Kisheria Samia hajakosea popote, ila Kiuongozi kakosea kwenye kumpa huyu jamaa ujaji
Ukisoma Sheria hiyo vizuri, inasema DPP anaweza kuondoka kama akiumwa au sababu nyingine zozote za kumfanya asiweze kutekeleza majukumu yake
Sasa DPP kwa mfano akichaguliwa kuwa rais atawezaje kwa mfano kutekeleza majukumu ya urais na uDPP?
DPP akiteuliwa ubalozi, atawezaje kufanya kazi ya ubalozi na uDPP?
Remember, sheria haijamuondolea DPP haki ya kuchaguliwa au kuteuliwa maana yake ni kwamba kama akiteuliwa na akskubali uteuzi basi uDPP ndo utakoma, kwa sababu ile requirement ya "sababu nyingine zitakazomfanya ashindwe kutekeleza majukumu ya uDPP itakuwa imepatikana kutokana na kuwa atakwenda kufanya kazi nyingine na hivyo hataweza kufanya uDPP"
Kisheria hao akina Kigogo wamechemka kwenye ishu hii.
Alichokosea Samia ni kumpa huyu mtu ujaji, yaani utampaje mtu aliyeshiriki kwenye kukamua peza za watu isivyo haki Ujaji?.
Yaani huyu alimkamua mhanga wa utawala wa Magufuli kama Erick Kabendera pesa ya plea bargain, Utampaje ujaji mtu wa namna hii?