Kama DPP haondolewi ofisini mpaka afanye makosa au awe na tatizo la kiafya, Rais kamuondoa katika mazingira gani?

Nimesoma mtandaoni kuhusu taratibu za kisheria zinazotakiwa kufuata ili kumuondoa DPP ofisini, ambapo sheria imetamka wazi kuwa DPP hapaswi kuondolewa ofisini isipokuwa tu kama ana tatizo la kiafya(illness) au amekwenda kinyume na maadili ya kazi.

Hata katika hili la kwenda kinyume na maadili ya kazi/ professional yake, Rais atapaswa kuunda tribunal kumchunguza kabla ya kumuondoa.

Sasa kama haya yana ukweli, Rais Samia amemuondoa DPP ofisini kwa kigezo gani?

Kama ana makosa, kwanini asichunguzwe kama sheria inavyotaka na badala yake anapewa ujaji?

Wanasheria tusaidieni kuhusu jambo hili.

Najaribu kuweka hicho kipande chenye hizo sheria kinachozunguka mitandaoni ila bado sijafanikiwa.
Kampandisha Cheo! JAji wa Mahakama Kuu anaweza hata kuhukumu kunyonga lakini DPP huo ubavy hana!
 
Ndio maana naomba wanasheria watusaidie kwani inawezekana huu ni muendelezo wa kuvunja sheria.
Hasomi alama za nyakati mteuzi
Mitandao ipaaze sauti haya yafikie kikomo
Ni kuandika na kupiga kelele kwenye mitandao habari zinawafikia
Katiba Mpya kwa Bunge lililopo ni kujidanganya
Kuna umuhimu wa kuvunja na kufuta kila kitu tuanze upya
Wateuliwa si Waungwana
Mama atulizane anapelekwa mbio sana
Kulikuwa na haja gani ya kubadilisha kuteua
Alipashwa asafishe wale wananchi wanawalaumu waliopendelewa kupewa vyeo kwa sababu ya faida ya mtu mmoja......

Yapo mengi ya kuzungumza humu lakini basi tu
Watawala wanatesa sana mioyo ya wengi
Mungu yupo
Tutapeleka hesabu zetu siku ikifika
 
Watanzania tumeshazoea kuona sheria na kanuni zikisiginwa kila siku (serikalini, kwenye vyama vyote vya siasa, michezoni etc) to the extent sasa ni kama tumezoea na kuona ni kawaida na sehemu ya maisha yetu.

Juzi kati tu hapa TFF imeahirisha mechi kwa masaa kadhaa KINYUME KABISA NA TARATIBU NA KANUNI, tena kwa kupokea SMS tu, ila watanzania wengi kwa kivuli cha ushabiki eti wanasema Yanga ndio wenye makosa na kwamba eti "walipaswa kutumia busara".

Hii kitu inatakiwa ianzie kwenye mindsets zetu. Otherwise watu wataendelea kusigina kanuni wakijua hakuna wa kuwafanya kitu and the best we can do ni kukimbilia kwenye social media na kulaumu/kutukana...nothing more na life litasonga
 
Hasomi alama za nyakati mteuzi. Mitandao ipaaze sauti haya yafikie kikomo. Ni kuandika na kupiga kelele kwenye mitandao habari zinawafikia
We need to do more. Hii strategy seems imeshafail
 
Nimesoma mtandaoni kuhusu taratibu za kisheria zinazotakiwa kufuata ili kumuondoa DPP ofisini, ambapo sheria imetamka wazi kuwa DPP hapaswi kuondolewa ofisini isipokuwa tu kama ana tatizo la kiafya(illness) au amekwenda kinyume na maadili ya kazi.

Hata katika hili la kwenda kinyume na maadili ya kazi/ professional yake, Rais atapaswa kuunda tribunal kumchunguza kabla ya kumuondoa.

Sasa kama haya yana ukweli, Rais Samia amemuondoa DPP ofisini kwa kigezo gani?

Kama ana makosa, kwanini asichunguzwe kama sheria inavyotaka na badala yake anapewa ujaji?

Wanasheria tusaidieni kuhusu jambo hili.

Najaribu kuweka hicho kipande chenye hizo sheria kinachozunguka mitandaoni ila bado sijafanikiwa.
Kwan Prof Assad alifanya kosa gani
 
Kisheria Samia hajakosea popote, ila Kiuongozi kakosea kwenye kumpa huyu jamaa ujaji

Ukisoma Sheria hiyo vizuri, inasema DPP anaweza kuondoka kama akiumwa au sababu nyingine zozote za kumfanya asiweze kutekeleza majukumu yake

Sasa DPP kwa mfano akichaguliwa kuwa rais atawezaje kwa mfano kutekeleza majukumu ya urais na uDPP?

DPP akiteuliwa ubalozi, atawezaje kufanya kazi ya ubalozi na uDPP?

Remember, sheria haijamuondolea DPP haki ya kuchaguliwa au kuteuliwa maana yake ni kwamba kama akiteuliwa na akskubali uteuzi basi uDPP ndo utakoma, kwa sababu ile requirement ya "sababu nyingine zitakazomfanya ashindwe kutekeleza majukumu ya uDPP itakuwa imepatikana kutokana na kuwa atakwenda kufanya kazi nyingine na hivyo hataweza kufanya uDPP"

Kisheria hao wanaolalama wamechemka kwenye ishu hii.

Alichokosea Samia ni kumpa huyu mtu ujaji, yaani utampaje mtu aliyeshiriki kwenye kukamua peza za watu isivyo haki Ujaji?.

