Kama huelewi ubaya wa Majimbo ya Lissu, angalia kinachoendelea Ethiopia

Huelewi chochote kuhusu Kenya.

Mauaji ya watu zaidi ya 1500 katika uchguzi wa 2007 kichocheo kikubwa ilikuwa ni huo umajimbo
Yaani mauaji ya kenya mwaka 2007 chanzo majimbo,kivip yan
 
Wala sitafuti uteuzi. Shida nyie mnaotafuta mnafikiri kila mtu anatafuta uteuzi. Kuna wale wanatafuta viti maalum hadi wamebakia na ukimwi. Ubinafsi ndio umetawala nyoyo zenu.
Wataje tu Boss
 
Tofautisha kati ya UKABILA na UJIMBO.

Waishio jimbo la TIGRE ni kabila hilohilo wanaizungumza TIGRINYA.

Negation: Kanda pendekezwa hapa Tanzania zinaundwa ba MAKABILA TOFAUTI.
LUGHA: KISWAHILI !! Lugha moja.

Hoja zingine mjitafutie FACTS kwanza na sio ushabiki wa tofauti za kisiasa na hata za kupuuzi zaidi za kidini na kikabila.
 
Kenya hakuna mikoa wewe kuna majimbo.

Walikuwa Na mikoa nane kabla ya katiba Mpya sahizi wanamajimbo mengi tu idadi kamili imenitoka but I reckon ni more than 35+ counties ambazo zote zina majimbo Na standing governments.
 
Ethiopia haijawahi kutawaliwa hauoni kama Ethiopia ni taifa kongwe kuliko USA?
Anajua hilo hata?

Unapozungumzia mataifa makongwe zaidi duniani huwezi iacha Ethiopia. Taifa lipo kabla hata yesu hajazaliwa!! Hata Suleiman nabii kaikuta Ethiopia Na imesimama mpaka Leo hafu unafananisha Na marekani ya juzi juzi tu hapa serious kabisa !!!
 
Marko 7:15: "Nothing that goes into someone from outside can make that person unclean; it is the things that come out of someone that make that person unclean."
 
SERIKALI ZA MAJIMBO NI NINI

Rafiki yangu aliniuliza kuhusu mfumo wa utawala/ wa majimbo ni nini? ,Alihoji hili baada ya kusikia sera za CHADEMA, kwamba wataanzisha utawala wa majimbo kupitia mgombea wake wa Uraisi TUNDU A. MUGWAI LISSU.

HAYA NI MAJIBU YANGU KWAKE:
  • Mfumo huu wa utawala wa majimbo siyo Mgeni hapa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla. Kabla ya mwaka 1962 nchi yetu ya Tanganyika ilikuwa pia na mfumo huu wa utawala wa majimbo, lakini mfumo huu ambao ulikuwa Tanganyika naweza kuuita ulikuwa ni mfumo wa utawala wa majimbo wa ulionzishwa na serikali ya kikoloni. Hata wenzetu Wengine Afrika, Kenya, Congo, Uganda nao pia walikuwa na mfumo huu wa majimbo, na baadhi ya nchi nyingi nyingine za Afrika.

  • Lakini kama ilivyo Tanganyika, nchi nyingi za Afrika ambazo zilikuwa na utawala wa majimbo ulikuwa ni mfumo uliowekwa na kuanzishwa na wakoloni.

  • Kwa kifupi utawala wa majimbo ni mfumo wa utawala wa kisiasa na kikatiba unaogawa Madaraka kutoka serikali kuu kwenda kwenye serikali za majimbo (Kwa Kikerewe au kijita tunasema to devolve power from central government to the provisional or state or county or city, or municipality, or federal government).

  • Mfumo huu wa utawala ni mfumo ambao unashare Madaraka baina ya majimbo na serikali kuu, lakini majimbo bado yanabaki kuwa chini ya uangalizi wa serikali kuu katika uangalizi wa jumla.

  • Mfano wa nchi zenye mfumo wa serikali ya majimbo ni MAREKANI (USA), INDIA, BRAZIL, MEXICO, RUSSIA, GERMAN, CANADA, SWITZERLAND, ARGENTINA, NIGERIA, PAKISTAN, AUSTRALIA, SOUTH AFRICA,ETHIOPIA,UNITED ARAB EMIRATES, AUSTRIA, MALAYSIA NA KENYA.

