungia mahali aka-copy baadhi ya mistari ktk Bible ili atengeneze kitabu chake kisha aka-limit uhuru wa kuhoji kwa kutoa conclusion kwamba atakaehoji aambiwe ni mambo ya lugha tu nitakuwa napotosha?hizo lugha zenyewe ni man made watu walikaa wakatengeneza maana wanazojua wao wakazitumia ni kwa vipi Mungu ang'ang'anizane nazo?
Tatizo lako Mkuu unajua kiswahili tu, hapo ndio tatizo linapoanzia, ukijifundisha lugha mbalimbali ushamba kama huu unatoka. Ukitaka kila kitu ukilete kiswahili na ku assume dunia inazunguka around kiswahili tutabiashana hadi kesho.

Wakati nafundishwa kifaransa nilikuwa na mawazo kama yako kila kitu kina jinsia mpaka visu, vikombe, sahani nk, maneno yote ni Feminine ama Masculine, ukileta hii concept kwenye kiswahili haimake sense, hatuna jinsia kwenye kisu sisi.

Hizi lugha kongwe zina maneno kibao ambayo kwetu kiswahili hayapo, moja wapo ni Hilo, Royal We haipo kiarabu tu lugha nyingi ipo na ni concept ya kawaida sana, ila kwenye kiswahili haipo hapo ndo unapoanza kuchanganyikiwa.

Bible kuna vifungu kibao sio kimoja wala viwili vinamuelezea mungu kama wingi, nimekupa link ya wikipedia kuna mifano kibao ya Royal we.
 
MaashaAllah. Umemuelezea kwa ufupi na kwa namna inayoeleweka. Huenda akaelewa kwa idhini ya Allah. Allah akulipe kheri.

Na Allah anajua zaidi.

Mimi namuomba Allah amuongoze Saint Anno II na wenzie.
 
MaashaAllah. Umemuelezea kwa ufupi na kwa namna inayoeleweka. Huenda akaelewa kwa idhini ya Allah. Allah akulipe kheri.

Na Allah anajua zaidi.

Mimi namuomba Allah amuongoze Saint Anno II
Mfano mwingine namuongezea.
Nina kiduka changu cha spare za pikipiki nauza mwenyewe ila kwenyebango naandika [TUNAUZA SPARE ZA PIKI PIKI KWA JUMLA NA REJA REAJA]
hapo wamiliki wa hilo duka n wangapi?
 
wao wafuge majini tu[emoji23][emoji23].
Mwamposa mbona naona raia wanapona au ni maigizo? na kama nimaigizo mbona watu ni wengi
Mwamposa Ni tapeli ,hakuna anayepona pale

Usibabaishwe na wengi , maana Sifa ya manabii wa uongo Ni kukomba wengi, kumbuka wengi hawajui maandiko wanataka Mteremko /kitonga

Mwamposa anafanya biashara kwa mgongo wa dini

Mt 7:13-27 SUV

Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao.
 
Ndiyo maana nikasema hivi Wakristo Elimu ya uhakiki wa Habari hamna. Mmeshawahi kuthibitisha ya kuwa hizi habari ni za kweli ?

Unajua hiki hata wewe unaweza kukaa ukakisimulia. Mimi sipo kwenye matini, Mimi nipo katika kuhakiki kiini Cha habari zilipo Toka.

Hii ni stori kama stori nyingine, kumbuka hapa tunaongelea habari za ufunuo

Daniel I alikuwa nani na hizi habari nani amewanukulia mpaka zimewafikia nyinyi ?
Kuhusu Danieli ,nabii zake zimetimia kwa kustajaabisha

Hata Isack Newton alichunguza kitabu Cha Daniel ,na alikichambua kuliko hata Calculas

Kupitia kitabu Cha Daniel hata Alexander mkuu alipokisoma akasema hakika huu Unabii unanihusu Mimi

Kitabu Cha Daniel pekee huwez kufananisha hata robo na Quran nzima

Acha kabisa mzee ,

Ndio kitabu kinaonesha Historia nzima ya Ulimwengu Hadi MWISHO

Ndio kitabu kilitabiri Hadi Hizi G7, UMOJA WA MATAIFA, 666,

Ndio kitabu kilitabiri kwa usahihi Hadi mwaka Aliokufa na kusulubiwa Yesu

(Ukitaka ushahidi wa kutosha na kihistoria nakupa)

Ndio kitabu kina kitu kinaitwa DANIEL FEAST , ambayo Daniel alifunga Siku 10 akila Vegetables na maji ,Nyuso zikawa nzuri kuliko waliokula Haram Kule babeli

(Ingia Google andika DANIEL FEAST utapewa ratiba ilivyo halafu jaribu)

Mzee baba,Biblia Ni tamu Sana, hapo nakueleza Kuhusu Daniel book tu kidogo, sijagusia vitabu Kama Isaya ,Yeremia , Ezekiel Kuna madini hatari Sana humo

Unajua GOGU NA MAGOGU?

