Kama binadamu wa kwanza alikuwa mweupe, watu weusi wametoka wapi?

Kama binadamu wa kwanza alikuwa mweupe, watu weusi wametoka wapi?

waislam mko wapi? mjibu hoja maana jama wanataka ushahidi wa kimantiki saidieni hapo maana nyie ndio huwa mnasema duniani dini ni 1 tu uwislamu zilizo baki batiril haya wenye dini tuleteeni aya
 
kutokana na sabau za kijiografia mtu wa kwanza alipoumbwa alikaa sehem fulani na shemu zingine zilikua tupu hazina watu walipozaana ndio watu wakazagaa sehemu tofauti


kwanini watu weusi
jibu ni sabau za kijografia mfano africa imepitiwa na mstari wa ikweta mabara yaliyopitiwa na mstari huu yanakua na joto sana kwa hiyo sababu hzi zinapelekea ngozi kutengeneza melanini nyingi sana ukiangalia america ya kusini nchi kama venezuela ,brazili na peru watu ni weusi ukija africa watuu ni weusi ukienda indonesia malyasia na nk unapata watu weusi pia ila kadri watu wanapozagaa na ndio wanachanganya damu

Mi nadhani hiyo issue ipo beyond human knowledge. Africa kuna joto sana zaidi ya sehemu nyingine duniani sidhani kama ni kweli. (ukisema muda mwingi katika mwaka average temp ni kubwa hapo inawezekana ikawa ni sahihi)

Nimeishi TZ nilikuwa nasikia TZ joto, nikawa naamini hivyo. Nikaenda U.S state fulani hivi wakati summer imekolea, pale ndipo nilipogundua kwamba TZ hakuna joto kali tunaongopeana tu. Nikapita nchi moja ya kiarabu wakati wa majira ya jua ilikuwa ni balaa.

Hizo nchi kama venezuela,peru, brazil bado weupe ni wengi mno kulinganisha na weusi. Na ukifuatilia historia ya weusi utaambiwa waliletwa kama watumwa kwa ajili ya kulima.
 
Wewe ni Mungo sana, tena hufai kabisa wewe.

Niletee ushaidi wa rangi ya mtu wa kwanza kutoka hivyo vitabu vya dini unavyo visingizia.

Kwa mujibu wa biblia mtu wa kwanza kuwepo alikuwa yesu AMBAE kwa mujibu wa picha ZOOTE duniani na kwenye MAKANISA zinaonyesha NI MZUNGU!

Biblia inasema Yesu alikuwepo kabla ya chochote duniani!

Sasa tuulize hio biblia Mtu mweusi katoka wapi!?? Au sisi waafrika hatukutajwa kwenye biblia?
 
Kuna maandiko mengine yanasema mtu wa kwanza aliishi Tanzania (olduvai George) na waandishi wengine wanasema ni Ethiopia..

Hapa sijausisha biblia....

Wa kwanza ni mrangi kutoka kondoa irangi tanzania.
 
katika vitu ambavyo dini imeshindwa kuthibitisha kabisa ni ukweli kuhusu mwanadamu wa kwanza...historia ya dini inasema kwamba Adam alizaa watoto 2 kwanza ambao ni Kaini na Abel, Kaini akamuua Abeli na kulaaniwa , akafukuzwa kutoka ukoo wa Adam na kuhamia mbali ambapo ndipo alipoanzisha familia ya wafua vyuma wa kwanza duniani(blacksmiths) swali ni vipi alianzisha familia hiyo wakati huo hapakuwa na watu wengine zaidi ya Adamu, Eva kama mwanamke pekee, na kaini baada ya kifo cha Abel..kama alikoenda alikutana na watu na kuanzisha familia hiyo..watu hao waliumba na nani na lini? Je huoni kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kwamba Adamu na Eva sio wanadam wa Kwanza.

Kuna watu wanaamini kwamba Watu wa kwanza kuumbwa walikuwa ni Adam na Lilit. Lilit akagoma kuwa chini ya Adam akaondoka kwa Adam. Hapo ndipo akaletwa Eve/Hawa. Wanaamini Kaini alikokwenda alikutana na Lilit wakaendeleza kizazi chao cha watu wao.
 
Kwa mujibu wa vitabu vya dini mtu wa kwanza kuumbwa alikuwa ni Adamu kisha Eva ambao walikuwa sio watu weusi, ni nini kilitokea mpaka watu weusi wakatokea duniani?