  • Mifumo hii katika nchi hizi zinatofautiana lakini lengo kubwa ni kupunguza Madaraka ya serikali Kuu kwenda kwenye serikali za majimbo( UNAWEZA KUSEMA UGATUZI WA MADARAKA).

  • Na mifumo hii inatofautiana kwa nchi na nchi maana sehemu nyingine wakuu wa majimbo hayo wanapigiwa kura na sehemu zingine wanateuliwa na Serikali Kuu, na wanakuwa na majukumu yao ya ndani yanayofanywa/kudhibitiwa na Bunge dogo la jimbo husika.

  • Pia katiba ya nchi ndiyo inapanga sasa shughuli mbalimbali zitakazokuwa na kutekelezwa chini ya jimbo na zile ztakzobaki kama shughuli au wajibu wa Serikali Kuu, Na hata vyanzo vya mapato vinagawanywa kati ya Serikali Kuu na Jimbo husika,

  • Kwa mujibu wa mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu, wao wanazungumzia Serikali za majimbo ambayo watu watakuwa na Madaraka ya kumpigia kura anayewaongoza katika majimbo husika.

  • Sasa huyo anayepigiwa kura na kuwa Mkuu wa jimbo mnaweza kumwita Gavana kama anavyoitwa USA, Kenya, Waziri Kiongozi kama anavyoitwa India.

  • Wenzetu Kenya wanaita County Government,

  • Mfumo huu unaopendekezwa na Chadema kupitia TUNDU ANTIPHASY MUGWAI LISSU unatofauti kumbwa na majimbo ya kikoloni sababu haya majimbo ya sasa yatakuwa ni majimbo ambayo watu wenyewe wanajiamulia nani awe kiongozi wao kwa kuwapigia kura, na kwamba hao wakuu wa majimbo watawajibika kwao moja kwa moja ( they will be accountable to the people).

  • Chadema wao wamependekeza kuanza na majimbo 10 , ikiwa wananchi wataridhia,,

  • Pia mfumo huu unaweka pia vyanzo tofauti vya mapato kati ya serikali kuu na Serikali za majimbo, kuna baadhi ya kodi haziwezi kutozwa na serikali za majimbo, zitatozwa na serikali kuu.

  • Kuundwa kwa mfumo huu hakuondoi wajibu wa serikali kuu kuzisaidia serikali za majimbo zinazo chechemea,,.na majimbo yanakuwa na uwezo wa kukopa,

  • Mfumo huu ndiyo ulioboresha na kukuza sana uchumi katika nchi nyingi duniani kama Australia, German, Marekani, Malaysia.
FAIDA ZA UTAWALA WA MAJIMBO:

  • Kupunguza Madaraka kwenye Serikali Kuu (kwa Raisi) na kuwapelekea wananchi wenyewe.

  • Kujenga ushindani wa kimaendeleo kati ya jimbo moja najimbo linguine ndani ya nchi moja.
  • Kuimarisha uzoefu wa kiuongozi kutoka katika serikali za kimajimbo ili kwenda kuutumia katika ngazi ya serikali Kuu, mfano George Bush na Bill Clinton kutoka Ugavana hadi kugombea Uraisi na kuwa Maraisi Marekani.
  • Kusogeza na Kuboresha Huduma za wananchi karibu.
  • Kubuni na kushughulikia mambo ambayo siyo lazima yashughulikiwe na Serikali kuu mfano kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo kutoka kwenye jimbo husika hadi kwenda majimbo mengine au kutoka jimbo husika kwenda nchi zingine. Hapa mfano Korosho Mtwara, Mawese Kigoma,Pamba Mwanza. Hii yote inatokana na upekee wa maeneo yetu Tanzania na Upekee wa mazao katika nchi yetu, huwezi kumtegemea Waziri mmoja wa biashara kutafuta masoko ya mazao yote nchi nzima, Badala yake serikali za kijimbo kupitia viongozi wake watatafuta masoko hayo,
  • Kusimamia huduma za mipango miji katika maeneo yao.Hati na mipangilio ya majimbo inapangwa na jimbo husika.
 
Post utopolo ya UVCCM hii, Congo, Somalia kuna majimbo ? Ambapo wanapigana vita.

