Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mlaleo, kama kawaida maelezo rahisi sana yanaweza kusaidia kuelewa.Ulishawahi ufuatilia? kuna mmoja niliufuatilia hadi nikachoka mimi nilikuwa mdadisi sana utotoni... hata kivuli nilikuwa najaribu kukikimbia... hivi nacho vipi? maana kipo down nacho!
Kuna vitu kama Moto na Moshi huwa unavutwa juu tu au ndahani vitu visivyo na uzito au uzito mwepesi zaidi huvutwa juu?
Hata Gesi za aina nyingi hukimbilia juu
Kwa wale mliouliza kuhusu ndege kupaa na mtu kuruka kwenda juu
Ni kwamba dunia huzunguka na anga pamoja..yaani dunia inazunguka with the 'atmosphere'..kwa hiyo basi kama ndege ikiruka juu huwezi kusema inaweza kusimama pale pale ili dunia ikizunguka ijikute imefika ilipokua inaenda...hapana,itazunguna na dunia pamoja!!kwa hiyo ndio maana ndege inakua na spidi yake ili kuovertake dunia ambayo inaiforce kwenda nayo
Kuhusu kuruka ili ujikute kwingine labda kama utaruka na kuacha dunia na anga yake yani uende mbali kabisa na earth's gravity ili mzunguko wa dunia usiathiri eneo lako...
Nilikua MMU wakuu kule kukanisahaulisha intelijensia ya huku kidogo.
Mlaleo, kama kawaida maelezo rahisi sana yanaweza kusaidia kuelewa.
Kuhusu unyoya.
Unyoya wa ndege ni mwepesi na hivyo hupaa angani kirahisi zaidi hasa kunapokuwepo na upepo (extra force). Lakini katika chumba kisichokuwa na upepo unyoya ule unatua chini taratibu. Unyoya uliofuatilia wewe lazima ulikuwa unapulizwa na upepo na hii si kwa unyoya tu, kunapokuwepo na upepo mkali vitu vyepesi vitapaa mbali sana kwa nguvu ya upepo ule.
Kuhusu kivuli
Kivuli si kitu bali ni eneo mwanga ulipozibwa kupita. Kivuli unachokiona chini basi lazima mwanga wake unatoka juu au angle nyingine inayolenga chini. Inapotokea mwanga ule ukazuiwa na kitu basi eneo ambalo mwanga hautafika ndio kivuli. Kama unakiona kiko "chini" basi chanzo cha mwanga kiko "juu". Kama utakiona kiko "juu" basi chanzo cha mwanga kiko "chini". Kusema kivuli siku zote kiko chini labda kama hujawahi kuwasha tochi kuelekea darini katika chumba chenye giza alafu ukaweka mkono wako mbele yake.
Kuhusu moshi na gesi
Ziku zote hewa yenye joto/ya moto ni nyepesi kuliko hewa iliyopoa. Pia gesi zina uzito tofauti hivyo gesi fulani yaweza kuwa nzito zaidi ya nyingine. Tunaona kama moshi "unavutwa" juu lakini hii ni kawaida katika mfumo wa mpangilio wa uzito wa vimiminika (fluid). Katika fizikia gesi ni fluid pia na gesi nyingi zinaweza kubadilishwa kuwa liquid ndani ya shinikizo la kawaida la atmosphere ingawa pia baadhi ya gesi haziwezekani kuwa liquid katika shizikizo hilo la kawaida la atmosphere. Moshi ni mchanganyiko wa gesi na particles zinazotokana na kuunguzwa kitu fulani. Moshi kwa kawaida ni hewa ya moto hata particles hizo ndogo zilizomo ndani yake ni za moto pia na nyepesi sana. Kwa uzito kati ya moshi na hewa inayokuwa katika atmosphere, moshi ni mwepesi zaidi hivyo ni lazima ukae juu kabisa. Kama kanuni zilivyo basi katika atmosphere hii tuliyomo moshi kama "hot air" utaenda juu na cold air itabaki chini.
Mifano hai ya kanuni hizi ambazo sisi binadamu tumepata fursa kuzitumia kwa matumizi mbalimbali ni nyingi sana lakini rahisi kabisa na ya zamani unayoweza kuona ni zile hot air baloons kule mbugani na kwingineko. Baloon hili linakuwa na burner na hujazwa hewa ya moto na hivyo kulifanya liwe jepesi zaidi ya hewa katika atmosphere na matokeo ni kupaa juu. Hewa inapopoa basi baloon huanza kushuka chini taratibu na ukitaka lipae sharti uchome hewa zaidi.
Moshi unaweza kwenda chini?
Jua lina atmoshpere pia (Corona) . Hali katika atmosphere ya Jua ni ya kushangaza maana atmosphere yake ni yenye joto kali sana kuliko eneo la surface yake (Photosphere). Hii ina maana kitu kikiungua katika surface ya Jua moshi wake kamwe hauwezi kwenda juu maana juu yake kuna joto maradufu. Eneo la surface ya Jua (Photosphere) inakuwa na takribani 6,200 degrees centigrade wakati ile ya Corona inakuwa na takribani 500,000 degrees centigrade. Unaweza soma hapa kuhusu tofauti ya joto yake surface na atmosphere ya Jua.