Hizo ni kauli za BIBLIA! na SIO DINI ZOTE.
Na hata taswira zinazo sambazwa na Makanisa ni Taswira za KIZUNGU PEKE YAKE.

Hata Ktk Historia ya Uongozi wa VATICAN hakuna mtu mweusi Aliyewahi kuwa PAPA kwa zaidi ya Miaka 800. Ndio maana UKADHANI KILA Dini Ina msimamo huo huo.

Soma Historia utakuta ni completely opposite.

Mtu wa kwanza kuishi hapa Duniani HAKUWA MWEUPE! bali ni wa rangi mchanganyiko, yaani mfano wa (mix races).

Na UISLAMU Haujadili suala la ASILI YA RANGI ya ngozi ya Binaadamu kwa njia Uitakayo wewe Rather inataja Rangi ya ngozi ya mtu KAMA KITAMBULISHO.

Mfano:-

Kuna mtu alikwenda kumtafuta mtume Muhammad (rehama na amani ziwe juu yake) na hali ya kuwa HAMTAMBUI, maswahaba wakamwabia" ni yule pale mtu mweupe mwenye nywele nyingi!

Hicho ni KITAMBULISHO na sio UBORA wa mtu.
LKn hadithi hii wagalatia mara nyingi huitumia eti kuonyesha kuwa kwa waislamu mweupe ni mali.

Na Quraan imeongelea Suala la Mataifa na Makabila kwa kusema

QURAAN.

Al-hujiraat 43:13

Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane.
Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi.

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.

Hapo Tunaambiwa kuwa MBORA ktk wanaadamu mbele ya MUNGU ni yule MCHAMUNGU kuliko wenzake.

Na sio MWEUPE au MWEUSI.

Sasa labda Uwaulize WAKRISTO hili suala la RANGI YA NGOZI YA BINAADAMU wanaliongelea vipi.

Sasa tazama wagalatia watakavyoanza kurusha ngumi hewani.

Manake ukiwaambia ukweli tu! Ni tusi kubwa sana kwao.

I am waiting with my AK48!
 
Ndg.. Hakutakuwa na mabadiliko yoyote makubwa unayodhania,hawa wanasayansi kuna baadhi wameweza kuthibitisha lakini mengine hawajaweza na hii ni sawa na ile kurefuka kwa shingo la Twiga eti sababu anakula majani yaliyo juu katikati ya mti wakati akizaliwa mtoto anakuwa na umbile hilohilo la shingo kuwa ndefu(kala muda gani huyu). Vipi kuhusu waarabu Libya, Misri, Kuwait, Iran miaka nenda rudi wanapigwa na jua kuliko sisi fika South Africa -Port Elizabeth pale ambapo barafu inadondoka miaka dahali kabla hata hao wazungu hawategemei kuja walikuwepo wenyeji ambao ni weusi kama mimi mpaka leo. Amini usiamini hii nadharia ni mfu.

Ulivoonggelea hilo ka twiga tu nikajua basi huyu mtu hata biology kaishia form four nikimueleza hawezi kuelewa... Hilo la twiga halikuwahi kukubalika kwenye biology hizo ni story mnapiga mtaani afu mnadanganyana science imesema hivo, usiisingizie science.

Naomba tuishie hapa maana kama ulikimbia biology kuna terms nyingi napenda ningezitumia kukuelekeza sema hatutoelewana ila hii ni true science na hadi leo imetumika the same knowledge kwenye mambo mbalimbali na yakafanya kazi kuprove kabisa kua si uongo... ni kama kusema equation ya force=massxgravity hakuna mwenye kusema newton aliitoa wapi, sema tumeitumia kwenye science na imetengeneza mashine nyingi sana mnazotumia leo hii, hiyo ndio inastand kama proof kua ni kweli...

Sasa same thing kwa evolution na genetics, kwa hiyo knowledge watu mnaosema ni uongo imetumika kufanya vitu ambavo vipo hadi leo.. Ndo maana narudia hapa ka biology ulikimbia afu una faith tutapelekeshana hadi mwaka utaisha, just so u know nina faith pia, ila hii sayansi haina uongo
 
Kwa mujibu wa biblia mtu wa kwanza kuwepo alikuwa yesu AMBAE kwa mujibu wa picha ZOOTE duniani na kwenye MAKANISA zinaonyesha NI MZUNGU!

Biblia inasema Yesu alikuwepo kabla ya chochote duniani!

