No hakuna jeshi ila kuna majeshi madogo kama mgambo au jeshi la maliasili
Kila jimbo linakua na Gavana wake ambaye amechaguliwa na wananchi wa eneo husika
Serikali za majimbo zinashabihiana kama ilivyo serikali ya Zanzibar yenye bunge (baraza la wawakilishi) baraza la mawaziri n.,k
Kuna faida na hasara Zake
Mfano Sisi watu wa kusini ( Lindi na Mtwara) pamoja na kua tunachangia kiasi kikubwa cha mapato ya nchi kutokana na gesi. Korosho. Ufuts n, k
Lakini Ndio sehemu pekee ambayo tunapewa pesa kidogo kutoka serikali kuu
Kusini mpaka Leo watoto wanasoma chini ya miti hakuna Barbara wala vituo vya afya
Kule kaskazini wenzetu kila baada ya hatua 20 sekondari na vyuo pamoja na vituo vya afya.. Lami mpaka mlangoni kijijini na mijini
Kama tungekua na serikali ya Majimbo Chato wasingepata uwanja wa ndege wenye hadhi ya kimataifa
Katika serikali kuu Rais wa federation.. hawezi kua Dikteta Heshima mtindo mmoja