Kwanini hewa yenye joto ni nyepesi zaidi?
Hewa ya moto ni nyepesi zaidi kwa kuwa haina density kubwa. Density ni sawa na Mass kugawa kwa Volume. (Density = Mass/Volume.) Hewa inapochomwa zile particle zake zinapata kinetic energy hivyo zinanza kuvibrate kwa kasi zaidi na kuachana. Kitendo hiki kinahitaji nafasi zaidi kwa kuwa kule ku-vibrate hakuwezi kufanyika katika nafasi finyu. Hii inasababisha Volume iongezeke kama kiasi cha gas ni kilekile (Constant Mass). Kulingana na formula hiyo Volume ikiongezeka basi Density inapungua (hewa inakuwa nyepesi zaidi).
Mkuu je ni kitu gani kinachoifanya dunia yenyewe ielee?
Gravity ya Jua ndio inafanya Dunia pamoja na sayari nyingine zote ziwe hapo zilipo. Ni gravitational force iliyonyuma ya vitu hivi. Hata jua liko hapo pamoja na nyota nyingine zote katika galaxy tuliyomo kwa mvuto (gravity) wa super massive blackhole katikati ya Milkyway.
Asante kwa majib mazuri.
1.Je hizo sayari zimekaa kwa mpangilio kama tunavyoona kwenye vitabu au zipo zig zag
2.Hizo blackhole zina umuhim gan na zipo ngapi
3.Ina maana kila sayari ina blachhole
4.Wanasema huko ndani ya dunia kuna volcano inayochemka, Je unaizungumziaje iyo fact ukiihusisha na blackhole
Tuendelee kuelimishana.......!
Si kweli kwamba density haibadiliki. Ukibadilisha jotoridi la kitu au mkandamizo, ujazo hubadilika na density hubadilika. Maji, kwa mfano, yanafikia density ya juu kabisa kwenye nyuzi 4.Je density ya kitu inabadilika?hapana
Si kweli kwamba ujazo wa kitu haubadili. Kwa baadhi ya sababu nilizojadili hapo juu.Je volume ya kitu inabadilika?hapana
Si kweli kwamba mlinganyo huo wa Eistein hutumika kwenye tabia ya mwanga tu. Hiyo ni universal law inayo apply wakati wote japo huwa dhahiri zaidi kwenye chembechembe za maada.Einstein's equation ... ambayo utaitumia kutafuta mass ya wave-particle behavior of light only.....
Kuna vitu vinanitatiza sana sijui ni sababu ya kutaka kujua kila kitu Mimi sio mtaalam wa Geography japo wakati nipo sekondari tu kwa nadharia na kuna concept inasema dunia huwa inazunguka au inajizungusha kwenye mhimili wake. Ila maswali ninayojiuliza inazunguka vipi? Na kwanini isifike kipindi leo tujione tupo upande huu kesho upande mwingine? au mwaka huu tupo upande huu mwaka kesho tupo upande mwingine.
Na pia pia kama inazunguka nilitegemea kwa hali ya kawaida kama unavyozungusha kitu chochote chenye maji kisicho na mfuniko maji yale yatamwagika lakini maji ya bahari mbona hayamwagiki? au ndio hiyo gravity? Na pia effect ya miamba na milima hainokeni labda kupomoka zaidi ya ile wanayosema plate movement kwenye Physical Geography.
Swali la msingi kama inazunguka Je, kwanini kila siku tunajiona tupo sehemu ileile?​
dats gudUkienda Nairobi tembelea Kenyatta conference center. Kuna mgahawa ghorofa ya mwisho ambao unazunguka. Ukiwa pale unakula au kunywa chai hutaona au kuhisi mzunguko huo. Utajikuta tu unatazama upande mwingine bila kujua imetokeaje. Japo kwa kweli huwezi kufananisha na dunia kwa kuwa ni mviringo lakini ni mfano tu wa dunia inapozunguka bila sisi kuhisi.
Ukienda Nairobi tembelea Kenyatta conference center. Kuna mgahawa ghorofa ya mwisho ambao unazunguka. Ukiwa pale unakula au kunywa chai hutaona au kuhisi mzunguko huo. Utajikuta tu unatazama upande mwingine bila kujua imetokeaje. Japo kwa kweli huwezi kufananisha na dunia kwa kuwa ni mviringo lakini ni mfano tu wa dunia inapozunguka bila sisi kuhisi.
What will happen kama dunia ikipoteza force of gravity;je vitu vitangukia wapi
Si kweli kwamba density haibadiliki. Ukibadilisha jotoridi la kitu au mkandamizo, ujazo hubadilika na density hubadilika. Maji, kwa mfano, yanafikia density ya juu kabisa kwenye nyuzi 4.
Si kweli kwamba ujazo wa kitu haubadili. Kwa baadhi ya sababu nilizojadili hapo juu.
Si kweli kwamba mlinganyo huo wa Eistein hutumika kwenye tabia ya mwanga tu. Hiyo ni universal law inayo apply wakati wote japo huwa dhahiri zaidi kwenye chembechembe za maada.
Mkuu Seanherms,