Ebu angalia USA, KENYA penye majimbo kuna vita ?, migogoro ndani ya nchi sio sbb ya majimbo ni uongozi wa raisi dhaifu
Kenya na USA walitwangana wenyewe kwa wenyewe ndio wakaanzisha majimbo .Kikwete ndie alienda saidia kumaliza mapigano kenya wakaja na sera ya majimbo

Congo na Msumbiji kuna majimbo
 
Kenya na USA walitwangana wenyewe kwa wenyewe ndio wakaanzisha majimbo .Kikwete ndie alienda saidia kumaliza mapigano kenya wakaja na sera ya majimbo

Congo na Msumbiji kuna majimbo
USA kuna majimbo tangu 1776, kabla na baada ya uhuru,,
 
USA kuna majimbo tangu 1776, kabla na baada ya uhuru,,
Yaliazishwa baada ya Vita za wenyewe kwa wenyewe walipouana sana wakaamua kila bwana la Vita liwe na jimbo lake lenyewe kumaliza Vita
 
useless kushindwa uchaguzi kwa figisu ndio usema haitaji akili kubwa? wew bado akili ndogo tuu bado uko gizani
 
Kenya hakuna mikoa wewe kuna majimbo.

Walikuwa Na mikoa nane kabla ya katiba Mpya sahizi wanamajimbo mengi tu idadi kamili imenitoka but I reckon ni more than 35+ counties ambazo zote zina majimbo Na standing governments.
Umewahi kufanya au kujua hali ya maisha yao katika maeneo/majimbo yao kote?
 
Haiku- tawaliwa.

Hoja ni kwamba Marekani Ni Mazingira ila ni Europe ndio chimbuko la Maendelo yao.

90% ni wa kuja sio wazawa
Ebu lete chanzo cha uhakika chenye kuonyesha hilo kwamba chimbuko la maendeleo ya Marekani ni Ulaya.

Pili, kuna mifano mingi tu ya nchi zenye mfumo wa majimbo ambazo zina mazingira (siasa, ikolojia, utamaduni n.k.) sawa na Tanzania, ambazo hazina shida kama ya Ethiopia. Mfano, zimetajwa Afrika ya Kusini, Kenya, Botswana, Nigeria, Cameroon n.k.

Tatu, tatizo la Ethiopia ni 'complex' kuliko lilivorahisishwa na mleta mada: moja haswa ni dominance ya Tigrayan ambao si kabila kubwa ukilinganisha na Oromo na Amhara. Tigrayan walikuwa na mizizi mikubwa ndani ya dola iliyowapa kuhodhi uchumi mkubwa; sasa alipoingia Abiy Ahmed, amefanya kazi ya kufyekelea mbali dominance ya Tigrayan, ambao bado wanataka waendelee kuwa na nguvu kubwa za dola na uchumi.

Soma hapa upate kuelewa kidogo: https://foreignpolicy.com/2020/11/1...isnt-about-autonomy-its-about-economic-power/

Hapo majimbo hata hayahusiki. In fact wa Oromo na Amhara ndiyo walitaka kuwa na serikali za majimbo ili wawe na mamlaka kamili na kuepuka kuendeshwa na wa Tigrayan. Abiy Ahmed akiendelea, mbona ataweka mambo sawa tu.
 
Historia ni darasa. Hivyo siyo lazima na sisi tutwangane ili tuunde serikali za majimbo zenye mamlaka kamili.
Haswa kwa kuwa ni dhahiri mfumo wa uendeshaji serikali wa Tanzania umeshindwa kukabiliana na wale maadui wa maendeleo waliosemwa toka 1961.
 
Anajua sana tu sema wamepandikizwa upuuzi wa kutisha vichwani mwao
 
Kwani Tanzania hakuna Majimbo? Hao wabunge uliokuwa unawachagua walikuwa hawagombei kwenye majimbo? Kwanza Majimbo ya Lissu yatakuwa machache kuliko majimbo ya CCM. Leo tuna majimbo zaidi ya 200 wakati majimbo ya Lissu hayatazidi 20.
 
Pole
 
Historia ni darasa. Hivyo siyo lazima na sisi tutwangane ili tuunde serikali za majimbo zenye mamlaka kamili.
Haswa kwa kuwa ni dhahiri mfumo wa uendeshaji serikali wa Tanzania umeshindwa kukabiliana na wale maadui wa maendeleo waliosemwa toka 1961.
kote kilichosumbua ukabila na ubaguzi wa rangi. Tanzania huko tulishavuka ndio maana hatuhitaji majimbo. Hao wengine ikiwemo ubelgiji, marekani, Kenya, Nigeria, Afrika Kusini, Ghana, uingereza, nk
 
Kasema katiba ya Ethiopia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…