Yaani huyu alimkamua mhanga wa utawala wa Magufuli kama Erick Kabendera pesa ya plea bargain, Utampaje ujaji mtu wa namna hii?
 
Nimesoma mtandaoni kuhusu taratibu za kisheria zinazotakiwa kufuata ili kumuondoa DPP ofisini, ambapo sheria imetamka wazi kuwa DPP hapaswi kuondolewa ofisini isipokuwa tu kama ana tatizo la kiafya(illness) au amekwenda kinyume na maadili ya kazi.

Hata katika hili la kwenda kinyume na maadili ya kazi/ professional yake, Rais atCa na badala yake anapewa ujaji?

Wanasheria tusaidieni kuhusu jambo hili.

Najaribu kuweka hicho kipande chenye hizo sheria kinachozunguka mitandaoni ila bado sijafanikiwa.
Mlivyomfukuza CAG hamkuyatambua haya? Maza kanyaga twende !! bado hao waliokuwa wanawachapa wananchi wasio na hatia fimbo na kuvamia Ma- hotel ya kitalii kusaka pesa.
 
Kisheria Samia hajakosea popote, ila Kiuongozi kakosea kwenye kumpa huyu jamaa ujaji

Ukisoma Sheria hiyo vizuri, inasema DPP anaweza kuondoka kama akiumwa au sababu nyingine zozote za kumfanya asiweze kutekeleza majukumu yake

Sasa DPP kwa mfano akichaguliwa kuwa rais atawezaje kwa mfano kutekeleza majukumu ya urais na uDPP?

DPP akiteuliwa ubalozi, atawezaje kufanya kazi ya ubalozi na uDPP?

Remember, sheria haijamuondolea DPP haki ya kuchaguliwa au kuteuliwa maana yake ni kwamba kama akiteuliwa na akskubali uteuzi basi uDPP ndo utakoma, kwa sababu ile requirement ya "sababu nyingine zitakazomfanya ashindwe kutekeleza majukumu ya uDPP itakuwa imepatikana kutokana na kuwa atakwenda kufanya kazi nyingine na hivyo hataweza kufanya uDPP"

Kisheria hao akina Kigogo wamechemka kwenye ishu hii.

Alichokosea Samia ni kumpa huyu mtu ujaji, yaani utampaje mtu aliyeshiriki kwenye kukamua peza za watu isivyo haki Ujaji?.

Yaani huyu alimkamua mhanga wa utawala wa Magufuli kama Erick Kabendera pesa ya plea bargain, Utampaje ujaji mtu wa namna hii?
Kwa kifupi Mama hayuko serious na anaendeleza baadhi ya mambo ya mtangulizi wake.
 
Ana kauli nzuri lakini mpaka sasa hajaonyesha jitihada za kubadili sheria yoyote kandamizi!

Magufuli mwanzoni alikuwa kama kitu kilichoko kinyume cha sheria anakitaka basi anavunja sheria waziwazi bila hofu na kukitekeleza, baada ya kelele kuwa nyingi kuwa anavunja sheria basi akaamua kuhalalisha mambo yake mabaya kwa kuyatungia sheria.

Sasa huwezi ku UNDO mambo mabaya yaliyoko kisheri kwa maagizo ya hapa na pale, bali solution ni kurekebisha Sheria, Na Samia hajafanya hilo hata moja.

Kuhusu kumlinganisha Samia na Magufuli, Samia ana nafuu kubwa kuliko Magufuli, Magufuli alikuwa hafai kabisa, ameiumiza nchi hii kupita kiasi!
 
Nimesoma mtandaoni kuhusu taratibu za kisheria zinazotakiwa kufuata ili kumuondoa DPP ofisini, ambapo sheria imetamka wazi kuwa DPP hapaswi kuondolewa ofisini isipokuwa tu kama ana tatizo la kiafya(illness) au amekwenda kinyume na maadili ya kazi.

Hata katika hili la kwenda kinyume na maadili ya kazi/ professional yake, Rais atapaswa kuunda tribunal kumchunguza kabla ya kumuondoa.

Sasa kama haya yana ukweli, Rais Samia amemuondoa DPP ofisini kwa kigezo gani?

Kama ana makosa, kwanini asichunguzwe kama sheria inavyotaka na badala yake anapewa ujaji?

Wanasheria tusaidieni kuhusu jambo hili.

Najaribu kuweka hicho kipande chenye hizo sheria kinachozunguka mitandaoni ila bado sijafanikiwa.
Amefanya kosa la kukaidi Amri ya kumtoa sethi na Rugemalira mahabusu
 
Sheria husika uliyorejea imesema DPP hawezi kuwa "removed" kwenye position hiyo tofauti na mazingira ulivyosema. Kilichofanyika amekuwa "Appointed" kwenda kwenye "position" nyingine. Ingawa katika hiyo "Appoinment" amaekuwa "removed" "indirectly" ni "legal technicalities" ambazo zinaweka "loop hole" ya kufanya kilichofanyika bila kuvunja sheria maana ku-"appoint" sio ku"removal" Ingawa katika utekezaji wa "appointment" kuna "indirect removal" uelewa wangu mdogo wa Sheria ni kiwa Sheria iliyoweka Ofisi ya DPPP haikuzia DPP kuwa "appointed".
Ninawasilisha.
 
Katiba inasemaje kuhusu nguvu ya rais, tuazie hapo ...vyote vilivochambuliwa kikatiba havina maana kwenye nguvu ya rais kikatiba...pengine samia katazama hilo

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom