Huyu mzee anasaidiwa sana,nilisikikiza intvw ya Queen aliyofanyiwa na Soudy miaka kama minne iliyopita ila tatizo lake anapenda sana kamera,manake siku hiyo mpaka Queen Darleen alimtukana sana baba yake,sijui alikuwa yupo mtungi au kala kijiti.
Ila yote kwa yote sisi wanaume tuwajibike kwa matendo yetu,tunajua wengi hatuliziki na mwanamke mmoja sasa ikitokea umetia mimba we lea tu hata kisirisiri mkeo asijue,huku uswahilini kuna watoto lukuki ambao wapo tu wanasoma St Kayumba wakati baba zao wana hela nishamshudia mmoja,mama yake anauza supu ya kuku asubuhi mara nyingi huwa nanunuaga na mchana anakaanga kiepe,yule mama ana strugle sana kulea mtoto peke yake wakati baba yake yupo na anauwezo mkubwa tu.
Na hata ikitokea mmekorofishana na mke wako,haina haja ya kuhamishia hasira mpaka kwa watoto,timiza wajibu wako kwa watoto wako kama mwanaume,mengine muachie Mungu atakulipia kwani mwanaume hasusi so husiisusie familia yako,kesho watoto wanaweza wakatoboa ukapata aibu kama huyo mzee,manake wanaweza wakakuliza kama tusingefanikiwa ungetutafuta?.