Unafahamu Unabii wa Ninawi ambao aliuzungumzia Nabii Nahumu ,ambao umedumu mpaka leo?

Acha kabisa , Nimeisoma Quran Sana maana nilikuwa muislamu mzuri tu, Uislamu una loophole kubwa Sana, Kabla ya Muhammad hakuna ushahidi wa ki archeolojia au kimaandishi kuliwahi kuwepo dini inaitwa uislamu au jengo linaitwa msikiti , Siku nilipouacha uislamu niliuacha mbele ya masheikh niliwauliza hili swali ,wakaleta bla blaa eti uislamu Ni unyenyekevu ,hivo manabii walikuwa wanyenyekevu hivo uislamu ulikuwepo toka adamu[emoji1787][emoji1787]

Niliishia kucheka tu
images.jpg
images%20(2).jpg
images%20(1).jpg
images.jpg
 
ROBERT HEREL

Sasa kama hili la kuthibitisha tu sehemu alipo zaliwa Yesu (LEBOR YA YESU) Quran imeshinda vipi hizi hoja zako zilizobakia si ndio za kitoto zaidi

Quran 19:23.
Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!

24.
Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!

25.
Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.

26.
Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu.

Luka 2 (KJV)
6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,
7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

Hili andiko halisemi kama Yesu amezaliwa katika hori la ngombo linasema amevikwa nguo akalazwa katika hori tena amelazwa hapo baada ya Mariam kukosa nafasi nyumba ya wageni inamaana wangepata nafasi nyumba ya wageni hapo katika hori la ngombo wasingefika

kama yupo mkristo yoyote analo andiko linalosema Mariam amemzaa Yesu ndani ya hori la ng'ombe alitoe tulione
 
Tuambie wewe Yesu Kristo alizaliwa wapi na lini ?
Wewe unayemjua Yesu vizuri sana.

Tupe na ushahidi wako wa kimaandishi.
 
Huyu jamaa bora awe anachambua mambo yanayohusu wanawake kwenye dini mweupe kabisa hana ushahidi na hafanyii utafiti kile anachokizungumza , hata mkiristo mwenzake Championship kuna siku alimkosoa jamaa na kudai hata Bible hajua anatafsiri maandiko kiujanja ujanja.

Hili ndio tatizo la mtu kujifanya mjuzi kila kitu na kuiamini sana akili yako kinyume na uhalisia ,kuna uzi wake wa kudai "Putin ni Nabii au Mtume wa zama hizi ametumwa na Mungu " yaani ugoro mtupu hajui hata vigezo vya Mtume na Nabii.
Mimi huwa nasema ukweli siku zote, nilimkosoa kwenye ile mada ya talaka kwa wakristo maana niliona anaandika mambo yasiyokuwa sahihi.

Kwenye mada hii ROBERT HERIEL amejenga hoja vizuri nadhani waislam mjipange na kuzijibu badala ya kutukana na kubisha.
 
Ungekua na akili ungetambua hakuna zaidi ya kufuata mila na tamaduni za waarabu.

Wewe ni mtumwa wa mila na tamaduni za waarabu hakuna zaidi ya hapo.

#MaendeleoHayanaChama
Nikueleweshe kitu kimoja mila na tamaduni za kiarabu zilipingana sana na uislam yani uislam aliokuwa anaufundisha Muhammed ulilenga kuziangamiza mila na taratibu za waarabu na ndio maana hata wao walimpiga vita ndo ikawa sababu yakutaka kumuua na akatokomea Madina kwaiyo sio sisi tu tunauona mgeni hata hao waraabu wenyew ulikua mgeni kwao

Na hiyo ni kwa manabii wote walionekana kuharibu tamaduni

Ukifatilia vizuri historia yani kiundani utagundua uislam ulitangulia kuingia Africa ndo ukaenda madina na kiukweli sisi watu weusi hatukuwa na tamaduni zenye nguvu yani misingi yetu ilikua mibovu unavyoona viongozi wetu wakiyafanya zama hizi hata zamani ilikua ivo ivyo yani walikua wachumia matumbo na makabila yalikua mengi hatukuwa na muunganiko imara so tamaduni za kigeni ilikua ni rahisi kutuingia ilikua ukiamua kuwa chawa wa mzungu au chawa wa muarabu ni wewe tu nikumsifia tu ili we uishi poa kama ilivyo sahizi kwa viongozi wetu

Swala utumwa sisi ni kama tumeumbiwa mila na tamaduni zetu zisingetufaa na chochote God mwenyew anatujua ndo maana hakuleta nabii pande zetu angechezea tu unabii[emoji16]
 
Mimi huwa nasema ukweli siku zote, nilimkosoa kwenye ile mada ya talaka kwa wakristo maana niliona anaandika mambo yasiyokuwa sahihi.

