Kama binadamu kuzaa kwa uchungu ni adhabu vipi kuhusu ng'ombe, mbuzi, nguruwe na wanyama wengine wanaozaa kwa uchungu?

Kama binadamu kuzaa kwa uchungu ni adhabu vipi kuhusu ng'ombe, mbuzi, nguruwe na wanyama wengine wanaozaa kwa uchungu?

Mungu anasema hivi katika kitabu cha Quran


Quran 90:4
Hakika tumemuumba mtu katika taabu.

Sura ya 46:15

"Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapo fika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu."
 
itoe Quran katika hilo.

Quran haikusema kuwa Mungu amempa adhabu mwanamke kuwa atazaa kwa uchungu.

Quran haikusema kuwa mwanaume kapewa adhabu ya kula kwa jasho

Nanukuu Quran sura ya 7:11-25

"Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.

Mwenyezi Mungu akasema (kumwambia Iblis): Nini kilicho kuzuia kumsujudia (Adam) nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo.

(Mungu) Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe (Iblis) u miongoni mwa walio duni.

(Iblis) Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa.


(Mungu) Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula (umri mrefu).

(Iblis) Akasema: Kwa kuwa (Mungu) umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.

Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani.


(Mungu) Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.


Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu.

Basi Shet'ani (iblis) aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele.

Naye (Iblis) akawaapia (Adam na mkewe) : Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini.

Basi (Iblis) akawateka (Adam na mkewe) kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri?

(Adam na mkewe) Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika.

Akasema: Teremkeni! Mtakuwa nyinyi kwa nyinyi maadui. Na kwenye ardhi itakuwa ndio makao yenu na starehe yenu mpaka ufike muda.

Akasema: Humo mtaishi, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa."
Porojo tu na hadithi za Abunuwasi
 
Unapaswa ujiulize wewe kuwa kwa nini haujui wanyama nao wanazaa kwa uchungu
Sasa ntajuaje wanazaa kwa uchungu!? Hayo maumivu anayahisi muhusika au !? Sisi tumefaham kwamba wanawake wanazaa kwa uchungu kwasababu tumeambiwa au tumehisi huo uchungu !?
 
Sasa mzee baba..Mungu s anatusisitiza kusamehe sasa Mbona kashindwa kuwasamehe viumbe vyake
Anasamehe kwa yule anayetaka kusamehemewa...Iblis alifanya kiburi cha kugoma kutii amri ya Mungu pale alipoamrishwa kumsujudia Adam (kwa kumpa heshima ya kuwa Adam kamzidi katika mtihani wa utambuzi na ujuzi wa vitu).

Iblis alivyokata amri ya Mungu hakutaka kuomba msamaha...bali aliomba apewe umri mrefu sana ili apate kuhakikisha anaviangamiza vizazi vyote vya Adam.

Ilihali Adam na Mkewe walivyomkosea Mola wao...waliomba msamaha na Toba...Wakasamehewa kosa lao.


Mungu ukiomba mkate hawezi akakupa jiwe au ukaomba Samaki akakupa nyoka...!!

Ibilis yeye kaona uhai mrefu ndio dili kwake na wala sio msamaha wa Mungu. Matokeo yake kahukumiwa kuingia Motoni. Hivyo yupo hai mpaka leo kuhakikisha anavuna kundi kubwa la kizazi cha Adam ili apate kuingia nao Motoni.
 
Qur'an 10.94
"Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka."


Isome vizuri hiyo aya ili usiinukuu nje ya maana yake halisi....Mungu anasema kuwa ikiwa unashaka juu ya haya tuliyokuretemshia (katika Quran) basi waulize wasomao kitabu kabla yako (Wanazuoni wa wana wa Israil waliosilimu na kuikubali Quran).

Quran 7:157

"Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.'"


Mfano mzuri Mtume Muhammad (s.a.w) alipohamia katika mji wa Madinah kutoka Makkah ,kulikuwa na mwanazuoni mkubwa wa kiyahudi aliyesilimu na kuingia katika Uislam jina lake aliitwa Abdullah ibn Salaam. Wayahudi walikuwa wakimtegemea huyu kama mwanazuoni mkubwa sana....ila aliingia katika uislam mara baada ya kusoma Taurat na kukuta Sifa za Mtume Muhammad ndani yake hivyo alivyoitambua haki moja kwa moja aliamua kuifuata.
 
Porojo tu na hadithi za Abunuwasi
MUNGU amewaelezea watu mfano wako kuwa ni watu ambao nyoyo zenu ziwekwa pazia,hivyo hamuwezi kuamini..Kiufupi wewe ni kiziwi japo kuwa unatembea huku ukisikia ila huna unachokielewa

Quran 6:25

"Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza; na tumezitia pazia nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi masikioni mwao, na wakiona kila Ishara hawaiamini. Hata wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema walio kufuru: Hizi si chochote ila hadithi za watu wa kale."
 
"Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka."


Isome vizuri hiyo aya ili usiinukuu nje ya maana yake halisi....Mungu anasema kuwa ikiwa unashaka juu ya haya tuliyokuretemshia (katika Quran) basi waulize wasomao kitabu kabla yako (Wanazuoni wa wana wa Israil waliosilimu na kuikubali Quran).

Quran 7:157

"Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.'"


Mfano mzuri Mtume Muhammad (s.a.w) alipohamia katika mji wa Madinah kutoka Makkah ,kulikuwa na mwanazuoni mkubwa wa kiyahudi aliyesilimu na kuingia katika Uislam jina lake aliitwa Abdullah ibn Salaam. Wayahudi walikuwa wakimtegemea huyu kama mwanazuoni mkubwa sana....ila aliingia katika uislam mara baada ya kusoma Taurat na kukuta Sifa za Mtume Muhammad ndani yake hivyo alivyoitambua haki moja kwa moja aliamua kuifuata.
Sikuhitaji maneno mengi mkuu
 
Mungu ameweka labor pain kwa hekima ,ujuzi na elimu yake...

Uchungu ndio hupelekea mwanamke aweze kusukuma mtoto atoke tumboni wala sio adhabu kwake na lazima asikie maumivu kwasababu maumbile ya mwanamke (uke) ni madogo kulinganisha na kichwa /mwili wa mtoto.
 
anaitwa mzazi kwa sababu kazaa, huwezi kusema mke wako kazaa utasema amejifungua, yule si ng'ombe, ng'ombe ndiye anazaa
Amejifungua linatumika tu ndani ya siku 30 tu mtu akitoka kuzaa

Sasa hivi hatuwezi kusema mama yako amejifungua wewe Loth hema ,tutasema mama yako alikuzaa wewe loth lema
 
Back
Top Bottom