Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Rudi post number moja soma ,alafu pangua hoja moja baada ya nyingine
Usinipangie kitu cha kuandika. Simu ni yangu, bando ni langu na muda pia ni wangu.
Naandika nikitakacho mimi sio utakacho wewe.
Una uhuru wa kufurahia au kutofurahia nilichoandika lakini huna uhuru wa kunipangia nini cha kuandika.
 
Usinipangie kitu cha kuandika. Simu ni yangu, bando ni langu na muda pia ni wangu.
Naandika nikitakacho mimi sio utakacho wewe.
Una uhuru wa kufurahia au kutofurahia nilichoandika lakini huna uhuru wa kunipangia nini cha kuandika.
Umesha panic baada ya kukosa majibu 😂😂
 
Ndiyo unayotumia kanisani kwenu ?
Wewe una ukichaa , umepewa uhuru hautaki , nimekupa moja utumie hautaki tena , Mimi kanisani natumia nyingi , nimekwambia tumia uliyonayo napo hutaki

Ni kwamba unakwepa maswali
 
Wewe una ukichaa , umepewa uhuru hautaki , nimekupa moja utumie hautaki tena , Mimi kanisani natumia nyingi , nimekwambia tumia uliyonayo napo hutaki

Ni kwamba unakwepa maswali
Mbona unaanza kurusha vichwa , ?
Kanisa lako ni lipi?
 
Ona sasa 😂😂😂 la biblia tena hukitaki , tumia biblia Kati 1000 ulizonazo chagua moja uje ujibu , niliyokuwekea umekataa
Ndiyo kanisa lako hilo linalotumia biblia ya BHN pamoja na biblia nyingi?
 
Ndiyo kanisa lako hilo linalotumia biblia ya BHN pamoja na biblia nyingi?
Ndio natumia biblia nyingi , sasa kwa sababu wewe unazo 1000 chagua moja au tumia zote ujibu huu uzi
 
Ndio natumia biblia nyingi , sasa kwa sababu wewe unazo 1000 chagua moja au tumia zote ujibu huu uzi
Kanisa lako linalotumia biblia ya BHN pamoja Na biblia nyingi ni kanisa gani hilo ?
 
Kanisa lako linalotumia biblia ya BHN pamoja Na biblia nyingi ni kanisa gani hilo ?
Natumia biblia nyingi na wewe pia izo nyingi umesema unazo , tumia jibu maswali , sio unauliza maswali tena ya kabisa na nimekupa uhuru utumie biblia unayotaka
 
Natumia biblia nyingi na wewe pia izo nyingi umesema unazo , tumia jibu maswali , sio unauliza maswali tena ya kabisa na nimekupa uhuru utumie biblia unayotaka
Ndilo kanisa lako hilo?
 
Hivi semeni KWELI waislamu.
Muwe honest.

Kama Mahakama ya Kimataifa ita waamuru mukaoneshe hapo ulipo kuwa Mti wa Mtende ambapo mnasema Yesu Kristo ndipo alipo zaliwa.

Kuna mmoja wenu atainuka kwenda kupaonesha ?

Kuna mmoja wenu amewahi kupaona kwa macho yake ?

Au ni Mtende wa ndotoni ?

Kitabu cha Qurani kikipelekwa mahakamani kuthibisha kinayo ya sema kitashindwa hata na magazeti haya yakawaida yanavyo toa habari zake.

Kitatupiliwa mbali kwa kuiongopea jamii ya dunia.
Quran 2:2
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu,

3.
Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa.

4.
Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo.

5.
Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa.

6.
Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini.

Kitabu chenyewe kinasema hakina shida yani wewe ndio mwenye shida sio Quran Yani wewe ndio punguani

Na ukikiuliza upunguani wako upo wapi kitakujibu hiyo Quran
 
Quran 2:2
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu,
Ata wewe unaweza ukaandika kitabu na ukasema hakina shaka

Embu jibuni basi mada mnarukaruka sana
 
Kwema Wakuu!

Kutokana na mjadala fulani uliokuwa unaendelea katika Jukwaa la Intelligence nimeona nianzishe uzi huu kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia kupima katika mizania ya kimahakama/kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.

Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?

Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi, bali nipo kujadili nani mkweli kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama, majaji mtakuwa ninyi wasomaji.

Mahakamani siyo kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa sheria, hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.

Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema kwa vile mambo haya yanagusa imani za watu jambo hilo linaweza kuwa gumu.

Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa rejea kuu zaidi ya Quran, kwa sababu;

1. Biblia kwa sehemu kubwa haina maneno ya 'Hearsay' wakati Quran kwa 90% maneno yake ni 'Hearsay'. Kimahakama maneno ya 'hearsay' hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu. Hoja hii ndiyo hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.

a) Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, Yona n.k.

Wakati msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo. Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita. Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.

Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, Mathayo na Yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu waliyoshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya. Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka kwa sababu yeye alisimuliwa.

Hata hivyo ulikuwa ni wakati ule ule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka. Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.

2. Waandishi wa Biblia walikuwepo maeneo tajwa kwenye Biblia, lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika maeneo anayoyasimulia. Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na Waisrael ambapo hajawahi kufika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.

Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman halafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman, wakati Suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.

Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia. Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.

3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.

Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo!😀😀

Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.

Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi kwasababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni kama vile kitabu cha Mzee wetu Mwinyi au Mzee wetu Mengi.

Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay), kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa ukweli na ikachukuliwa kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.

4. Biblia imeandikwa na Wayahudi kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu kwa lugha ya Kiarabu lakini inasimulia habari za wasiyo Waarabu, inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.

Yaani mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo. Hivi ninyi mtanisikiliza mimi Mpare ninayesimulia habari za kale za Wasukuma au mtasikiliza Wasukuma wenyewe?

Muhammad Muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo halafu yeye anakwambia alizaliwa kwenye mtende halafu kuna mtu Myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye hori la ng'ombe.

Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni Myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza nani?

Haya Quran na hadithi za Kiyahudi kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji wa Daudi na mwanaye Suleiman, hajui Kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.

Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini, lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo majini. Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika vitabu vyake vilivyopo katika Biblia? Jibu utabaki nalo.

5. Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa Waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah, Mungu wa Waarabu wa kabila la Wakurdi wa zamani lakini cha ajabu huyo Allah, ati huyo Allah kuna sehemu anamuagiza kina Musa (Myahudi na dini yake Uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.

Hata hivi leo Mungu wa Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu wa waarabu hajabadilika ni yule yule Allah. Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa Muarabu.

Wahusika kuanzia kwa Yakobo mpaka kwa Yesu ni Wayahudi na dini yao ni Uyahudi na Mungu wao ni Yahweh, lakini Quran imepuyanga katika eneo hilo.

6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran, siyo ajabu Quran yenyewe ndiyo imenakili baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.

Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndiyo baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovinakili kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya Kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile.

7. Mtiririko na visa na matukio ya Kihistoria.
Biblia ni kitabu ambacho kimeandikwa Kwa kufuata mtiririko wa visa na matukio unaoleweka. Kuanzia kisa cha Adamu mpaka Yusufu anachosimulia Musa, Kisha tawala za dunia kama Tawala la Nimrodi, kisha tawala la mafarao, kisha tawala la Waashuru na Wakaldayo, kisha wakafuata Waajemi na Wamedi, kisha wakafuata Wayunani/wagiriki, kisha wakafuata Warumi ndipo alipozaliwa Yesu.
Lakini Quran haina mtiririko wa visa na matukio, kumaanisha haiwezi kutumika hata shuleni Kama rejea za kihistoria kuhusu tawala, au mambo ya kuitawala au Kisiasa kwani Quran haijui wapi dunia imetoka ilipo na wapi inapoenda. Wakati Biblia inaeleza wapi Dunia ilipotoka na wapi ilipo na inapokwenda.

Quran inaweza kuulizwa swali, Yesu alizaliwa wakati WA utawala gani na wanani na ukashindwa kujibu?
Kimahakama Quran kama haijui baadhi ya taarifa muhimu kama Zama na Maeneo husika ya tukio lilipotukia haiwezi kutumika kama Rejea au ushahidi muhimu katika mambo ya Kidini.
Kwa mfano; Issa kazaliwa kwenye mtende Kwa mujibu wa Quran lakini haielezi ni eneo gani au nchi gani Issa alizaliwa, hata Hapa Tanzania ipo mitende, hii ni tofauti na Biblia inataja na kuelezea visa katika mtiririko uliokamilika.

Quran ambacho ingefanya ni kutoa nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na siyo kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo. Mbona Injili haujarudia visa? Quran haiwezi kuchukuliwa kama rejea kuu kuzidi Biblia kwa sababu nilizozitaja hapo juu.

Majaji mjadili kwa hoja.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Wewe uliye andika pia huna akili unacho kiandika hata hakieleweki kabisa nosense ulicho kiandika ni upuuuzi mtupukabisa.
 
Back
Top Bottom