Kwenye mada hii ROBERT HERIEL amejenga hoja vizuri nadhani waislam mjipange na kuzijibu badala ya kutukana na kubisha.
Tuanze na wewe thibitisha vita vilivyotokea huko mbinguni ,hii stori ipo kwenye bible.
 
Tuambie wewe Yesu Kristo alizaliwa wapi na lini ?
Wewe unayemjua Yesu vizuri sana.

Tupe na ushahidi wako wa kimaandishi.
Ushahidi gani unaoutaka zaidi ya huu Yesu amezaliwa chini ya Shina la mtende

Tena Quran imetuambia Hadi maneno aliyokuwa anasema Mariam wakati yupo Lebor

Quran 19:23.
Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
 
Ushahidi gani unaoutaka zaidi ya huu Yesu amezaliwa chini ya Shina la mtende

Tena Quran imetuambia Hadi maneno aliyokuwa anasema Mariam wakati yupo Lebor

Quran 19:23.
Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
Yesu unamsoma kwenye vyanzo vya Waarabu [emoji848]
Kwahiyo ukiambiwa ufanye utafiti wa maisha ya Yesu unaenda Uarabuni kufanya utafiti wako.

Kwani hujui ndugu zake walipo ?
Au huyo Yesu wako ndugu zake ni Waarabu ?
Na unajiita msomi. Hapo watakaofadhiri utafiti wako ni Al-qaida na Al-Shababu na ISIS tu
 
Kuhusu Danieli ,nabii zake zimetimia kwa kustajaabisha

Hata Isack Newton alichunguza kitabu Cha Daniel ,na alikichambua kuliko hata Calculas

Kupitia kitabu Cha Daniel hata Alexander mkuu alipokisoma akasema hakika huu Unabii unanihusu Mimi

Kitabu Cha Daniel pekee huwez kufananisha hata robo na Quran nzima

Acha kabisa mzee ,

Ndio kitabu kinaonesha Historia nzima ya Ulimwengu Hadi MWISHO

Ndio kitabu kilitabiri Hadi Hizi G7, UMOJA WA MATAIFA, 666,

Ndio kitabu kilitabiri kwa usahihi Hadi mwaka Aliokufa na kusulubiwa Yesu

(Ukitaka ushahidi wa kutosha na kihistoria nakupa)

Ndio kitabu kina kitu kinaitwa DANIEL FEAST , ambayo Daniel alifunga Siku 10 akila Vegetables na maji ,Nyuso zikawa nzuri kuliko waliokula Haram Kule babeli

(Ingia Google andika DANIEL FEAST utapewa ratiba ilivyo halafu jaribu)

Mzee baba,Biblia Ni tamu Sana, hapo nakueleza Kuhusu Daniel book tu kidogo, sijagusia vitabu Kama Isaya ,Yeremia , Ezekiel Kuna madini hatari Sana humo

Unajua GOGU NA MAGOGU?

Unafahamu Unabii wa Ninawi ambao aliuzungumzia Nabii Nahumu ,ambao umedumu mpaka leo?

Acha kabisa , Nimeisoma Quran Sana maana nilikuwa muislamu mzuri tu, Uislamu una loophole kubwa Sana, Kabla ya Muhammad hakuna ushahidi wa ki archeolojia au kimaandishi kuliwahi kuwepo dini inaitwa uislamu au jengo linaitwa msikiti , Siku nilipouacha uislamu niliuacha mbele ya masheikh niliwauliza hili swali ,wakaleta bla blaa eti uislamu Ni unyenyekevu ,hivo manabii walikuwa wanyenyekevu hivo uislamu ulikuwepo toka adamu[emoji1787][emoji1787]

Niliishia kucheka tuView attachment 2404567View attachment 2404570View attachment 2404568View attachment 2404569
Icho kiburi chako hakikusaidia kijana
Unajisifu kuuacha Uislamu?

Pole sana aiseee ni pumzi tu iyo inayokupa kiburi we mwanadamu

Yni mkishasoma na hivi vimawazo uchwara vya binadamu wenzako ety waanza kumkashifu Mungu

Pole sana kijana

Uislamu ni dini ya haki ww ata ukikimbia Uislamu utabaki na utaendelea
 
Yesu unamsoma kwenye vyanzo vya Waarabu [emoji848]
Kwahiyo ukiambiwa ufanye utafiti wa maisha ya Yesu unaenda Uarabuni kufanya utafiti wako.

Kwani hujui ndugu zake walipo ?
Au huyo Yesu wako ndugu zake ni Waarabu ?
Sasa nyie mbona mnawaamini wazungu na yesu hakuwa mzungu
Makanisa yote wameanzisha wazungu
Roman
Lutheran
Protestant

Mimi nawashangaa sana nyie wakristo wakati hao wayahudi wenyewe hawaukubali ukristo na hawamkubali yesu hhhhhhhhhhh poleni sanaaaaa
 
Back
Top Bottom