Sasa tuulize hio biblia Mtu mweusi katoka wapi!?? Au sisi waafrika hatukutajwa kwenye biblia?

Kwa hiyo unaamini zile picha ni za Yesu? hahaha duh..
usije ukawa ndo wale mnapigia magoti picha ile afu unaomba..
 
Kwa hiyo unaamini zile picha ni za Yesu? hahaha duh..
usije ukawa ndo wale mnapigia magoti picha ile afu unaomba..

Mkuu! ! !
Mi niabudu sanamu ya mzungu kavaa nepi?

Nitake radhi tafadhali sana. Tena sana!!
Sijawahi kutukanwa km hivi.
 
mi naamini kuna muumba. lakini uumbaji na sababu za uumbaji ni siri.
dini ni kulazimisha kuelewa siri hiyo.

theory ninayoipenda sisi, wadudu na wanyama wengine wote tulitolka kwenye sayari nyingine... tukiwa na program ya kuja kuzaliana hapa kwenye sayari hii.

dini ni jitihada za kuelewa siri ya tulikotoka. kwa hiyo kwangu mimi swali kubwa ni kwa nini safari ya kutuleta huku haikuruhusu blue print ya kule tulikotoka? dini tunakisiakisia tu jibu ndo maana ziko dini lukuki

Uko nami kwenye hili la siri ya uumbaji, ila uwalakini upo kwenye kutoka sayari nyingine kuja sayari tuliyomo. Je tuliletwa na nini, nguvu/ kani ipi ilitumika kutuleta hapa duniani?? Na kwann hatukuweza kuishi/kuzaliana hukohuko katika sayari asilia?? je tulipokewa na viumbe gani duniani?? ..Nina mengi sana ila hayo ni machache tu.
 
kwani unauhakika gani alikua mweupe???? Kwani kuna udongo mweupe
 
1.mimi nina amini kuwa mwanadamu wa kwanza alikuwa mweusi sababu ukisoma maandio utaona Mungu alifinyanga udongo kisha akapulizia pumnzi ndio mwanadamu aka kama alivyo sasa jiulize udogo ni rangi gani utapata jibu

2. Watu weupe wametokana na kizazi cha kaini baada ya kumuua ndugu yake Mungu alimlaani na kupigwa chapa ya muhuri ambayo ndio ngozi nyeupe, (ukirudi nyuma utangundua nyoka/ shetani aliwadanganya wakila tunda basi watajua mema na mabaya maana ake watakuwa na akili nyingi) ndio maana ngozi nyeupe ni werevu zaidi yetu sisi weusi.

NB: ndio maana wanasema fuvu la mtu wa kwanza limepatikana ngorongoro

Umechanganya habari mpaka imekuwa kichekesho, umesema mtu wa kwanza aliumbwa mwesi kutokana na udongo mweusi, kisha ukasema adam alikula tunda la ujuzi wa mema na mabaya ndo maana watu weupe wana akili sana, embu panga vizuri habari yako, inawezekana ukawa na habari nzuri ya kutueleza ila shida una haraka sana utafikiri uko ukweni.
 
Kwa mujibu wa vitabu vya dini mtu wa kwanza kuumbwa alikuwa ni Adamu kisha Eva ambao walikuwa sio watu weusi, ni nini kilitokea mpaka watu weusi wakatokea duniani?

Mkuu biblia haijaeleza Adamu/Eva walikuwa na rangi gani.

Biblia yangu niliyokuwa naitumia nikiwa shule ya msingi (nashangaa ni tofauti na hizi ninazoziona mtandaoni) ilikuwa inasema hivi:

Miaka kadhaa baada ya gharika baada ya Nuhu/Noah kufariki dunia nzima walikuwa wanatumia lugha moja.
Wakaanza kufuru za hapa na pale. Mkuu wao akasema sasa hivi dunia ni sisi na sisi ni wamoja na kwa hiyo tujenge mnara mrefu sana mpaka Mungu ashangae, aseme kwamba hawa watu nimewaumba lakini wakiamua kufanya kitu hawashindwi, na vilevile tusitawanyike mbali na mnara huu, yaani walitaka kumshangaza Mungu.
Wakati wanajenga huo mnara Mungu akawachanganya Lugha wakawa wote hawaongei tena lugha moja isipokuwa kila fungu na lugha yake, mmoja akimuagiza mwenzake lete jiwe yeye analeta maji, ikatokea mtafaruku na kutokuelewana kila kundi likatawanyika kivyake sehemu mbalimbali za dunia
.
 
