Kama dunia inazunguka, kwanini miamba na milima haiporomoki? Na kwa nini bahari isimwage maji yake?

Mlaleo, kama kawaida maelezo rahisi sana yanaweza kusaidia kuelewa.

Kuhusu unyoya.

Unyoya wa ndege ni mwepesi na hivyo hupaa angani kirahisi zaidi hasa kunapokuwepo na upepo (extra force). Lakini katika chumba kisichokuwa na upepo unyoya ule unatua chini taratibu. Unyoya uliofuatilia wewe lazima ulikuwa unapulizwa na upepo na hii si kwa unyoya tu, kunapokuwepo na upepo mkali vitu vyepesi vitapaa mbali sana kwa nguvu ya upepo ule.

Kuhusu kivuli

Kivuli si kitu bali ni eneo mwanga ulipozibwa kupita. Kivuli unachokiona chini basi lazima mwanga wake unatoka juu au angle nyingine inayolenga chini. Inapotokea mwanga ule ukazuiwa na kitu basi eneo ambalo mwanga hautafika ndio kivuli. Kama unakiona kiko "chini" basi chanzo cha mwanga kiko "juu". Kama utakiona kiko "juu" basi chanzo cha mwanga kiko "chini". Kusema kivuli siku zote kiko chini labda kama hujawahi kuwasha tochi kuelekea darini katika chumba chenye giza alafu ukaweka mkono wako mbele yake.

Kuhusu moshi na gesi

Ziku zote hewa yenye joto/ya moto ni nyepesi kuliko hewa iliyopoa. Pia gesi zina uzito tofauti hivyo gesi fulani yaweza kuwa nzito zaidi ya nyingine. Tunaona kama moshi "unavutwa" juu lakini hii ni kawaida katika mfumo wa mpangilio wa uzito wa vimiminika (fluid). Katika fizikia gesi ni fluid pia na gesi nyingi zinaweza kubadilishwa kuwa liquid ndani ya shinikizo la kawaida la atmosphere ingawa pia baadhi ya gesi haziwezekani kuwa liquid katika shizikizo hilo la kawaida la atmosphere. Moshi ni mchanganyiko wa gesi na particles zinazotokana na kuunguzwa kitu fulani. Moshi kwa kawaida ni hewa ya moto hata particles hizo ndogo zilizomo ndani yake ni za moto pia na nyepesi sana. Kwa uzito kati ya moshi na hewa inayokuwa katika atmosphere, moshi ni mwepesi zaidi hivyo ni lazima ukae juu kabisa. Kama kanuni zilivyo basi katika atmosphere hii tuliyomo moshi kama "hot air" utaenda juu na cold air itabaki chini.

Mifano hai ya kanuni hizi ambazo sisi binadamu tumepata fursa kuzitumia kwa matumizi mbalimbali ni nyingi sana lakini rahisi kabisa na ya zamani unayoweza kuona ni zile hot air baloons kule mbugani na kwingineko. Baloon hili linakuwa na burner na hujazwa hewa ya moto na hivyo kulifanya liwe jepesi zaidi ya hewa katika atmosphere na matokeo ni kupaa juu. Hewa inapopoa basi baloon huanza kushuka chini taratibu na ukitaka lipae sharti uchome hewa zaidi.

Moshi unaweza kwenda chini?

Jua lina atmoshpere pia (Corona) . Hali katika atmosphere ya Jua ni ya kushangaza maana atmosphere yake ni yenye joto kali sana kuliko eneo la surface yake (Photosphere). Hii ina maana kitu kikiungua katika surface ya Jua moshi wake kamwe hauwezi kwenda juu maana juu yake kuna joto maradufu. Eneo la surface ya Jua (Photosphere) inakuwa na takribani 6,200 degrees centigrade wakati ile ya Corona inakuwa na takribani 500,000 degrees centigrade. Unaweza soma hapa kuhusu tofauti ya joto yake surface na atmosphere ya Jua.

Kwanini hewa yenye joto ni nyepesi zaidi?

Hewa ya moto ni nyepesi zaidi kwa kuwa haina density kubwa. Density ni sawa na Mass kugawa kwa Volume. (Density = Mass/Volume.) Hewa inapochomwa zile particle zake zinapata kinetic energy hivyo zinanza kuvibrate kwa kasi zaidi na kuachana. Kitendo hiki kinahitaji nafasi zaidi kwa kuwa kule ku-vibrate hakuwezi kufanyika katika nafasi finyu. Hii inasababisha Volume iongezeke kama kiasi cha gas ni kilekile (Constant Mass). Kulingana na formula hiyo Volume ikiongezeka basi Density inapungua (hewa inakuwa nyepesi zaidi).
 
Last edited by a moderator:

Sasa kwa mfano tuseme ile ndege kule juu igande isiende mbele wala nyuma kwa muda, je itaachwa au itaenda sawa na dunia?
 

Mkuu je ni kitu gani kinachoifanya dunia yenyewe ielee?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu je ni kitu gani kinachoifanya dunia yenyewe ielee?

Gravity ya Jua ndio inafanya Dunia pamoja na sayari nyingine zote ziwe hapo zilipo. Ni gravitational force iliyonyuma ya vitu hivi. Hata jua liko hapo pamoja na nyota nyingine zote katika galaxy tuliyomo kwa mvuto (gravity) wa super massive blackhole katikati ya Milkyway.
 

Asante kwa majib mazuri.
1.Je hizo sayari zimekaa kwa mpangilio kama tunavyoona kwenye vitabu au zipo zig zag
2.Hizo blackhole zina umuhim gan na zipo ngapi
3.Ina maana kila sayari ina blachhole
4.Wanasema huko ndani ya dunia kuna volcano inayochemka, Je unaizungumziaje iyo fact ukiihusisha na blackhole
Tuendelee kuelimishana.......!
 

Mkuu MWAMFUPE labda ungependa kupitia mada hii Ukweli wa kustaajabisha kuhusu nyota za angani niliwahi kuandika mambo mengi sana kuhusu nyota na sayari. Nina uhakika utapata majibu mazuri sana na unaweza kuuliza maswali tu.
 
Last edited by a moderator:
Je density ya kitu inabadilika?hapana
Si kweli kwamba density haibadiliki. Ukibadilisha jotoridi la kitu au mkandamizo, ujazo hubadilika na density hubadilika. Maji, kwa mfano, yanafikia density ya juu kabisa kwenye nyuzi 4.

Je volume ya kitu inabadilika?hapana
Si kweli kwamba ujazo wa kitu haubadili. Kwa baadhi ya sababu nilizojadili hapo juu.

Einstein's equation ... ambayo utaitumia kutafuta mass ya wave-particle behavior of light only.....
Si kweli kwamba mlinganyo huo wa Eistein hutumika kwenye tabia ya mwanga tu. Hiyo ni universal law inayo apply wakati wote japo huwa dhahiri zaidi kwenye chembechembe za maada.
 

Ukienda Nairobi tembelea Kenyatta conference center. Kuna mgahawa ghorofa ya mwisho ambao unazunguka. Ukiwa pale unakula au kunywa chai hutaona au kuhisi mzunguko huo. Utajikuta tu unatazama upande mwingine bila kujua imetokeaje. Japo kwa kweli huwezi kufananisha na dunia kwa kuwa ni mviringo lakini ni mfano tu wa dunia inapozunguka bila sisi kuhisi.
 
dats gud
 
wataalam wamejaribu kutoa elimu zao juu ya kuzunguka kwa dunia saw a sio watu wote wanaosoma habari hizi au wenye maswali gaya wako kiwango hicho vivo wanahitaji wapate mifano hai kwa majibu yao.
jiulizeni mchana na usiku vinatoka wapi? huwezi kusa mungu amaweka kitambaa kuleta Giza Bali in mzunguko was saysri katika mduare Universe dunia kulizunguka jua mwezi pia kulizunguka jua na vitu kama hivyo ndio sababu kuna kupatwa kwa mwezi na jua pia.
usisite kuuliza ukiwa na swali tulimsikiliza vzr mwl.
 

Nairobi mbali sana aende tu pale Golden jubilee tower karibu na PPF tower juu kabisa Kuna mgahawa unaitwa Akemi .ni revolving restaurant
 
Surprise rotational speed of earth surface is 1680 km/h. Kasi kubwa ajabu sihisi upepo mkali. Unless? What?
 

Mkuu Anheuser

Elewa ninachoongelea..

Niliposema mass haibadiliki na volume ni ile ile ni hivi

Ukichukua kitabu hapa duniani ukikipima weight utakayopata si ile utakayopata kwa kitabu hicho hicho ukiwa mwezini na sehemu nyingine kama sayari zingine huko...

Lakin mass ya hapa na ya kule ni ile ile kwa kitu hicho hicho..
Na hii husababishwa na gravity ...ukipima mass ya redio yako hapo kwako si ile utakayopata ukiwa mwezini japo mass ni ile ile...nadhani hapo umenielewa nilichokimaanisha...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Anheuser

Elewa ninachoongelea..
Mkuu Seanherms,

Nielewe ndio wakati unaandika vitu potofu????

Ukisema density ya kitu haibadiliki watu wakakukosoa sema kwanza ulikosea katika maelezo yako halafu jirekebishe.

Usiseme "elewa ninachoongelea." Nielewe nini wakati umepotoka?

Anyhow, mass sio uzito, na mass ya kitu huweza kubadilika. Na density pia hubadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…