Luka 2:7
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Mtoto amevikwa nguo akalazwa katika hori sio kuzaliwa
Na Mariam amefika hapo baada ya kukosa nafasi nyumba ya wageni
Vipi kama angepata chumba katika nyumba ya wageni?
Mimi sifuati matamanio ya akili yako nafuata andiko linasema nini
Toa andiko linalosema Lebor ya Yesu ilikuwa sehemu gani ili Quran iliyosema Lebor ya Yesu ilikuwa chini ya Shina la mtende ionekane imedanganya
Hilo andiko hamna Umebaki unajiuma uma tu Bibilia imekuwa bubu kutaja Lebor ya Yesu ilikuwa wapi
Sio wewe tu hakuna kafiri yoyote katika Dunia hii anayeweza kuthibitisha kuwa Aya za Quran zimesema uongo
Wakili WA Quran naona unatangatanga, hujui hata unachokieleza!
Haya eleze kwa mujibu wa Quran sababu ipi ilimfanya Mariam azaliwe kwenye Mtende kama ilivyoeleza.
Alafu Mimi Wakili WA Biblia nakuwekea sababu za Yesu kuzaliwa Kwenye Hori la ng'ombe.
Soma;
Luka 2:4
Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;
Luka 2:5
ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.
Luka 2:6
Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,
Luka 2:7
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Biblia inajieleza wazi hapo,
Sio kwamba Mariam na Yusufu walifika Bethlehem alafu siku huyohuyo uchungu ukampata Mariam, isipokuwa Walikuwa katika kukaa huko Bethlehem, yaani wakukaa zaidi ya siku moja.
Usitake kuniambia Mariam na Yusufu hawakujua kuwa siku za kujifungua mtoto zimefika, huo utakuwa ni uongo.
Ndio maana eneo walilolipata ambalo ni kwenye Zizi la ng'ombe walikuwa wameliandaa Kwa dharura yoyote endapo ungejitokeza Mariam akajifungua.
Hata Yesu alizaliwa usiku, na Nyota ndio iliyowaongoza Mamajusi(wanajimu na wachungaji wa Kondoo waliokuwa porini) kufika usiku huohuo mahali alipozaliwa Yesu.
Embu tuambie Quran inatoa sababu ipi ya Yesu kuzaliwa Kwenye mtende?
Wakati Mariam anajifungua Yusufu alikuwa wapi?
Maana Quran inaeleza kuwa Mariam alikuwa mwenyewe.