Mkuu! ! !
Mi niabudu sanamu ya mzungu kavaa nepi?

Nitake radhi tafadhali sana. Tena sana!!
Sijawahi kutukanwa km hivi.
Sijasema unaabudu,mnaona ume-quote vibaya, we umesema yesu amechorwa kanisani kama mzungu, nikauliza kwa hiyo unaamini kua ile picha ni ya Yesu.. mbona swali rahisi sana kulijibu.. kama unaona hilo ni tusi una matatizo kichwani
 
Kwa hiyo unaamini zile picha ni za Yesu? hahaha duh..
usije ukawa ndo wale mnapigia magoti picha ile afu unaomba..

Mkuu! ! !
Mi niabudu sanamu ya mzungu kavaa nepi?

Nitake radhi tafadhali sana. Tena sana!!
Sijawahi kutukanwa km hivi.

Sijasema unaabudu,mnaona ume-quote vibaya, we umesema yesu amechorwa kanisani kama mzungu, nikauliza kwa hiyo unaamini kua ile picha ni ya Yesu.. mbona swali rahisi sana kulijibu.. kama unaona hilo ni tusi una matatizo kichwani

Mwenye matatizo kichwani ni babu yako!

We sio ulioanza kijichekesha hapa na kusema mi huenda nalipigia goti sanamu!?

Bloody sangara! Mtoto wa bata mlemavu.
 
Mwenye matatizo kichwani ni babu yako!

We sio ulioanza kijichekesha hapa na kusema mi huenda nalipigia goti sanamu!?

Bloody sangara! Mtoto wa bata mlemavu.

Mkuu ukisema matusi ninayomengi sema hua siyatoi... pale juu nimeuliza swali cha kufanya ungesema hapana, au question mark hukuiona? sasa ya babu yangu yanakuhusu nini? haha ati bloody sangara.. mtoto wa bata... am far better than u in everyway possible sio kiakili tu, poor guys! pole sana aisee... endelea kumwaga matusi hadi keyboard iharibike maana it doesn't hurt.. sanasana inaonyesha ulivo mjinga
 
Far more better than me!? Teh teh teh!
For what! Having a big butt or what!
Be specific young man.

Dont say things you dont mean it! .
They might bit ur backside!

Back to the topic now!

We si mgalatia!?
Na wagalatia wote wanaamini kuwa Mtu wa kwanza alikuwa Yesu!
na yesu mlioletewa na Wakoloni ni yule mzungu aliyevaa nepi kwenye msalaba.

Thats why a lot of you folks believe that the first human being was WHITE! which is a biig wooopy Lie!

kimlugo mlugo weee! Jenga hoja kwa Kiswahili unachokifahamu vyema.
 
evolution inaelezea jinsi watu tunavotofautiana, kuna mambo mengi sana ndani yake yanayofanya species aina moja kua na genes tofauti, mazingira ikiwa ni kitu mojawapo, mwili unatend kuadopt kulingana na mazingira, sasa kwa binadamu ambaye anakaa sehemu za joto, over period of years lazima changes zitokee mfano anakuwa na nywele fupi sana sababu hakai kwenye baridi, sasa mwili unakua exposed kwenye jua, hapo ndipo melanin inachukua kazi yake sasa, melanin inafanya ngozi yetu kua nyeusi ili kuweza kuishi bila kuhitaji vitu kama sunscreen ambao wenzetu weupe huzitumia sana wakati wa jua kali.... Hakuna kitu kama laana wala nini, its simply evolution tu

je waarabu nao mbona wanakaa kwenye joto na wana nywele ndefu na ni weupe?
 
Mi Nnavojua huu weusi tulionao laana hii...kipindi kile cha nuhu ,baada ya gharika kuna mtoto mmoja alimchungulia baba ake akiwa uchi akamcheka wengine wawili wakaenda kinyume nyume wakamfunika,NUhu akamlaani yule aliemchungulia kuwa 'utakuwa mtumwa wa ndugu zako'...na ndo haya mnayoyaona throughout history,slave trade ,neocolonialism,underdevelopment yani ilimradi wazungu wako mbele...ingekuwa genes and revolution basi tungeevolve kuwa wazungu au wao kuwa weusi...source ndo hyo apo ,nikipata andiko specific ntaweka hapa mjionee

Can you please give a bit explanations on what you just wrote? i will be pleased if you'll incoparate your arguments with relevant sources.
 
Back
Top Bottom